Habari Kali
Loading...

Mbabe wa unga ‘El Chapo’ anavyofanya Mexico hawalali… stori gerezani mambo yako hivi !!

Niligundua uzito wa ishu ya Joaquin “El Chapo” Guzman pale ambapo mpaka Rais wa Mexico, Rais Enrique Pena Nieto  alipost Tweet ya ushujaa wa kumkamata El Chapo !!
EL-CHAPO-III
Sasa leo ni kama siku ya tano hivi tokea El Chapo amekamatwa, kutoka ndani ya gereza la Altiplano Mexico ambako jamaa amefungwa kwa sasa, taarifa iliyonifikia ni kwamba ndani ya siku tano tayari kahamishwa kwenye vyumba nane tofauti ndani ya gereza ili kuhakikisha kama kuna mpango unasukwa kumtorosha basi usifanikiwe.
el chapo iii
Kingine ni kwamba sakafu za gereza zimeimarisha kuhakikisha mchezo wa kwanza kutoboa sakafu alioufanya miezi sita iliyopita haujirudii, vilevile kuna ulinzi zaidi ya kawaida, camera za CCTV zinamfatilia kwa kila sekunde kila anachokifanya.

MSHUKIWA WA MAUAJI YA WATU TISA KANISANI NCHINI MAREKANI AKAMATWA


Dylann Storm Roof baada ya kukamatwa na polisi.Roof akiwa chini ya ulinzi.Dylann Storm Roof akiwa ametiwa pingu.Roof akiwa na gari aina ya Hyundai alilokimbia nalo baada ya kutekeleza shambulio hilo.....Akipelekwa uwanja wa ndege kusafirishwa.....Akipandishwa kwenye ndege.Waumini wa Kanisa la Methodist wakifanya maombi, siku ya shambulio.Polisi wakiwa katika doria.Muonekano wa Kanisa la Merthodist.Kijana wa miaka tisa, Liam Ellern akisaidia kutoa maua kwenye mlango wa kanisa hilo.Wahanga wakiwa katika hali ya sintofahamu mara baada ya shambulio hilo kutokea.Waumini wakiwa katika majonzi.
Carolina Kaskazini, Marekani
JESHI la ulinzi la Marekani limemkamata mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika Kanisa la Methodist la kihistoria mjini Carolina Kusini, Dylann Storm Roof, na kumpeleka gerezani kusubiri kufunguliwa mashtaka yanayomkabiri.
Vyombo vya usalama vya Marekani vinasema, Bw. Roof mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa huko Selby Carolina Kaskazini umbali wa maili 250 kutoka eneo ambapo shambulizi hilo lilitekelezwa (Kanisa la Methodist) saa 13 baada ya shambulizi kabla ya kupandishwa ndege na kupelekwa mahabusu.
Maofisa wa Polisi wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami kwa bunduki aliketi katika mkutano wa mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja kabla ya kufyatua risasi na kuwaua wanawake sita na wanaume watatu akiwemo mchungaji wa kanisa hilo usiku Jumatano.
Maofisa wamelitaja shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki na ubaguzi wa rangi.
Aidha Mwanasheria Mkuu Bi. Lorreta Lynch, amesema Idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini mwafaka ya kumfungulia mashtaka mshukiwa.
Roof alitekeleza shambulio hilo ndani ya kanisa la Emmanuel African Methodist Church maarufu kama AME, kanisa linaloaminika kuwa la zamani zaidi linalotumiwa na watu wa asili ya Afrika nchini Marekani na kuwaua watu tisa wakiwemo wanawake sita na wanaume watatu miongoni mwao akiwa ni mchungaji wa kanisa hilo, Clementa Pinckney.
CHANZO NA DAILY MAIL

POLISI WAFUNGULIWA MASHTAKA BALTIMORE

Meya wa jimbo la Baltimore nchini Marekani Stephanie Rawlings-Blake.
Maandamano yaliyofanywa katika jimbo hilo.
Meya wa Mji wa Baltimore nchini Marekani, Stephanie Rawlings-Blake, amesema kuwa amehudhunishwa na kuvunjwa moyo baada ya polisi sita kushtakiwa, kufuatia kifo cha mwananaume mweusi, Freddie Gray.Polisi mmoja anakabiliwa na mashtaka ya mauaji huku wengine watano wakikabiliwa na mashtaka ya kuua bila kukusudia.
Tangazo hilo lilisababisha watu kusherehekea kwenye mji wa Baltimore lakini wengine waliiendelea kuandamana.Wakili anayewakilisha chama cha polisi katika mji huo, alilaani kile alichokitaja kuwa kuharakisha katika kuwafungulia mashtaka polisi hao.
Rais wa Marekani Barack Obama anasema kuwa, ni muhimu uchunguzi wa kina ukafanyika ili kubainisha ukweli kuhusu kile kilichosababisha kifo cha Bw. Gray.
CHANZO: BBC

JESHI LA NIGERIA LAWAOKOA MATEKA 293 WA BOKO HARAM


Jeshi la Nigeria likishambulia ngome za Boko Haram katika msitu wa Sambisa.
Wanajeshi wa Nigeria wakiimaklisha ulinzi dhidi ya Boko Haram nchini humo.
Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa wasichana 293 kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko katika msitu wa Sambisa, Kaskazini-Mashariki mwa nchi hiyo. Jeshi hilo limesema kuwa, wasichana hao waliokolewa siyo wale waliotekwa na kundi hilo mwaka jana katika eneo la Chibok.
Akizungumza na vyombo vya habari, msemaji wa Jeshi limeiambia limeongea na vyombo vya habari kwamba, wanawake na wanawake na wasichana hao walikutwa katika kambi nne tofauti Boko Haram ambapo silaha pia zimekamatwa, ameongeza kuwa, Jeshi liliwapata mateka hao baada ya kuzivamia na kuzishambulia kambi kisha kufanikiwa kuwaokoa.
"Ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu." Alisema kiongozi huyo.
Kwa sasa Jeshi limezuiwa kutoa kuweka wazi majina ya mateka hao waliookolewa kusisitiza kuwa wasichana hao siyo wale wanafunzi waliotekwa katika mji wa Chibok mwaka jana.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria alisisitiza kwa kusema, "Tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote."
 NA BBC

MORSI JELA MIAKA 20


Mohammed Mosri.
Aliyekuwa Rais wa Misri, Mohammed Mosri amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kuwachochoea wafuasi wa kundi la Muslim Brotherhood kuwaua waandamanaji wa upinzani alipokuwa madarakani mwaka 2012.

MWILI WA KAMANDA WA ISIS WAKABIDHIWA KWA WIZARA YA AFYA YA IRAQ LEO

Mwili wa marehemu Izzat Ibrahim al-Douri baada ya kukabidhiwa kwa Wizara ya Afya, Baghdad leo.
Izzat Ibrahim al-Douri enzi za uhai wake.
Maofisa wa jeshi wakiwa wamebeba mwili wa Izzat.
Wanaharakati wakiangalia mwili huo, huku wanahabari wakichukua picha.
SERIKALI ya Iraq leo imekabidhi mwili wa Izzat Ibrahim al-Douri (72) kwa wizara ya Afya ya Iraq  kwa uchunguzi zaidi.
Mwili huo ulitembezwa katika gari kwenye mitaa mbalimbali na kuonyeshwa moja kwa moja na Televisioni ya Irag.
Izzat alikuwa mfuasi wa Saddam Hussein na alikuwa Kamanda wa Kundi la ISIS na aliuawa katika mapigano na majeshi ya serikali kwenye Mji wa Tikrit, siku ya Ijumaa.
Marehemu Izzat ameacha watoto sita ambao ni Ibrahim al-Douri, Abla al-Douri, Ahmed al-Douri, Hamraa' al-Douri, Ali al-Douri, Houzan al-Douri

NHLANHLA NCIZA WA MAFIKIZOLO KUSAIDIA WAHANGA WA VURUGU AFRIKA KUSINI

Nhlanhla Nciza.
MMOJA wa wanamuziki wanaounda Kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini, Nhlanhla Nciza, ametangaza uamuzi wake wa kusaidia familia zilizokimbia makazi yao kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo.
Vurugu zikiendelea katika Mji wa Durban, Afrika Kusini.
Ni wiki ya pili sasa tangu Afrika Kusini ikumbwe na vurugu zinazoambatana na mauaji zinazosababishwa na makundi ya watu wenye silaha ambayo yanawalaumu wahamiaji wa Kiafrika kwa kuchukua kazi zao.
Nhlanhla amelaani mauaji hayo na kupitia akaunti yake ya Instagram hivi karibuni amewaomba mashabiki wake, marafiki na wengine wote kuungana katika kuwasaidia wahanga wa vurugu hizo zinazoendelea.
Rais nchi hiyo, Jacob Zuma amesitisha ziara yake ya nchini Indonesia ili kukabiliana na vurugu hizo huku akiwatembelea watu walioathirika.


WABONGO SAUZI SI SALAMA

INATISHA! Huku Wabongo wengi wakiendelea kukimbilia Afrika Kusini (Sauzi) kwa kigezo cha kutafuta maisha mazuri, imethibitika kwamba hali ya amani nchini humo si salama.
Wahamiaji wakionekana kujiokoa pamoja na watoto wao.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kutoka nchini humo, Wabongo wengi na wageni wengine kutoka nchi tofautitofauti Afrika kama Zimbabwe, Botswana, Namibia na nchi nyingine wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya kikatili na hata kuuawa na wenyeji wa nchi hiyo wakidai wanawakosesha ajira.
“Jamani hali inatisha sana huku, wageni tunauawa sana, wengine wanachomwa moto na kuchomwa visu hadharani, hakuna amani tena,” alisema Mbongo mmoja anayeishi nchini humo.Chanzo kiliendelea kudadavua kwamba Waafrika Kusini wanachukizwa na wageni hao kwani wamekuwa wakipokea ajira kutoka kwa matajiri kiasi kwamba wao wameonekana hawafai kwani wengi hawataki kazi ngumu tofauti na ilivyo kwa wageni ambao hupiga kazi yoyote bila kujali ugumu wa kazi.
Wahamiaji wakiwa kwenye hifadhi baada ya kukimbia machafuko.
Imeelezwa kuwa usalama wa wageni nchini humo umekuwa mdogo mno kiasi kwamba wengine wamekuwa wakijificha ndani kwa wiki nzima pasipo kutoka nje kwa kuhofia kuuawa na wenyeji ambao wamekuwa wakirandaranda mitaani kuwatafuta wageni ili wawadhuru.
“Sijatoka nyumbani wiki nzima, nipo nimejifungia tu, hata kwenda kununua chakula inakuwa ngumu sana, jamani, chondechonde waambie Watanzania wasikimbilie huku, hali inatisha sana,” kilisema chanzo chetu.
Mara baada ya kusambaa kwa taarifa za mauaji yanayoendelea kutokea Afrika Kusini, Watanzania wengi wameonekana kukasirishwa na kitendo hicho hivyo kukemea vikali mauaji hayo.
“Hii siyo fair kabisa, sifurahii kuona ndugu zetu wakiuawa huko, naomba warudi nyumbani na hata sisi tuliokuwa hapa nyumbani tutulie tu kwani maisha popote pale,” alisema kijana mmoja aishiye Manzese Midizini.

Hali Bado Ni Tete Kenya....Mapigano Kati Ya Jeshi Na Al Shabaab Bado Yanaendelea Katika Chuo Kikuu Cha Garrissa ambapo Wanafunzi 15 Wameuawa


Takriban watu 15 wanaodaiwa kufunika nyuso zao wameshambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
 
Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.

Kufuatia shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ,Shirika la msalaba mwekundu Red Cross limewataka raia wa Garissa kutoa msaada wa damu.
 
Walioitikia wito huo tayari wameeleka katika hospitali kuu ya Garissa mbapo kituo cha kutoa damu kimeanzishwa chini ya mti.

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa Collins Wetangula amesema kuwa wakati wapiganaji hao walipoingia katika nyumba anayolala aliwasikia wakifungua milango na kuwauliza watu iwapo ni waislamu ama wakristo.
 
''Kama wewe ni mkristo unapigwa risasi papo hapo.Kila mlio wa risasi nilipousikia nilidhani nitauawa'',ameliambia shirika la habari la AP.
 
Amesema kwamba maafisa wa usalama baadaye waliingia kupitia dirisha moja na kumtoa yeye na wenzake hadi katika eneo salama.

Mwandishi wa habari wa Kenya Dennis Okari ambaye yuko katika eneo la chuo kikuu cha Garissa ameandika katika mtandao wake wa Twitter akisema kuwa:
 
Wapiganaji hao wako katika jumba la kulala wanafunzi .''Ninaweza kusikia milio ya risasi kutoka upande wa pili.@ntvkenya"

Hali ni Mbaya Kenya...Al Shabaab Wanadaiwa Kuanza Kuwachinja Mateka Inayowashikila Katika Jengo La Chuo Kikuu Cha Garissa

Baadhi ya wanafunzi waliouawa au kujeruhiwa darasani
**********  
Katika style kama ile ya shambulizi la Westgate Mall, wanamgambo wa al-Shabaab wamevamia na kushambulia  chuo  kikuu  cha  Garissa kilichopo katika mji wa Garissa. Zaidi  ya watu 15 wameuawa, na wengine zaidi ya 53 wamejeruhiwa.

Mkuu wa jeshi la polisi Kenya, Inspector General Joseph Boinnet amesema kuwa magaidi hao walivamia geti kuu la chuo hicho na kuwarushia risasi walinzi alfajiri saa 5.30, wakati wanafunzi wa Kiislam wakienda kwenye swala ya asubuhi.
 
Polisi waliokuwepo chuoni hapo walikimbilia katika eneo la tukio na kuanza kurushiana risasi na magaidi hao, ambao walifanikiwa kuingia kwenye mabweni ya wanafunzi.

Polisi wa ziada na wanajeshi waliitwa kuja kusaidia na mirindimo ya risasi ilisikika kati ya wavamizi hao, polisi na wanajeshi.
 
Wanafunzi waliokuwa wakipiga simu kutoka ndani ya mabweni wamesema kuwa kuna majeruhi wengi sana. 
 
Wanafunzi waliofanikiwa kutoroka wamesema kuwa idadi ya wavamizi hao ni angalau watano  na bado kuna wanafunzi na maprofesa wengi wanashikiliwa mateka.

Taarifa za hivi punde zinaarifu kuwa magaidi hao wameanza kuwachinja baadhi ya mateka waliowashikilia.
 
Mateka mmoja (mwanafunzi) mwenye asili ya Somalia aliyeachiwa huru na magaidi hao ameviambia vyombo vya habari vya Kenya kuwa wanafunzi kadhaa wamekwishauawa na miili yao imetapakaa ndani ya vyumba na madarasa huku zoezi la Uchinjaji wa mateka wengine walio hai likianza.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametuma salamu za rambi rambi kwa familia za wale waliouawa katika shambulizi hilo.

Kenyatta amewataka wakenya kuwa watulivu wakati huu ambapo maafisa wa usalama wanakabiliana na wapiganaji hao. 
Wanajeshi wa jeshi la Kenya katika geti la chuo hicho

Baadhi ya miili ya marehemu waliouawa katika shambulio la al-Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa


Helicopter ya jeshi ikitua na maiti na baadhi ya majeruhi katika kambi ya jeshi la Langata


Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Excel, iliopo karibu na chuo kikuu cha Garissa wakiondolewa kutoka shuleni kuhakikisha usalama wao

Breaking News: Magaidi Wavamia Chuo Kikuu Cha Garrisa Kenya......Waliofariki mpaka sasa ni 15


Takriban watu 15 wameuawa baada ya watu watano wanaodaiwa kufinika nyuso zao kushambulia chuo kikuu cha Garrissa Kaskazini mashariki mwa Kenya.
 
Watu hao wanadaiwa kuingia katika taasisi hiyo mwendo wa saa kumi asubuhi wakati ambapo waislamu walikuwa wakifanya sala yao ya alfajiri.
 
Hatahivyo maafisa wa polisi wanasema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mwendo wa saa kumi na moja unusu.
 
Taarifa  zaidi  zinaarifu  kuwa walinzi wawili waliuawa katika lango la chuo hicho huku maafisa wawili wa polisi waliokuwa wakilinda chuo hicho pamoja na wanafunzi wakijeruhiwa.
 
Walioshuhudia wanasema kuwa kumekuwa na majeruhi mengi ndani ya chuo hicho.Wapiganaji hao bado wako ndani ya chuo hicho na wamewateka nyara watu kadhaa.
 
Jeshi la Kenya KDF ,maafisa wa polisi na amabulansi wamefika katika eneo la tukio na sasa wameingia ndani ya majengo ya chuo hicho ambapo kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya washambuliaji na maafisa wa jeshi.
 
Wanafunzi 27 wamefanikiwa kutoroka na sasa wako katika kituo kimoja cha kijeshi.
 
Kufikia sasa hakuna kundi ambalo limekiri kutekeleza shambulizi hilo ijapokuwa kundi la wapiganaji wa Somalia Al Shabaab limeshukiwa kutekeleza shambulizi hilo.
 
Chuo hicho ndio taasisi ya kipekee ya masomo ya juu katika eneo hilo kilichofunguliwa mwaka 2011 na kiko takriban kilomita 350 kutoka mji mkuu wa Nairobi.

JAJI AKUBALI RUFAA DHIDI YA OSCAR PISTORIUS


Mwanariadha Oscar Pistorius.
MAHAKAMA nchini Afrika Kusini imemruhusu kiongozi wa mashitaka, Gerrie Nel kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Oscar Pistorius baada ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.

Kiongozi wa Mashitaka, Gerrie Nel.
Kesi hiyo, sasa itaanza kusikiliza katika mahakama ya juu zaidi upande wa mashitaka ukitaka Pistorius ahukumiwe kwa kumuua mpenzi wake kwa makusudi.
Jaji Thokozile Masipa aliyemhukumu Pistorius, alisema hataruhusu rufaa dhidi ya hukumu hiyo aliyoitoa ya miaka mitano dhidi ya Oscar mwezi Oktoba mwaka huu.
Gerrie Nel aliiambia mahakama kuwa hukumu hiyo ni ndogo sana ikilinganishwa na kosa la alilolifanya mwanariadha huyo maarufu wa Afrika Kusini.

MSHINDI WA BBA HOTSHOTS APOKELEWA KWA KISHINDO JIJINI DAR

Mshindi wa zaidi ya milioni 500 za shindano la Big Brother Hotshots, Idris Sultan (katikati) baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.
Mama yake Idris Sultan, Naima Idris  akimpokea mtoto wake.
Idris akiongea na waandishi wa habari.
...Waandishi wakichukua picha.
Waandishi wa habari na baadhi ya ndugu na marafiki wakimsubiri.
Msafara ukiondoka Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Idris akiwasili katika Hyatt Regency Dar Es Salaam aliyofikia baada ya kutoka Sauz.
Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top