Habari Kali
Loading...

Lulu Awaogopa Wachawi Kutaja Baba Kijacho Wake


Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa anaogopa wachawi kumtaja mhusika wa mimba aliyonayo.
 
Lulu alifunguka hayo juzikati wakati mwanahabari wa GPL alipotaka kujua mhusika wa mzigo alionao ndipo msanii huyo aliposema aachwe kwanza maana wachawi ni wengi.
 
“Mh! Naomba mniache kwanza maana mjini hapa wachawi ni wengi, mambo yakiwa freshi kila mmoja atamjua,” alisema Lulu. 

Lulu Michael Kawa Mtamu Chuoni.....Wanafunzi wampongeza


Mrembo na mwigizaji wa filamu,  Elizabeth Michael ‘Lulu’ ,  ambae kwa sasa ameamua kupiga kitabu , anadaiwa kuwafunika kimasomo wanafunzi wenzake katika Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) kilichopo Magogoni-Posta jijini Dar.
 
Akizungumza hivi karibuni chuoni hapo, mmoja wa wanafunzi wanaosoma na mwigizaji huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema Lulu amekuwa akihudhuria vizuri darasani na kufanya vyema kwenye masomo yake mbalimbali zaidi ya wanafunzi wengi anaosoma nao.

“Lulu yupo vizuri sana kimasomo, anawapita hadi wanafunzi wengine. Mahudhurio yake ni mazuri na anafanya mitihani yake na kufaulu.
 
“Anavaa nguo zinazostahili na hapa chuoni kila mwanafunzi anampenda kwa sababu yupo ‘peace’ ile mbaya,” alisema mnyetishaji huyo na kusisitiza kuwa msanii huyo haishi kama supastaa.
 
Kwa kifupi unaweza sema Lulu amekuwa mtamu kama Mcharo!!

LULU APELEKEWA BARUA YA UCHUMBA

Stori: waandishi wetu
STAA ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amepelekewa barua ya uchumba kutoka kwa mfanyabiashara mmoja jijini Dar na kumfanya mama mzazi wa Lulu, Lucresia Karugila abaki ameshangaa.Tukio hilo lilitendeka Januari 8, mwaka huu, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam ambako ndiko yaliko makazi ya Lulu na mama yake huyo.
Mshenga anayefahamika kwa jina moja la Isaya akipeleka posa kwa akina Lulu Elizabeth Michael.
MSHENGA NI MPAMBE
Kwa mujibu wa watonyaji wetu ambao waliwataarifu mapaparazi wetu wa Kitengo cha Kufichua Maovu (OFM) kuhusu barua hiyo na kutia timu nyumbani hapo, mtu aliyepewa kuifikisha kwenye familia hiyo ni mpambe mkubwa wa mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Isaya, mkazi wa Kinondoni B, Dar es Salaam ambaye sasa amekuwa mshenga pia.
Staa ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
MSHENGA GETINI KWA AKINA LULU
Ilikuwa saa tano asubuhi, mshenga huyo akiwa ndani ya gari aina ya Toyota Corolla (namba hazikupatikana mara moja), alishuka nje ya geti kuu la nyumbani kwa akina Lulu ambapo anaishi na mama yake.
Mshenga huyo alibisha hodi kwa muda wa kama dakika tano ambapo mfanyakazi wa ndani (hausigeli) alifika getini na kufungua mlango.
Mshenga akigonga hodi getini kwa akina Lulu.
KILICHOZUNGUMZWA GETINI
Haikujulikana mara moja, wawili hao walikuwa wakizungumza nini getini lakini mapaparazi wetu waliweza kushuhudia mshenga huyo akinyoosha mkono na kumpa bahasha msichana huyo kisha geti likafungwa, mshenga huyo akasimama pembeni, huenda kusubiri majibu.
MSICHANA AREJEA
Baada ya dakika kama kumi, msichana huyo alirudi getini, akafungua nusu ya mlango kama awali na kuanza kuzungumza na mshenga huyo.
MSHENGA AONDOKA
Baada ya mshenga huyo kuondoka hatua kama ishirini mbele mapaparazi wetu walimwibukia na kumuuliza shida iliyompeleka kwenye nyumba ya akina Lulu.“Kwani vipi?” aliuliza mshenga huyo kabla ya kusema.
Mshenga akiondoka mara baada ya kumaliza majukumu mazito.
Risasi: “Sisi tulipata habari kwamba wewe umepeleka barua ya posa pale, ni kweli?”
“Kweli nimetoka nyumbani kwao na Lulu, nilipeleka barua ya uchumba ya bosi wangu.
“Nimefurahi nilipofika pale nikagonga geti, akatoka msichana mmoja, nilimuuliza kama mama Lulu yupo akasema yupo, nikampa barua akapeleka maana hakutaka mimi niingie,” alisema mshenga huyo.
MAJIBU YALIKUAJE?
“Baada ya muda yule msichana alirudi, akanipa barua akisema eti si ya Elizabeth wala Lulu. Sasa ni ya nani wakati jina la juu ya bahasha ni Elizabeth Michael.”“Naamini kabla mama Lulu hajaisoma aliangalia juu ya bahasha na kuliona jina la Elizabeth Michael ndiyo maana wakati ananirudisha tayari bahasha ilikuwa imefunguliwa.”
Barua ya uchumba iliyowasilishwa na mshenga kwa mama Lulu.
UTARATIBU ULIFUATWA?
Risasi lilimuuliza mshenga huyo kama bosi wake alifuata utaratibu wa barua za posa katika utamaduni wa Kitanzania ambapo ndani ya bahasha huwekwa pesa kidogo.“Tulifuata utaratibu wote, ndani ya bahasha tuliweka shilingi laki moja na zimerudi zote.”
MAMA LULU ANASEMAJE?
Baada ya kudokezwa ishu hiyo, Risasi lilimtafuta mama mzazi wa Lulu ili kumsikia anasemaje kuhusu madai ya mshenga huyo, kwamba alipeleka kweli barua ya posa kwa Lulu au alikwenda kwa shida nyingine.
“Mimi mwenyewe nawashangaa ninyi waandishi. Mambo ya kuolewa anayetakiwa kuulizwa ni Lulu mwenyewe. Kama mtu alileta barua au nini, Lulu ndiyo atajibu.
Staa ndani ya Tasnia ya Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Halafu naomba kuwaambia kwamba nilishasema siku nyingi mimi sitaki mambo ya magazeti, hata hao mabosi wenu niliwahi kuwaambia,” alisema mama Lulu na kukata simu.
LULU HAPOKEI SIMU
Baada ya kuzungumza na mama mtu, gazeti hili lilimsaka Lulu mwenyewe ili kumsikia anazungumziaje kuhusu barua hiyo lakini simu yake iliita kwa muda mrefu bila kupokelewa.

LULU AFUNGUKA KUWA HAPENDI KUWA KATIKA UHUSIANO WA MAPENZI

Stori: Imelda Mtema
Staa wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto wa kipekee, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefunguka kuwa kamwe hapendi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na masharobaro akidai kuwa siku zote ni pasua kichwa ila anazimikia watu wazima waliomzidi sana umri.
Staa wa filamu hapa Bongo mwenye mvuto wa kipekee, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi..
Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Lulu alisema akiwa na mwanaume anapenda ampite angalau miaka kumi na kuendelea kwa kuwa anakuwa ni mtu mzima na muelewa siyo masharobaro kila wakati wanafikiria jinsi gani wataonekana smati na si kufikiria maisha.
“Masharobaro hawana nafasi kwangu, kwa sababu hawafikirii maisha kabisa, hata mwanaume atakayenioa nafikiri atanipita zaidi ya miaka kumi, hapo ndiyo itakuwa sawa tofauti na hivyo sitaki masharobaro,” alisema Lulu.

LULU AHIFADHI NGUVU ZA KUJIFUNGUA

Stori: Hamida Hassan na Gabriel Ng’osha
MASTAA wana mambo! Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ametoa kali ya aina yake kwa kusema kamwe hatumii nguvu nyingi kwenye mapenzi kwa sababu yanapoteza muda bila sababu za msingi bora nguvu zake azitunze hadi pale atakapokuwa akijifungua.
Mtoto mzuri wa Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akipozi.
Akimwaga cheche mbele ya mwanahabari wetu, Lulu alisema siku hizi wanaume wengi wanawafanya wasichana watumie nguvu kutetea penzi kutokana na migogoro isiyokuwa na msingi.
“Bora nguvu zangu nizihifadhi za kuendea leba kuliko kuzipoteza katika mapenzi kwani hayo mambo yamepitwa na wakati kabisa,” alisema Lulu.

HATIMAYE: MSANII LULU AITAMBULISHA FILAMU YAKE MPYA INAYOITWA "MAPENZI YA MUNGU"




 Msanii wa Sanaa ya Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Alipokuwa akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU ambayo amewashirikisha Flora Mtegoha au Mama Kanumba na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Linah Sanga.

Msanii Wa Maigizo Nchini, Elizabeth Michael almaarufu kama Lulu akiitambulisha filamu yake Mpya iitwayo MAPENZI YA MUNGU leo mbele ya wanahabari (hawapo pichani).,Kulia ni Mmoja kati wa wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ajulikanae kama Flora Mtegoha almaarufu kama Mama Kanumba

Meneja Masoko wa Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Evance Stephen akiongea na wanahabari leo katika Ofisi za Proin Promotions Ltd zilizopo Mikocheni mtaa wa Ursino wakati wa Utambulisho wa Filamu mpya ya Lulu Iitwayo MAPENZI YA MUNGU.
Msanii Elizabeth Michael aka Lulu leo ametambulisha Filamu yake Mpya ambayo imeingia sokoni leo iitwayo MAPENZI YA MUNGU, huku akiwa amemshirikisha Msanii wa Bongo Fleva Linah Sanga na Mama Kanumba.
Wakati akiilezea filamu hiyo leo mbele ya wanahabari Lulu amesema Kuwa Ni Filamu inayofundisha na Kutoa somo kwa mtu yoyote yule ambae yupo hapa duniani kwa kuendelea kuonyesha kuwa MUNGU YUPO. Akiongezea kuwa..."Sisi kama binadamu tumekuwa tukifanya mambo mengi sana hapa Duniani na kupelekea kumsahau Mungu na pengine kuendelea kufikiria kuwa yote tuyafanyayo ni kwa uwezo wetu kumbe Sio uwezo wetu na Ni Mapenzi ya Mungu tu ndio yanayofanya sisi kufikia hapa tulipo leo"
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU imekuwa gumzo kabla ya kutoka kutokana na watanzania wengi kuwa na shauku ya Kutaka kumuona Lulu tena mara baada ya Kuonekana  katika Filamu Zake Mbili zilizotangulia za FOOLISH AGE na FAMILY CURSE. Sasa Lulu kuonekana tena katika kiwango cha Juu katika Filamu hii Mpya ambayo imeingia Sokoni Leo.
Filamu ya MAPENZI YA MUNGU ni filamu inayosambazwa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd.
   

LULU: BONGO MOVIES ISHABUMA

Stori: Imelda Mtema
STAA wa filamu mwenye makeke mengi, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema kwa mtazamo wake anaona Bongo Movies imebuma hivyo ameamua kukomaa na shule ili awe na kitu kingine tofauti na sanaa.
Staa wa filamu mwenye makeke mengi, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Lulu alisema kuwa kwa sasa yuko Chuo cha Uhazili Magogoni, Posta jijini Dar akichukua ‘course’ ya Utawala wa Umma (Public Administration) kwa ajili ya kupata ujuzi mwingine kichwani.
“Mwe-nzangu naona Bongo Movies kunaelekea kubaya, bora hata nikomae na shule angalau hata niwe na kitu kingine kichwani nipate mbadala wa sanaa,” alisema Lulu.

LULU AMLEGEZEA MKONGO

Na waandishi wetu
SiKU chache baada pedeshee Mkongo, Mwami Rajabu kutangaza kuwa anamtaka staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa gharama yoyote, mwigizaji huyo ametoa jibu linaloonesha dhahiri kwamba alikuwa radhi kumkubalia.
Staa wa sinema Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na waandishi wetu mara baada ya habari ya Mkongo huyo kuandikwa gazetini hivi karibuni, Lulu alisema kilichomshangaza kutoka kwa mwanaume huyo ni kwamba hakutakiwa kuanika hisia zake katika vyombo vya habari kama kweli ana nia ya dhati, angemtafuta mwenyewe au kwenda kujitambulisha nyumbani kwao.
“Namshangaa sana huyo Mkongo kwa kweli  kama angekuwa na mapenzi ya kweli asingeyaeleza kwenye magazeti, angenitafuta au angekuja nyumbani kwetu hapo ningemuona kweli ananipenda,” alisema Lulu.
Pedeshee Mkongo, Mwami Rajabu.
Staa huyo aliendea kumwaga chache kuwa, kama mwanamke, anahitaji kupewa heshima yake na kudai kuwa wanaume wengi wa sasa wamejisahau kupindisha mila za Kiafrika kufuata taratibu na badala yake wanatanguliza fedha mbele.
“Nadhani watu wamesahau mila za Kiafrika kabisa, huwezi kuwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke halafu utumie rafiki au vyombo vya habari umpate, hiyo inakuwa siyo heshima kabisa,” alisema Lulu.

LULU AFUNGUKA UKARIBU WAKE NA KADINDA

Stori: Mayasa Mariwata
MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amefafanua ukaribu wake na Martin Kadinda kwa kudai ni rafiki yake wa karibu na hakuna cha ziada.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiwa na Martin Kadinda.
Akipiga stori na paparazi wetu, Lulu alisema yeye na Kadinda ni marafiki wa kweli na amekuwa akiinjoi maisha yao kwa kushauriana masuala mbalimbali ya kimaisha tofauti na wengine wanavyojiongeza.
Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
“Kadinda ni mtu wangu wa nguvu hakuna kingine zaidi ya urafiki wa kawaida, manenomaneno ni kawaida kwa wanadamu,” alisema Lulu.

HUU NDIO UJUMBE WA LULU MICHAEL KWENDA KWA MAMA YAKE MZAZI, DAH UNAHUDHUNISHA SANA!! SOMA HAPA




STAA wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu' amemfagilia mama yake mzazi Lucresia Karugila kwa kupitia akaunti yake ya Instagram. 
Lulu akiwa katika pozi na mama yake.
Staa huyo ameachia picha yake wakati akiwa mdogo pamoja na mama yake kisha kuandika ujumbe wa kumfagilia mama huyo ambao ulisomeka hivi: 
Ni miaka 19 sasa tangu tulipoanza rasmi mahusiano haya, ni mahusiano ambayo yamekuwa na changamoto nyingi zaidi kwako kuliko kwangu.
Ni mahusiano yanayomiliki mapenzi ya kweli na mapenzi yasiyo na usaliti.
Haijalishi ni mara ngapi niliwahi kukukwaza na kukuumiza lakini hujawahi kuniacha katika hali yoyote na kusema utafute mwingine wa kuwa naye.
Haijalishi ni wangapi wazuri umewahi kuwaona duniani lakini siku zote mimi ni mzuri zaidi katika macho yako.
Haijalishi ni mabaya mangapi unayajua kuhusu mimi lakini unanitunzia siri zote zilizo mbaya na nzuri....wewe ni mtu pekee ninayeweza kusimama duniani na kujivunia kuwa ni wangu peke yangu, unayenipenda kiukweli, huwezi kunisaliti wala kumuona yeyote mwingine bora zaidi yangu hata kama ikiwa kweli..!
Nakuombea afya, furaha, nguvu na siku nyingi za kuishi duniani...! NAKUPENDA MAMA! 
Picha aliyoweka Lulu Instagram akiwa na mama yake enzi hizo.

LULU AMEMNASA MENEJA WA WEMA SEPETU, SASA MAPENZI MOTOMOTO!!


Taarifa ikufikie kwamba sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amemnasa aliyekuwa meneja wa Wema Isaac Sepetu, Martin Kadinda ambaye ndiye atakuwa meneja wake kwa sasa.
Sexy lady wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akizungumza na Amani kwenye Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro iliyopo Posta jijini Dar hivi karibuni waliponaswa wamegandana kama ruba, Kadinda alimuwahi mwanahabari wetu na kumsihi kuwa hawana uhusiano wa kimapenzi bali kuna habari mpya.
Kadinda ambaye hivi karibuni alimwaga kibarua kwa Wema, alisema kwamba aliongozana na Lulu hotelini hapo kwa kuwa kulikuwa na Fainali ya Shindano la Miss Ilala, Dar, wakiwa ni mtu na meneja wake kama alivyokuwa kipindi yuko na Wema.
Martin Kadinda.
“Kwa sasa ‘nammeneji’ Lulu. Naomba ieleweke hivyo ili baadaye watu wasiseme tunatoka kimapenzi kwa sababu nitakuwa naonekana naye kila mara na kwenye sehemu tofauti,” alisema Kadinda ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.
Kwa upande wa Lulu, alionekana kufurahia maneno hayo na kufanikiwa kumpata meneja huyo huku akiongezea kuwa amefarijika kuwa na meneja kama Kadinda.“Huyu ni meneja bora na siyo bora meneja kwa hiyo kama mtu anataka kufanya kazi na mimi, aanze kwa meneja wangu,” alisema Lulu.
Ukaribu wa Lulu na Kadinda ulianza kitambo hata kabla Kadinda hajafahamika kama ilivyo sasa.
  

Kisirani champonza LULU…Tajiri Wa Madini Ammwaga


Star wa filamu nchini aliyejaaliwa mvuto wa  kipekee, Lulu Elizabeth Michael anadaiwa  kutodumu na mwanaume sababu ya kuendekeza ubabe na kutaka kum-control mwanaume anayekuwa naye.
Inadaiwa Lulu hataki mchezo, mwanaume akishakuwa nae basi lazima ahakikishe hafurukuti. Taarifa  zinadai  kuwa miezi ya  hivi karibuni alikuwa na jamaa mmoja mdogo kimapenzi akammwaga na baada ya muda akawa anatoka na tajiri mmoja wa madin toka Arusha lakini tajiri huyo alinyoosha mikono juu baada ya Lulu kama kawaida kuruhusu majeshi yake yam-control jamaa huyo. 
Elizabeth Michael ‘Lulu’


Chanzo kimoja kikizungumza  kwa  sharti  la  kutotajwa  jina kimesema:
 
” Lulu ni mtu mwenye kisirani kwa wanaume, hadumu nao, wengie wanaokuwau nae ni wale wavumilivu sana. Nadhani ana matatizo ambayo yanahitaji mtaalam wa saikolijia ya mahusiano, akizinguliwa tu hachelewi kuvunja simu na kurejesha kila kitu alichokuwa amepewa”
  

JOTI, LULU BALAA


Stori: Waandishi wetu
Mastaa wawili Bongo waliokuwa watangazaji wa Shindano la Kuibua Vipaji vya Kuigiza, Tanzania Movie Talents (TMT), Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Lucas Mhuvile ‘Joti’ wamezua balaa na kuwaacha hoi mashabiki waliohudhuria fainali za shindano hilo kufuatia aina ya viwalo walivyokuwa wamepigilia.
Staa wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiingia ukumbini na kigauni kilichoacha sehemu kubwa ya kifua wazi.
Mpango mzima ulijiri kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, wikiendi iliyopita ambapo katika kuonesha ubunifu, mchekeshaji Joti, alitupia vazi la jinsi zote ambalo upande mmoja lilionekana ni sketi ya kike na mwingine suruali ya kiume.
Kama hiyo haitoshi, mwili wake aliugawa katika nafsi hizo mbili kwani licha ya sketi, pia mguu wake wa kushoto alivaa kiatu cha kike, kama ambavyo kichwani kwake, alisuka nywele upande mmoja kama mdada.Kitendo hicho kilionekana kama kuwapa bichwa wanaume wenye kufanya mapenzi ya jinsia moja, kwani waliona ni kitu cha kawaida kwa mwanaume kuvaa mavazi ya kike.
Staa wa vichekesho Bongo, Lucas Mhuvile ‘Joti’ akitumbuiza jukwaani ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
Kwa upande wake, Lulu alivaa kivazi kilichoonesha sehemu kubwa ya mwili wake, kikiwa kimeziba matiti kwa mbali na kusababisha wanaume wakware kutokwa na udenda.
Katika fainali hizo za kumsaka mwenye kipaji cha kuigiza ukumbini hapo, mshiriki kutoka kusini mkoani Lindi, Mwanaafa Libuyu ndiye aliyeibuka mshindi na kuondoka na cheki ya Sh. milioni 50.
LULU AINGIA UKUMBINI
Shushushu wetu alimshuhudia Lulu akizama ukumbini humo akiwa amevalia gauni hilo lililoacha wazi sehemu ya mwili wake hivyo kujichafua mbele ya mamia ya mashabiki waliohudhuria.
“Yaani Lulu huwa anaonekana kama hajali vile, hebu muone nguo aliyovaa, imemuacha wazi sana, karibu mwili mzima uko wazi na anatangaza kwa kujiamini mpaka dah! Ni balaa!” alisikika mmoja wa wahudhuriaji hao.
‘Joti’ akizidi kuwaonyesha vimbwanga vya 'kikomedi' watazamaji waliohudhuria fainali za TMT ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
Kwa upande wake, Lulu alionekana kujiamini kupita kiasi bila kujali macho ya watu kwani alifanya kazi yake vizuri na hakuwa na wasiwasi wowote kufuatia nguo aliyokuwa ameivaa mwanzo.
JOTI NAYE
Kufuatia kipaji alichonacho, Joti, kila mtu hakuamini pale alipopanda stejini kutumbuiza kwa staili ya aina yake kufuatia vazi lake alilokuwa amevalia yaani nusu mwanaume na kuwafanya watu washindwe kukaa na kuishia kuangalia shoo aliyokuwa akiitoa kwa mashabiki.
“Ama kweli watu wana vipaji vyao, yaani kwa wakati mmoja Joti ameweza kuigiza kama mwanamke na mwanaume. Ukiachana na hayo, hadi nguo nayo imeshonwa hivyo! Dah! Fundi alifanya kazi tena nampongeza sana Joti maana nilijua anakuja kuigiza,” alisikika mhudhuriaji mwingine.
Mshiriki wa TMT kutoka kusini mkoani Lindi, Mwanaafa Libuyu akishangilia ushindi alioupata.
Katika maelezo yake, Joti alisema sababu ya kufanya vile ni sapraizi tu kwa mashabiki wake kwani huenda walijua atakuja kama ambavyo huwa anafanya sehemu mbalimbali.
“Nimeamua kuja kivingine, hii staili ni ya kawaida tu, sema watu wameshangaa kuniona vile, ndiyo maana Lulu alisema ni sapraizi kwa mashabiki, ni kweli nimewafurahisha sana na huwa wanashindwa kunielewa kwa jinsi ninavyobadilikabadilika,” alisema Joti.
Mwanaafa Libuyu akikabidhiwa zawadi.
Joti hakuishia hapo kwani baada ya mshindi kutangazwa tu, alitoa shoo ya nguvu huku watu wakimzunguka na kumuimbia kwa kufurahishwa jinsi alivyokuwa akicheza.
Kabla ya shindano hilo, Lulu na Joti waliwahi kudaiwa wanatoka lakini kwa pamoja walikanusha vikali skendo hiyo na kuweka hadharani kuwa uhusiano wao ni wa kikazi tu.

Vazi la Lulu Michael Lawatesa Wanaume Wapenda Sketi



Vazi  alilokuwa  amevaa Lulu  Michael  katika  fainali  za  Shindano  la  TMT  lilizua  balaa  kubwa  kwa  wanaume  wapenda  sketi  baada  ya  vazi  hilo  kuanika  hadharani  maungo  nyeti  ya  msanii  huyo.

Katika  shindano  hilo, Binti  mdogo  toka  Mtwara, Mwanaafa Mwinzago, aliibuka  kidedea  na  kujinyakulia  milioni  50


GARI LA LULU LAIBUA MAZITO

Stori: Musa Mateja na Shakoor Jongo
MAKUBWA! Mambo yamekuwa mambo, kadi ya gari jipya la staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ imeibua mazito kufuatia Jeshi la Polisi Dar es Salaam kubaini kuwa namba ya Sanduku La Posta (SLP) iliyoandikwa kwenye kadi hiyo ni Wizara ya Mambo ya Ndani Tanzania.
Gari ya staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ‘Lulu’ aina ya Toyota Rav 4 New Model
IMEVUJAJE?!
Hilo lilibainika baada ya gazeti dada na hili, Ijumaa toleo la Ijumaa iliyopita kuandika habari yenye kichwa kisemacho; LULU AANDIKA HISTORIA.
Katika habari hiyo, Lulu alipewa shavu kwa vile alinunua gari aina ya Toyota Rav 4 New Model kwa pesa zake mwenyewe tofauti na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao huhongwa magari na wanaume.
SIMU YAPIGWA
Wakati gazeti hilo likiwa mitaani, mtu mmoja aliyedai kuwa ni afisa wa jeshi la polisi jijini Dar es Salaam alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global Publishers na kusema kuwa S.L.P ya 9140 iliyotumika kwenye kadi ya gari la Lulu ni ya jeshi hilo.
NI KOSA LA JINAI
Ofisa huyo aliliambia gazeti hili kuwa raia wa kawaida haruhusiwi kutumia sanduku la barua la jeshi kitu alichodai kinaonesha jinai ilifanyika wakati wa usajili ya gari hilo.
“Haiwezekani Lulu atumie Postal Office Box (P.O.Box au S.L.P) ya jeshi kwenye kadi ya gari lake ikizingatiwa kuwa yeye ni raia wa kawaida.
'Lulu’ akipozi.
“Ukiachana na hilo hata sisi maofisa wa jeshi la polisi hatuwezi kuitumia hiyo anuani kwa shughuli zetu binafsi labda kuwe na kibali maalum,” alisema afisa huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa vile yeye si msemaji wa jeshi hilo.
LULU ANASEMAJE?
Baada ya kupata maelezo hayo, gazeti hili lilimtafuta Lulu ili kujibu madai hayo yenye utata ambapo alisema kuna mtu alimtengenezea namba yake ya TIN (Taxpayer Identification Number) ndiye aliyemwekea anuani hiyo bila yeye kujua.
Huku akisita kumtaja kwa jina mtu huyo lakini akimtaja kwa cheo ambacho kiko wazi na mapaparazi wetu wakamjua, Lulu alifunguka hivi:
“Namiliki gari langu kihalali kabisa na nina kila kitu, niko tayari kwenda kokote kuonesha uhalali wa umiliki wangu. Kuhusu hiyo anuani, mtu aliyenitengenezea TIN Number ili nipate leseni ya udereva ndiye aliyetumia hiyo anuani, mimi sijui chochote jamani.”
AOMBA AHIFADHIWE SIRI
Katika hali ya kushangaza, Lulu aliwaambia mapaparazi wetu wasimtaje jina gazetini mtu huyo aliyemsajilia TIN akisema asitiriwe siri yake.
Kadi ya gari la ‘Lulu’ yenye anuani za jeshi la Polisi (S.L.P ya 9140).
POLISI NAO WANENA
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, ambako ndiko usajili wa gari hili ulifanyika katika ofisi za TRA, Zakaria Sebastian, alisema jeshi lake halina taarifa za kuwepo kwa jambo hilo lakini watalifuatilia kwa karibu.
“Huenda ni mke wa askari au mwanafamilia. Unajua kuna baadhi ya maofisa wana msamaha, huenda alitumia hivyo, lakini tutafuatilia,” alisema kamanda huyo ambaye alielezwa kuwa, Lulu hajawahi kuwa mke wala mwanafamilia ya mwajiriwa wa jeshi la polisi.
“Kama hajawahi kuwa mwenye kustahili kutumia anuani hii, basi tutafuatilia ili kujua wakati akiitumia, je alikuwa anakusudia kufanya jinai? Tukijiridhisha hivyo bila shaka sheria itafuata mkondo wake.”
UCHUNGUZI WA RISASI MCHANGANYIKO
Katika uchunguzi wa gazeti hili, anuani hiyo imeshatumika na Jeshi la Polisi Magomeni na Mkoa wa Polisi wa Ilala jijini Dar. Namba hiyo inatofautiana tarakimu moja na ya Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

BAADA YA UVUMI KUWA LULU AMEMWAGWA NA BEDEJEE WAKE KWAKOSA LA KUCHEPUKA …..NA HIVYO KUNYANNG’ANYWA GARI…..LULU AIBUKA NA KADI ORIGINO YA GARI HILO..SOMA MKASA MZIMA…

Picha Lilianza Hivi Huko Instagram:

Baada ya siku za hivi karibuni Lulu Kuposti picha akiwa najamaa ambaye kajifunika kofia ambaye ilisemekana kuwa ndio jamaa anaekula MUZIGO…

Chokochoko Leo hiii Toto La Kimanga aliibuka nahii huko instagram;




"BbuahahahAaaaa hizi picha zasababisha mdogo wetu kupigwa chin....... Kaa namie nikupe umbeaaa...... Bishost unanijua una kibopa kinachokuweka mujin bila aibu unapost picha na kiserenget bwoy chako unategemea nn??? sasa tutakimbizana na bajaji wallah nahayo ndo madhara yakupewa mkoko without kadi uwiiiiiiiii ukiachwa unanyanganywa kila kitu... haya mereran chali... tmt naye kakupa kibuti poule my toto jamwaaaniii Naskia mshikaji kasharudiana na husna wakesasa sura yako unaiweka wapi mama Wallah sikuile ningekuwa na ndoo ningejaza machoz yako pale kibo complex usikate tamaa kila jambo linasababu yake lol Ulisema tupande milimao eeeh mie yangu na matunda yashaazaa kabisa mixture kutengeneza juise ya limaooooo .......baadae wapendwa"


Lulu akajibu..... Akatupia picha ya Kadi ya gari na kuandika;



"Sema nn...Leo imebidi tu niwe mswahili...akha...Alafu Wangu...we ndo nilikuwa nakuaminia kwa habari za uhakika sema Leo umeniangusha...!������My followers nisameheni bure....ntafuta baada ya muda kdo..! #OwnerDetails Hv Kwani google haisaidiagi kujua mambo madogo madogo Kama haya!??? Jina la kwenye cheti cha kuzaliwa hiloooo...�� Tuendelee kumwagia milimao,mimbilimbi alafu tupande na ukwaju kbsaaa...! ����mpk najishtukia cjawahi kufanya hz mambo...sema Leo ndo mwanzo na mwisho....Wallah tena.
Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top