Habari Kali
Loading...

VIJANA WAWILI WAUAWA NA WANANCHI WENYE HASIRA KALI BAADA YA KUMUUA MAMA YAO WA KAMBO KWA KUMCHARANGA MAPANGA

Vijana wawili wameuawa kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira mkoani Geita kwa kile kilichotajwa kuwa vijana hao walimuua mama yao wa kambo kwa kumcharanga mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Akizungumzia tukio hilo kaimu Afisa mtendaji wa kata ya Busanda alisema tukio hilo lilitokea juzi katika kijiji cha Nyamtundu majira ya saa tatu usiku ambapo Mama moja aliyejulikana kwa jina la Mwanamaila Mwanatenga (50) aliuawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana wakati akitoka chooni kujisaidia mara baada ya kumaliza kula.

Alisema mara baada ya kufanya mauaji hayo walitokomea kusikojulikana na wananchi kwa kushirikiana na jeshi la Sungusungu walianza msako wa kuwatafuta na hatimaye waliwakamata wakijaribu kutoroka.

Watuhumiwa hao walikamatwa katika kijiji jirani cha Msasa wakiwa na damu kwenye makoti waliyokuwa wamevaa ndipo wananchi hao wakiwa na jeshi la sungusungu waliwauliza kuwa wanatoka wapi.

Watuhumiwa hao  walijibu kuwa wanatoka kwenye sherehe ya harusi kwao na baada ya  wanafamilia kubaini kuwa mama yao wa kambo ameuawa walianza kuwapiga hadi kuwaua na kisha wakawababua kwa moto.

Afisa huyo aliwataja waliokufa kuwa ni Makoye Nzari(25) na Masumbuko Nzari(36) wote wakiwa ni watoto wa kambo wa mama huyo.

Diwani wa kata hiyo Aliphonce Matonange amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda wa jeshi la polis mkoani Geita Joseph Konyo alisema hakuna aliyekamatwa juu ya tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea wa kuwabaini waliofanya tukio hilo na  huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.

MUME AMPIGA NYUNDO NA KUMKATA MAPANGA MKEWE,KISA KUKATAA UKE WENZA

DAH! Inasikitisha sana jamani. Faustina Selali, 38, mkazi wa Mgeta, Mvomero mkoani hapa, yupo kwenye mateso makali akijiuguza kutokana na kipigo  
alichopata kutoka kwa mumewe wa ndoa aliyemtaja kwa jina la Lugasiani John Miasiku, kisa kikiwa ni mumewe huyo kutaka kuoa mke wa pili.
Faustina Selali, akiwa katika maumivu makali baada ya kushambuliwa na mumewe.
Mwanamke huyo amelazwa katika wodi nambi 3 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, ambapo amesimulia kisa chote mbele ya kamera ya Uwazi.
KISA CHENYEWE
Akizungumza kwa tabu, Faustina alisema tukio hilo lililobadilisha historia ya maisha yake na kumwachia machungu moyoni mwake, lilitokea Juni 25, mwaka huu majira ya saa nne usiku ndani ya nyumba yao.

“Mimi na mume wangu tumeishi kwenye ndoa kwa muda wa miaka 20 na kufanikiwa kupata watoto watano. Kwa kipindi kirefu nilihisi ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwingine, wakati naendelea kumchunguza, mume wangu akaniambia anataka kuoa mke wa pili,” alisema Faustina kwa uchungu na kuongeza:
“Nikamhoji mume wangu, dini yetu hairuhusu jambo hilo na zaidi ya yote anachotafuta kwa huyo mke wa pili ni kitu gani wakati tayari mimi nimeshamzalia watoto watano na bado naendelea kuzaa?
“Hakuwa na jibu la maana, akaendelea kushikilia msimamo wake. Mwisho nikaona nisimlazimishe sana, nikamwambia kama hivyo ndivyo basi tugawane mali ili mimi niondoke aje huyo mwenzangu kwani sitakuwa tayari kuishi maisha ya uke wenza. Kwa kweli hakuwa na jibu la maana.”
Akionyesha sehemu ya jeraha.
HARUFU YA KIFO
“Ugomvi huo ulitokea Jumanne, kesho yake yaani Jumatano (siku ya tukio) mume wangu alivyorudi shamba nilimtengea ugali kama kawaida. Alikula vizuri tu... tukapanda kitandani kulala, kama unavyojua tena wanandoa muda wao wa kuzungumza kwa utulivu ni usiku, nikaamua kuutumia muda huo kumwuliza mwenzangu.
“Nikamwambia kama bado ana msimamo wake uleule, anipe sehemu yangu niondoke zangu. Hapo nikawa nimechokoza moto. Ilikuwa ghafla tu, aliamka kitandani na kuchukua nyundo kisha akaileta kichwani na kunipiga nayo, baadaye akanipiga mdomoni na kuning’oa meno mawili ya mbele kwa kutumia ile nyundo.
“Hakuishia hapo, akanitoa panga kisha akanicharanga mikono yote, palepale damu zikaruka kama kachinja ng’ombe. Nilihisi maumivu makali sana, sikuwahi kupata maumivu makali kama yale. Kusema ukweli nilichanganyikiwa kabisa na kile kipigo.”
ATUMIA UJANJA KUJIOKOA
“Wakati akiendelea kunipiga bila huruma, alikuwa akisema dawa yangu mimi ni kufa ili aweze kumchukua huyo mwanamke wake bila usumbufu. Nilivyosikia hivyo ikabidi nitumie akili; nikajiangusha chini na kujifanya nimekata kauli ili nisiendelee kuumia.
“Alipoona hivyo kweli akaniacha. Akavaa nguo zake na kukimbia. Mwanangu mdogo Nesto akanisaidia kunikongoja hadi kwa jirani yetu Mzee Chota ambaye naye aliita majirani haraka, ilikuwa ni saa sita usiku, wakanikimbiza hadi Zahanati ya Mlali lakini nikapewa rufaa ya kuletwa hapa kutokana na hali yangu kuwa mbaya.”
Kwa mujibu wa Bi. Faustina, licha ya mume wake kumfanyia ukatili huo, ndugu wanaofika hospitalini hapo kumjulia hali, wanasema mumewe bado hajakamatwa na amekuwa akiendelea kutoa vitisho dhidi yake.
Uwazi lilifunga safari hadi kijijini Mgeta kwa lengo la kuhojiana na mtuhumiwa huyo na kufanikiwa kumkuta lakini alipomuona mwandishi wetu, Miasiku alitimua mbio akidhani alifuatwa na askari.

WANANCHI WAWAUA WABAKAJI KWA KUWACHOMA MOTO

UNYAMA...!! MTANZANIA ACHINJWA NCHINI KENYA KUZIKWA KESHO ARUSHA

Mkazi wa Mtaa wa Engurumaus kata ya Moshono jijini Arusha Siryakwi Maleko 78 amechinjwa huko Mombasa nchini Kenya katika tukio lililowahusisha watu wengine 4. 
Mtanzania huyo atakayezikwa jumatatu katika kata ya Moshono alikwenda Mombasa kumsabahi binti yake ambapo katika tukio hilo Al Shabab pia wamemchinja mkwe wake walipokuwa wote shambani wakilinda wanyama waharibifu.


UKATILI:Bosi adaiwa kumbaka house girl wake mwenye umri wa miaka 14 siku 4 baada ya kuanza kazi

Mfanyakazi wa ndani, miaka 14 mkazi wa kijiji  cha Mdenge, Kata ya Likombe katika Wilaya ya Mtwara, amebakwa na mwajiri wake usiku wa kuamkia jana na kumsababishia maumivu makali na kisha kutokomea kusikojulikana.
Akiongea na FikraPevu jana Jumatatu Juni 16, 2014, Mama mzazi wa mtoto huyo, mwenye umri wa miaka 36, amesema mtoto wake amekumbana na masahibu hayo siku nne tangu aanze kufanya kazi kwa mwajiri wake aliyemtaja kwa jina moja la, Sharifu (42), mfanyakazi katika kiwanda cha kuzalisha saruji cha Alosko mkoani humo.
Amebainisha kuwa, mtoto wake alipata kazi ya kufanya kazi za ndani kwa mwajiri huyo Juni 12, 2014 ambapo ilipofikia usiku wa kuamkia leo mtoto huyo aliamua kutoroka nyumbani kwa mwajiri wake anayeishi na mke wake bila kuaga kutokana na hofu ya kuzuiwa kwenda kwao au kufanyiwa unyama zaidi na kukimbilia nyumbani kwao.
“Alivyopata kazi anasema hii sio mara ya kwanza kufanyiwa hivyo hii ni mara ya pili, usiku wa kuamkia Jumamosi ya Juni 14, 2014 alimuingilia mtoto wangu na alipomwambia atatoa taarifa akamwambia asiseme kwa mtu yeyote kwani atamfanya kama mtoto wake, sasa leo tena amemuingilia.
“Nimemkuta yule mama aliyekuwa anafanya kazi kwake amesema alihisi kuwa kuna huo mchezo lakini aliogopa kuniambia tangu Jumamosi” alisema  mama  wa  mtoto.
Kwa upande wa mtoto huyo, amesema ,“Nilikuwa nimelala usiku wa manane ndipo niliposhtuka, nilipotaka kupiga kelele alinikataza kuwa nisiseme kwa mtu kwani atanifanya kama mtoto wake, na usiku wa kuamkia leo alikuwa ameenda kuangalia mpira nilivyoshtuka alikuwa ameniingilia kimwili ndio nikaondoka asubuhi kwenda kwetu kwa maana alisema nisipige kelele”
Taarifa yatolewa Polisi
Mama mzazi wa mtoto huyo amesema wameripoti tukio hilo katika Kituo cha Polisi Mtwara, kwa tuhuma hizo na amefunguliwa jalada namba Mt/RB/2198/2014 ambapo mtoto huyo amefanyiwa vipimo katika kituo cha Polisi kilichopo wilayani humo na kugundulika kuwa alibakwa na kupata majeraha makubwa.
binti
FikraPevu ilimtafuta Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Zelothe Stephen, ambaye hakupatikana kupitia simu yake ya mkoni baada ya kuita bila kupokelewa, huku upande wa ndugu wa mtuhumiwa wakigoma kuongelea suala hilo wakidai hawajui alipo ndugu yao licha ya kushangazwa na tukio hilo

UNYAMA...!! Watoto Njiti Mapacha Watelekezwa na Baba Yao

DADA mmoja Fatuma Hussein (30), anaomba msaada kwa Watanzania baada ya kutelekezwa na mzazi mwenzake.Akizungumza na mwandishi wetu maeneo ya Magomeni Makanya,
Dar dada huyo anadai kuwa aliishi na mzazi mwenzie kwa miezi miwili kama mke na mume na ndipo akapata ujauzito,wakati huo alishajitambulisha nyumbani kwao na kutoa posa baada ya kujifungua watoto  njiti mapacha wakiwa na miezi saba.
Fatuma Hussein akiwa na watoto wake mapacha.
Fatuma Hussein akiwa na watoto wake mapacha.
Watoto mapacha wakiwa wamelala.
Watoto mapacha wakiwa wamelala.
Rahma akiwa kalala
Rahma akiwa kalala
Rahmu akiwa kwenye pozi.
Rahmu akiwa kwenye pozi.
Anadai mzazi mwenzake aitwaye Mussa Unguja kamtelekaza, akaongeza kuwa huwa haji kuwaona watoto. “Nikimpigia simu hapokei lakini siku moja aliipokea na akasema hana shida na watoto wangu,  toka siku hiyo sijazungumza naye.
‘’Watanzania naomba msaada wa hali na mali, watoto wangu na wapenda na kwa sasa sina kazi, naishi kwa kubangaiza chumba chenyewe nimepanga,’’alisema Fatuma.

Watuhumiwa wa Kesi ya Mtoto wa Boksi kusomewa Mashitaka Upya…!!

1
Difenda iliyobeba watuhumiwa wa kesi ya mtoto wa boksi, Nasra Rashid ikiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro.
 2
Baba mlezi wa mtoto Nasra, Mtonga Omari akishuka kwenye gari la polisi kwa staili ya kuruka.
3
Bi. Mariam Said ambaye ni mama mkubwa wa Nasra, akishuka kwenye gari hilo.
4
Baadhi ya wananachi wakiwazomea watuhumiwa waliokuwa kwenye gari hilo baada ya kesi yao kuhairishwa hadi Juni 12 mwaka huu.
5
Wananachi hao wakilifukuza gari lililobeba watuhumiwa waliorejeswa polisi kwa mahojiano mapya baada ya mtoto Nasra kufariki dunia

Laana! Mzungu matatani kwa kumlazimisha hausigeli wake kula URODA na mbwa wake huko Tabata..!!

KHAA! Katika hali ya kushangaza, dada wa kazi za nyumbani (hausigeli) mkazi wa Tabata  jijini Dar aliyetambulika kwa jina moja la Aneth, amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kudai kuwa bosi wake ambaye ni Mzungu amemlazimisha kufanya mapenzi na mbwa wake.
Mzungu huyo ambaye jina tunalihifadhi, alidaiwa kufanya tukio hilo la kinyama Mei 26, mwaka huu na inadaiwa Aneth alipomkatalia, alimtimua nyumbani hapo kwa kumtupia virago.
Chanzo makini kilidai kuwa, baada ya kutupiwa virago bila kupewa mshahara wake sambamba na kipigo, Aneth aliripoti tukio hilo katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Tabata, Dar na muda mfupi polisi walifika nyumbani hapo lakini Mzungu huyo hakutoka ndani, akakataa kuzungumza chochote.
Mapolisi wakiwa wametinga nyumbani kwa mzungu na silaha. Kushoto ni hausigeli.
Mapolisi wakiwa wametinga nyumbani kwa mzungu na silaha. Kushoto ni hausigeli.

Taarifa zilidai kuwa, baada ya polisi kukutana na kizingiti hicho, walimpigia simu kiongozi wao ambaye aliwaamuru warudi kituoni wajipange upya.

Wananchi wakiwa wamezingira nyumbani kwa mzungu.
Wananchi wakiwa wamezingira nyumbani kwa mzungu.

Akisimulia zaidi ishu hiyo, Aneth alisema polisi walipoondoka eneo hilo, umati uliochukizwa na kitendo hicho ulikusanyika nje ya nyumba ili kumdhibiti ‘mtasha’ huyo kwa lolote.

“Kuna jirani mmoja alipiga simu tena kituo cha polisi alipoona hali ya hewa imechafuka ndipo polisi wakafika kwa mara nyingine na difenda na kufanikiwa kuingia ndani kwa kutumia geti kubwa, walipofika walikuta milango imefungwa lakini ilisemekana aliruka ukuta na kutimkia kusikojulikana.

“Polisi waliniambia nimpigie simu ajisalimishe lakini nilipompigia alisema hayupo na kama tunamhitaji tukutane sehemu huku na yeye akiwa na polisi wake,” kilisema chanzo.

Mbwa wa mzungu waliotakiwa kufanya mapenzi na hausigeli.
Mbwa wa mzungu waliotakiwa kufanya mapenzi na hausigeli.

Mmiliki wa nyumba hiyo anayeishi Kigamboni, Mr. Cris alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kupokea malalamiko na manyanyaso kutoka kwa Aneth.
Akisimulia zaidi maisha anayoishi na Mzungu huyo, Aneth alisema: “Alikuwa akinitafutia sababu za kunitimua kwani hivi karibuni kwa bahati mbaya nilipoteza ufunguo wa ndani, akanipiga mateke na kunisababishia maumivu makali mwilini kiasi cha kushindwa kutembea.

“Lakini lililoniuma zaidi ni hili la kunilazimisha eti nifanye mapenzi na mbwa wake, amekuwa akifanya hivyo mara kwa mara mimi nikaona siyo sawa na nilipokataa ndipo yakanikuta hayo.”
Aneth aliripoti matukio hayo katika Kituo Kidogo cha Polisi Tabata na kupewa fomu ya matibabu (PF-3) sambamba na kufunguliwa jalada la kesi namba TBT/RB/3132/2014/ SHAMBULIO na jalada la uchunguzi lenye nambaTBT/IR/1829/2014/UCHUNGUZI.

VIDEO HAPO CHINI

Picha za wazazi wa mtoto aliyefungiwa ndani ya Box kwa miaka 4 wakipelekwa Rumande

1
Washitakiwa hao watatu waliofikishwa katika mahakamani   ni baba mzazi wa mtoto huyo Bw Rashid Mvungi,mama mkubwa wa mtoto huyo Mariam Said na baba baba mlezi wa mtoto huyo ambaye ni mume wa Mariam, Bw Mtonga Omari
2
Pichani ni  baba mlezi wa mtoto huyo Bw Mtonga akitoka mahamakani na kuingizwa mahabusu ya mahakama hiyo kusuburi gari la kumpeleka gerezani akijutia tendo hilo kwa kushika kichwa.
3
 Mwenye shati la Katori ni baba mzazi wa mtoto huyo Bw Mvungi akiingia kwenye chumba hicho cha na mwenye mtandio ni mama mkubwa wa mtoto huyo Bi Mariam
Wazazi na walezi wa mtoto Nasra Mvungi  aliyefungiwa  ndani  ya  boksi  kwa  miaka  minne  juzi walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro na kusomewa mashtaka yanayo wakabilia ambapo kesi hiyo iliahilishwa hadi Juni 9 mwaka huu ambapo washitakiwa wote walirudishwa lumande  kwa  kuwa  hawakutimiza  masharti  ya  dhamana.

Wazazi wa yule mtoto aliyefungiwa ndani ya Box wasota rumande

BABA mzazi pamoja na walezi wa mtoto anayedaiwa kufichwa kwenye boksi kwa takribani miaka mitatu, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Morogoro na kusomewa mashitaka ya kula njama na kufanya ukatili dhidi ya mtoto huyo.
Rashid Mvungi (47), mkazi wa Lukobe na mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, ambaye ni baba wa mtoto huyo pamoja na wanandoa Mariamu Said (38) na mumewe, Mtonga Omar (30) walifikishwa mahakamani jana.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mary Moyo, Wakili wa Serikali, Sunday Hyera kwa kushirikiana na Mwendesha Mashitaka wa polisi, Anganile Msiani walidai washitakiwa walitenda makosa hayo kati ya Desemba mwaka 2010 na Mei mwaka huu katika eneo la Kiwanja cha Ndege, mjini Morogoro.
Walidai katika kipindi hicho, washitakiwa wakiwa walezi wa mtoto huyo, walimfanyia ukatili wa kumtelekeza na kumpa malezi akiwa ndani ya boksi na hivyo kumsababishia magonjwa. Walitaja maradhi yaliyomkumba mtoto huyo akiwa ndani ya boksi pamoja na utapiamlo, maumivu ya kifua na mvunjiko wa mifupa katika maeneo ya mikono na miguu.
Mawakili hao walidai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kuiomba mahakama kutaja tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Wakili wa Serikali, Hyera alidai mahakamani kwamba upande wa Jamhuri hauna kipingamizi kuhusu dhamana kwa washtakiwa.
Hakimu Moyo alisema dhamana kwa washitakiwa iko wazi ,lakini kwa masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni tano kila mmoja.
mtoto aliyefungiwa
Alisema sharti lingine ni kwa wadhamini kuwa na barua kutoka kwa waajiri wa kuaminika au serikali za mitaa.
Washtakiwa walishindwa kutimiza masharti hayo, hatua iliyowafanya warejeshwe rumande. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 9 mwaka huu kwa ajili ya usikilizaji wa awali.

TAZAMA JINSI MTUHUMIWA HUYU WA WIZI AKISHUSHIWA KIPIGO KIKALI NA WANANCHI

Jamaa wawili wanaotuhumiwa kuwa wezi, nusura wauawe kwa kuchomwa moto na raia waliamua kuchukua sheria mkononi baada ya kula kichapo ‘hevi’ kwa msala wa kukwapua mkoba wa mrembo aliyekuwa ndani ya Bajaj.

Kijana ambaye hakufahamika jina lake mapema amejikuta kwenye mikono ya wananchi wenye hasira kali baada ya kukwapua mkoba kwenye bajaji

Katika tukio hilo lililojiri maeneo ya Kijitonyama, Dar, mwanzoni mwa wiki hii, shuhuda aliyeona alisema aliwaona vijana hao wakiwa wamepanda pikipiki wakipora mkoba wa mrembi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Magdalena John (21).

Alisema baada ya kupora mkoba huo walianza kutoka nduki lakini kabla hawajafika mbali, mtu mmoja aliyekuwa na gari, ambaye pia aliona tukio hilo, aliziba njia na kuwafanya vijana hao kutumbukia mtaroni.

msichana huyo alishuka ndani ya Bajaj na kuanza kuwapigia kelele za wizi hivyo kuwafanya wapita njia kuanza kuwapiga kwa kutumia silaha mbalimbali zikiwemo mawe, fimbo na matofali.

Waandishi wa habari hii waliowahi kufika eneo la tukio, waliwashuhudia watu hao wakipokea kipigo kikali kilichowafanya wawe hoi.
Mtuhumiwa mwingine akihojiwa baada ya kupata kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali.

Akizungumzia mazingira ya tukio hilo, Magdalena alisema ana hofu kuwa waliompora, walianza kufuatilia nyendo zake tangu alikotoka nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala, Dar.

“Mimi naweza kusema huu ni mchezo ambao umepangwa tangu naanza safari,  kwani wangejuaje kama nimeshikilia mkoba wakati nilikuwa ndani ya Bajaj?” Alihoji msichana huyo ambaye aliomba vijana hao wauawe.

Hata hivyo, wakati jamaa hao wakipokea kipigo kutoka kwa wananchi, baadhi ya watu walipiga simu Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao baada ya muda mfupi waliwasili wakiwa tayari kwa lolote.

 Baada ya kufika eneo la tukio na kuona namna vijana hao walivyokuwa wamechakazwa, waliwachukua vijana hao na binti aliyeporwa kisha kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi.

Lakini katika hali ya kusikitisha zaidi, baada ya vijana hao kupora mkoba huo na kutumbukia mtaroni, baadhi ya watu waliokuwa wakiwapiga, nao waliuchukua mkoba huo na kutoweka nao kusikojulikana.

Mwalimu Aua Denti kikatili huko KAHAMA..!!

MWANAFUNZI  mmoja mkazi  wa Jijini Mwanza Clinton Majembe ameuwawa kwa kupigwa na mama yake wa kambo Lupinda Kauli Mwalimu wa Shule ya Msingi Malunga mjini Kahama kwa kinachodaiwa kuwa kuwa mtoto huyo aliacha jiko jiko la gesi likiwa linawaka ndani.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Noel Mseven ambapo tukio hilo lilitokea usiku wa kuakia Ijumaa kuu alisema kuwa Marehemu alikuwa ni Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule moja mjini Bukoba.
Mseveni alisema kuwa Marehemu Clinton alikuja kumsalimia mama yake wakati wa likizo ndogo ya pasaka na hivyo kumkosa hali ambayo ilisababisha mama yake huyo wa kambo aliyekuwepo katika nyumba hiyo kupiga kutokana na kudai kuwa alikuwa amewasha jiko la gesi bila ya idhini yake.
mwalimu
Alisema kuwa Mama huyoa ambaye ni mtu wa matukio katika mtaa huo pia inasadikiwa pia aliwahi kmtishia mume wake kumuua na hivyo kusababisha kuukimbia mji wake mpaka kufikia hivi sasa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Ernest Mangala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kwa sasa hayupo ofisi yupo nje kikazi na kuhaidi kulizunguzia tukio hilo pindi atakaporejea kazini hivi karibuni
Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top