Musa Mateja na Imelda Mtema
BAADA ya kula bata za
kutosha Bongo, wakati wakisindikizana kimahaba, staa wa Bongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mrembo mkali kutoka Uganda, Zarinah
Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, wamezua gumzo kwenye Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, Ijumaa lina mchapo kamili.
Mrembo
mkali kutoka Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady (mwenye
gauni jekundu) akishuka kutoka gari la ‘Diamond Platnumz’.
HABARI KAMILI
Tukio hilo lililoshuhudiwa na wanahabari wetu
lilijiri mishale ya mchana, Jumanne iliyopita katika maegesho ya airport
(uwanja wa ndege) ambapo Diamond alikuwa akimsindikiza Zari aliyekuwa
akitimua Bongo baada ya kufanya yao kwa siku kadhaa.
KABLA YA TUKIO
Awali kabla ya tukio
hilo, gazeti hili lilipokea ‘ubuyu’ kutoka kwa chanzo chake cha
kuaminika kwamba, wawili hao walikuwa wakijiandaa katika hoteli
waliyokuwa kwa siku kadhaa iliyopo kwenye Ufukwe wa Bahari ya Hindi,
tayari kuelekea uwanja wa ndege.
Zari au The Boss Lady akimwelekeza kitu mpambe wa 'Diomond'.
“Ijumaa acheni kulaza damu, kwa taarifa yenu Diamond ndiyo anajiandaa
kumpeleka Zari airport wahini pale mpate tukio kamili ili kumaliza
ubishi kuwa kweli walikuwa wote Bongo,” kilisema chanzo hicho kikiomba
hifadhi ya jina gazetini.
IJUMAA MZIGONI
Baada ya kunyetishiwa
ishu hiyo, wanahabari wetu walitia gia kwenye ‘motokaa’ ambapo dakika
kadhaa baadaye walikuwa wametega satelaiti zao uwanjani hapo tayari kwa
kunasa tukio.
Gari
jeusi aina ya BMW X6 ya mkali 'Diamond' ikiendeshwa na mpambe
wake aliyejulikana kwa jina la Q-Boy huku mwenyewe (Diamond) siti ya
nyuma.
BMW X6 LATOKEA
Wakati wanahabari wetu wakiwa wanakaribia kukata
tamaa, ghafla lilitokea gari jeusi aina ya BMW X6 ambalo tofauti na
magari mengine, badala ya namba za usajili, lenyewe lilikuwa na
maandishi yaliyosomeka kwa herufi kubwa ‘PLATNUMZ’ kisha likapaki kwenye
eneo la maegesho uwanjani hapo.
Gari hilo lilikuwa likiendeshwa na
kijana mmoja wa Diamond aliyejulikana kwa jina la Q-Boy na pembeni mwake
kwenye siti ya abiria alikuwepo mpambe mwingine wa msanii huyo ambaye
jina halikupatikana.
DIAMOND AJIFUNGIA
Wakiwa siti ya nyuma,
wakati Zari anashuka, Diamond alijifungia kwenye gari ili kuwakwepa
mapaparazi baada ya kuwashtukia kuwa walikuwa wakimsubiri.
Zari au The Boss Lady akisindikizwa na mpambe wa 'Diamond'.
WAZUA GUMZO
Wawili hao walizua gumzo uwanjani hapo ambapo baadhi
ya watu wakiwemo Wazungu walikuwa wakiwashangaa huku Wabongo wakitamani
Diamond atoke kwenye gari amtambulishe Zari kama ndiye mrithi wa Wema au
la!
“Huyu Diamond naye balaa. Kampata wapi
mtoto mrembo kiasi hiki? Hakyanani na mimi bora niwe msanii nitafaidi.
Mtoto kaumbika hasa,” alisikika mmoja wa madereva teksi huku wenzake
wakimkatisha tamaa kuwa hawezi kuwa msanii. Zari alishuka na yule mpambe
wa Diamond na kuambatana hadi sehemu ya kukaguliwa ili akapande ndege.
Zari, 'The Boss Lady' akilonga jambo na paparazi wa gazeti la Ijumaa.
IJUMAA LAMBANA ZARI
Kabla ya kufikia sehemu hiyo, wanahabari wetu
walibahatika kumfotoa picha za kutosha Zari kisha kumfuata na kumuuliza
alikuwa na ishu gani na Diamond ambaye alikuwa naye hotelini Bongo kwa
takriban siku tano.
Hata hivyo, Zari alishindwa kujibu na kuishia kusema kuwa hana
maoni.“No comment,” alisema Zari na hata alipoombwa kufafanuzi kidogo
aligoma.
DIAMOND AFUNGUKA
Baada ya tukio hilo,
wanahabari wetu walimtafuta Diamond kwa njia ya simu ili azungumzie kwa
kina juu ya uwepo wa Zari Bongo na tuhuma za kujihusisha naye kwenye
mapenzi ambapo Diamond alifunguka:
Mbongo Fleva 'Diamond' wakati akitanua na Zari, 'The Boss Lady'.
“Niliwaona airport mkimpiga picha na gari langu na mkaongea naye.
“Kweli ninyi ni noma sana, lakini nadhani mliandika hivi karibuni kuwa mimi nimeachwa na Wema (Sepetu).
“Ukweli hakuna mwanaume anayeweza kujitoa kwa demu wake hasa kumpatia
zawadi ya gari kama niliyotoa kwenye bethidei ya Wema halafu baadaye
usikie kuna mwanaume mwingine katoa zaidi na ukaendelea kufurahia.
ZARI NI RAFIKI TU JAMANI!
“Sitaki kuongea mengi ila Zari naomba atambulike kama rafiki yangu tu jamani.”
YATOKANAYO
Hivi karibuni Diamond alimwagana na Wema ambapo siku
chache baadaye habari zilivuja kwamba Zari ambaye ni msanii wa kike
tajiri Afrika Mashariki ndiye mwenye uwezo wa kuziba pengo hilo mara tu
baada kuonekana na jamaa huyo.