Habari Kali
Loading...

H MAMA AZINDUA KWA MBWEMBWE WIMBO WA ‘KIDOGO’ MAISHA CLUB DAR

H Mama akiimba kwa hisia wakati wa uzinduzi wa wimbo wake wa ‘Kidogo’ katika ukumbi wa Maisha Club jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.  H Mama ambaye jina lake halisi ni Flora Mvungi, ni mke wa mwanamuziki H Baba.H Mama akifanya yake na kipenziye H Baba.H Baba akianza ‘machejo’ kwa mbwembwe.
Prince Dully Sykes akikamua na Rashida Wanjara.
Mwanamuziki Pasha akiimba na kucheza sambamba na shabiki aliyeshindwa kuzuia mzuka wake.
Msanii wa Scorpion Girls, Isabella Mpanda, akiwakilisha jukwaani katika kusindikiza uzinduzi huo.
Umati wa mashabiki uliojaa kushuhudia shoo hiyo.   Madansa wakicheza kwa manjonjo.
Dogo Poteza akitoa burudani na mshirika wake.

HUSSEIN MACHOZI NAE KAACHIA WIMBO UNAITWA "MDOGO MDOGO"...KUSHINDANANISHA NA WA DIAMOND



Mtandao wa GHAFLA wa Kenya umewaweka ulingoni nyota wa Tanzania Diamond Platnumz na Hussein Machozi kwa kupambanisha wimbo wa ‘Mdogo Mdogo’ wa Platnumz, na wimbo ‘mpya’ wa Machozi ambao bado haujatoka wenye jina hilo hilo ‘Mdogo Mdogo’. 



“Is This Beef in the Making??” Ndivyo umeuliza mtandao huo kwenye kichwa cha habari hiyo.


“Hussein Machozi has chucked another tune dubbed Mdogo mdogo which surprisingly shares the same name with Diamond’s Mdogo mdogo barely 3 months after the latter dropped his. The BIG QUESTION could this be a drive to prove Diamond wrong? If you listen to this tune by Hussein Machozi its crystal clear that it is a big tune but do i say? “ Hivi ndivyo ilivyoandikwa na mtandao huo. 

GHAFLA wameongeza kuwa kuna tetesi kuwa Hussein Machozi na Diamond hawapikiki chungu kimoja. 

Iskilize ‘Mdogo Mdogo’ ya Hussein Machozi
   

TAZAMA KIPANDE CHA VIDEO MPYA YA SHILOLE "NAMCHUKA" ITAKAYOTOKA HIVI KARIBUNI


Mwezi uliopita Shilole alienda Nairobi, Kenya kushoot video ya single yake mpya ‘Namchukua’, video ambayo imeongozwa na director Kevin Bosco Jnr. Shilole amesema video hii imemgharimu si chini ya shilingi milioni 10. Hii ni teaser ya video hiyo inayotarajiwa kutoka ‘soon’.




VIDEO YA NEY WA MITEGO "MR. NAY" YAZUA GUMZO, MAMA YAKE MZAZI AMUITA AMUELEZEE VIZURI INA MAANA GANI..NI FREEMASON AU??

Nay wa Mitego msanii wa bongofleva ambae yupo kwenye list ya watakaotumbuiza katika stage ya Serengeti Fiesta 2014 Ijumaa hii hapa 98.6 Musoma na Jumapili 87.5 Shinyanga, amethibitisha kwamba Mama yake mzazi amemuita na kutaka kujua kilichoonekana kwenye video yake mpya ya‘Mr. Nay’ aliyoifanya Kenya kinamaanisha nini.
Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.10 AM
Nay ambae kabla ya kufanikiwa kimuziki aliwahi kuwa kinyozi wakati bado akisoma sekondari, ameongea na millardayo.com na kusema mama yake mzazi amemuita nyumbani September 2 2014 kutaka kujua kinachoendelea sababu alichoona na anachoambiwa na watu kimemfanya apate wasiwasi mkubwa.
Nay anasema ‘mimi nafanya kitu kutokana na idea ambazo huwa zinatoka kichwani mwangu, nafikiri watu wameona ni video kubwa nzuri na kali…. sijawahi kufanya video kali kama hii ambayo kidogo inataka kuniletea shida ila sio kitu kibaya kwangu’
Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.24 AM‘Zile damu, na vitu vingine kama vya kishetani pamoja na namba ninayopenda kuitumia ya #966 ni vitu vinavyofanya nipate sana msg na kuulizwa maswali, na ndivyo vitu vimemshtua mama mpaka akaniita, watu wengine wanadhani mimi ni mwabudu shetani ila nataka watu watambue kwamba hakuna kitu kama hicho, ni ubunifu tu… na hii namba kuna siku nitakuja kuielezea maana yake hapahapa kwa millardayo
Screen Shot 2014-09-03 at 3.30.32 AMNay amesema ataweka wazi kila kitu alichoambiwa na mama yake baada ya kukutana nae kuzungumza kuhusu hii video ambayo imemuhuzunisha kama mzazi ikiwa ni video ya kwanza kumfanya amuite na kuhoji.

Cheki video ya Nay wa mitego ya Mr Nay ilivyokua ikitengenezwa.


mrniceHii itakua video ya pili kutoka kwa Nay wa Mitego kufanya video nje ya ardhi ya 255 baada ya ile ya Nakula Ujana kufanya vizuri,siku chache zilizopita ameanza kutoa kipande kidogo cha video hiyo.
Millardayo.com imepata nafasi ya kuona video hiyo wakati ikitengenezwa na hiki ni kipande cha wakati wa utengenezwaji wa video hii ambayo kwa asilimia kubwa imefanywa Kenya.

DAAH KWELI MAPENZI NOMA...!! OMMY DIMPOZI AAMISHIA MAJESHI YAKE KWA JOKATE, SOMA HAPA HABARI KAMILI




kupitia Gazeti la Makorokocho leo mezani tumepata story ya muda mrefu ya Penzi la siri kati ya Ommy Dimpoz na Jokate aka Kidoti.
stori hii ilivuja baada ya beef la chini kwa chini kati ya Jokate na mwimbaji mmoja wa kike ambae hawana maelewano mazuri na chanzo kikidaiwa kuwa ni mwanamuziki huyu wa kike (jina lake linaanzia na herufi V)
kukuta meseji za Mapenzi kati ya Mpenzi wake huyo na dada yetu kidoti.
Chanzo kinasema kidoti na Ommy Dimpoz walianza mapenzi ya siri kwa siri baada ya dada huyo kuachana na diamond.
Mapenzi hayo yalianzia huko mikocheni A ambapo Ommy Dimpoz alikwa akiishi nyumba ya kushare na kila bibie kidoti alipokuwa akienda hapo watu walimuona na kuna kipindi dada yetu kidoti alikuwa akiminya ndani ya gari bila kushuka mahaba yakiwa tele kwenye gari hilo.
sasa wataalamu wa mambo wanasema dada yetu huyu anaonekana sana maeneo ya kinondoni katika mjengo wa kupanga wa star huyu wa ndagushima chande na mapenzi yao bado inasemekana yanaendelea chini kwa chini lakini nje nje.
ommy dimpoz ameingizwa kwenye list ya wanaume walio na mapenzi ya siri na dada yetu kidoti.
patamu hapoooo.
kama namiona vile
CREDIT : SOUDY BROWN
    

CHID BENZ AMWAGA MACHOZI CLOUDS ALIVYOKUWA ANAELEZEA STORY YA DIAMOND KABLA HAJAKUWA STAR


 
Chidi Benz alitabiri mbele ya Diamond Platnumz (wakati bado underground) kuwa angekuja kuwa msanii mkubwa.
Hata hivyo maneno muhimu ambayo rapper huyo alimwambia Diamond ni kuwa asije kunywa pombe wala kuvuta (unga/bangi) maishani mwake.
Chidi ambaye Jumanne hii ameachia single yake mpya 'Mpaka Kuche' aliyowashirikisha Diamond na AY, alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM. Katika kuashiria kuwa hiyo ilikuwa ni interview iliyogusa sehemu ya katikati kabisa ya moyo wake, Chidi alijikuta akibubujikwa na machozi.

Chidi alikumbushia siku Diamond alipompigia simu kujitambulisha kwake kuwa ni msanii mchanga anayetaka kumshirikisha kwenye wimbo wake. Hata hivyo siku Diamond amefanikiwa kumpata Chidi hewani ilikuwa ni baada ya kujaribu kumtafuta kwa siku nyingi bila mafanikio na aliwahi kumweleza mama yake namna alivyo na hamu ya kumshirikisha rapper huyo aliyekuwa akimkubali.
Baada ya kumpigia simu, Chidi anadai alimuambia Diamond aende kwao maghorofani Ilala wakazungumze vizuri.
"Sasa nikamuona (Diamond) nikajua huyo dogo ndio yule niliwaambiaga watu kuwa ‘huyu dogo ana sura moja hivi imekaa.. sura yake lazima utaiongelea tu, lazima utasema kitu, namuona atakuja kuwa staa tu, simjui lakini the way alivyo, atakuja kuwa staa,” alikumbushia Chidi.

HAYA SASA KUMEKUCHA BIFU LA ALI KIBA NA DIAMOND, ALIKIBA ANENA TENA...MSIKIE HAPA


Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na
tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu
waache kuwakosanisha.
Akizungumza na Bongo5 leo, AliKiba amewataka
watu kuachana na tabia ya kuwagombanisha
Diamond ili wafanye muziki mzuri.
“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na
Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti fake
za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema
kuna wengine wanafanya for fun na wengine
wanafanya ili kutukosanisha wengine wanafanya
lakini hawajui wanachofanya,” amesema Alikiba. “Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali
waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu
mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina
mambo hayo. Ninachowataka waendelee kusupport
kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi
ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania.
Wanapotupa moyo wao sisi tunazidi kukaza buti ili
tufike mbali zaidi. Watu wanaotengeneza ugomvi
wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye
kusupport muziki na watuambie ni mapungufu gani
ambayo yamepungua ili tujirekebishe,” ameongeza.
Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia
mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso
pamoja na ujio wa video zake. “Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama
nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani
yale malalamiko ya maana walikuwa wakilalamika
kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu
wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo zenyewe
zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya
kuelimisha na kuchezeka na ya kufurahisha.
Maandalizi ya video yapo tayari na booking ipo
tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla
sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni
hapa siwezi sema ni nchi gani bado ni mapema
nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa
track mbili moja itafanyika hapa na nyingine
itafanyika nje.”
   

AIBU...!!!! Baby Madaha Anusurika Kubakwa baada ya kupanda jukwaani akiwa na kivazi cha nusu uchi


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha amenusurika kubakwa nchini Kenya baada ya kupanda jukwaani akiwa ametinga kivazi cha nusu utupu.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu kubwa ya mapaja wazi, wanaume wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu.

“Nusura Baby Madaha abakwe, wanaume wakware walishindwa kuvumilia, palepale jukwaani wakaanza kumvuta huku wengine wakimng’ang’ania paja lake lakini aliokolewa na mabaunsa vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine,” kilisema chanzo.
Staa wa filamu Bongo, Baby Madaha
Staa wa filamu Bongo, Baby Madaha


Mpekuzi imezinasa picha kadhaa zinazomuonesha Baby Madaha akiwa anang’ang’aniwa na wanaume tofauti huku wengine wakimchungulia sehemu zake ‘muhimu’ pamoja na kumshika mapaja yake.

“Kweli ilikuwa ni hatari siku hiyo maana wanaume waliniganda balaa kila nilipokuwa naimba jukwaani walikuwa wakinivutia kwa huku chini walikokuwa wamesimama lakini niliokolewa na mabaunsa, hata hivyo shoo ilikuwa na mzuka sana,” alisema Baby Madaha.

Kwenye shoo hiyo iliyokuwa na nyomi ya kutosha, Baby Madaha alikamua vilivyo sambamba na wasanii wakali kutoka Kenya akiwemo Jua Kali na Wayree. 
Baby Madaha akifanya shoo na kunengua jukwaani akiwa ametinga sketi fupi.
Baby madaha akizidi kuwapagawisha wakenya.
Wanaume wakiung’ang’ania mguu wa Baby madaha.
Baby Madaha akiwa ameanguka chini baada ya kuvutwa na watazamaji waliokuwa karibu na jukwaa.
Baby Madaha akipata akiwa na baadhi ya mastaa kutoka Kenya.

YOUNG KILLER APIGWA HADI KUZIMIA ALIPOGUNDULIKA TU ANAFANYA MUZIKI

Mama wa msanii wa muziki wa Hip Hop Young Killer Msodoki, amesema kuwa anafurahishwa sana na kipaji cha mtoto wake ambacho kinaendelea kuonekana siku hadi siku licha ya kwamba mwanzoni aliwahi kumkataza kwa kumpiga mwanaye huyo mpaka kuzimia ile aachane na muziki.


Young Killer akiwa na mama yake

Mama Msodoki alikuwa akizungumza na Bongo5 jana jijini Mwanza.

“Kwanza namshukuru Mungu kwa kufanya mwanangu kufikia hapa alipo,” alisema. “Sasa hivi Young Killer anakaribia kumaliza nyumba yake, familia inamtegemea kwa sababu mimi niliona akifanya huu muziki na umri mdogo unaweza ukamwathiri, lakini nikashanga kaamua kuondoka nyumbani na kwenda Dar. Young Killer aliondoka tu bila kuniaga, siku hiyo akanipigia simu akaniambia ‘mama save hiyo namba yangu, mimi nipo Dar’.
Nikamuuliza kuna nini huko akasema ‘mama hebu niache kwanza’. Baada ya hapo nilikuwa nawasiliana na kaka yake ananiambia ‘mdogo wangu yupo hapa nyumbani’ nikamwambia ‘shule vipi? wewe utakaaje na mwenzako wakati unajua ni mwanafunzi!’ Akaniambia ‘mama nikiishi naye vizuri wewe naomba uniache kwa sababu naona hii ni talent yake hatoweza kusoma tena sasa hivi’ nikasema ‘mrudishe’ akasema ‘mama muache kwanza tusimrudishe,” aliongeza Mama Msodoki.

“Huyu mtoto nilimpiga mpaka nikahisi kuna tatizo litamkuta, yaani nilimpiga mapaka akazimia, mpaka majirani wanasema ‘muache’ lakini unaona nikimuacha wakati nimetoa ada ili asome shule wanakwambia ‘achana naye’. Mimi sikupenda nimuache, kwasababu katika familia yangu ya marehemu Mzee Msodoki wote ndugu zake wamesoma sasa nilikuwa siwezi kumuacha asiende shule. Mimi sikutaka asifanye muziki nilikuwa nataka asome kwanza.”
Katika hatua nyingine Mama Msodoki alielezea tabia ya mwanae wakati akiwa mdogo mpaka alivyoingia kwenye muziki.

“Hakuna mtoto aliyekuwa mtiifu kama huyu,” anasema. “Alikuwa Akitoka shuleni anafika nyumbani muda unaotakiwa, huwezi ukamkuta ametoka nyumbani katika muda ambao hakutakiwa kutoka. Hayo mazoezi yake ya muziki alikuwa anafanya labla muda wa shule, kwasababu muda wa kutoka shule ukifika anakuwa yupo nyumbani. Nikitoka kazini ninamkuta yupo nyumbani na anajisomea huwezi amini. Kwahiyo hata mtu anapokwambia kwamba ‘mwanao anafanya hivi’ huwezi ukamwamini. Lakini mpaka nikafikia hatua nikafuatilia shule mahudhurio yake kwakweli yakawa sio mazuri.

TundaMan aeleza alichoshauriwa na Ali Kiba baada ya kupokea simu na kuugua,.... "inawezekana ni ushirikina"


Mwimbaji wa Tip Top Connection, TundaMan aliwashangaza wengi baada ya kueleza kuwa alipokea simu yenye namba nyingi asizozielewa na ghafla akapata mshtuko na kuishiwa nguvu, hali iliyomsababisha akimbizwe hospitali ambapo alipewa matibabu.
 
Licha ya kuwa wataalam na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) walieleza wazi kuwa kitaalam simu haiwezi kabisa kuwa chanzo cha tatizo hilo, TundaMan alisisitiza kuwa yeye ndiye aliyepata tatizo na anajua kilichotokea.
 
“Wao wanasema haiwezekani kwa sababu hilo tatizo halikuwakuta…lakini kwa kuwa mimi ndiye nimekuwa affected kwa siku mbili tatu, mimi naamini kuwa tukio hilo lipo na limekuja baada ya kupokea ile simu. Wao wanaongea kitaalam siwezi kubishana nao, lakini mimi limenikuta na nimeona.” Amesema  Tundaman
 
Kutokana na sintofahamu hiyo, Tundaman ameeleza kuwa msanii mwenzake, Ali Kiba alimshauri kwenda katika nyumba ya ibada ili apate dua maalum.
 
“Yeah inawezekana (ni ushirikina) kwa sababu vitu kama hivyo huwa vinatokea sana na ndio maana ndugu yangu Ali Kiba amenishauri nikapate dua.” Amesema Tunda Man.
 
Ameeleza kuwa tayari amechukua uamuzi huo ingawa hali yake pia inaendelea kuimarika baada ya kupata matibabu.

Baby Madaha: Wasanii Wengi ni WACHAWI



Staa  wa  kike  anayefanya  vizuri  katika  tasnia  ya  muziki  na  filamu  nchini, Baby  Joseph  'Baby Madaha'  amewatolea  uvivu  wasanii  wenzake  kwa  kuifumua  tasnia  hiyo  kuwa  asilimia  kubwa  ya  wasanii  ni  washirikina  na  wanalogana....

Msanii huyo  amewashutumu  baadhi  ya  wasanii  Bongo  kuwa  hawawezi  kufanya  jambo  lolote  muhimu  bila  kufanya  ushirikina  na  wengine  hawapendi   kuona  wenzao  wakitoka  kimaisha.....

Madaha  amefikia  hatua  ya  kufumua  ushu  hiyo  kwa  madai  kuwa  hata  kufilisika  kwake  ghafla  kumetokea  baada  ya  aliyekuwa  mpenzi  wake  raia   wa  Kenya  Joe  Kairuki  kupunguza  nguvu  ya  kumsaidia  kisanii  na  kwamba  ilitokana  na  rafiki  zake  kumpiga  juju....

"Wasanii  wenzangu  wameniloga.Walikuwa  wanaona  donge  sana  Joe  alipokuwa  akinisaidia.Kiukweli  wameniporomosha  kabisa.Nilienda  kwa  mtaalamu  akanithibitishia  hili.Hata  hivyo  nimepata  mfadhili  mwingine.Siwezi  kumtaja  wasije  wakanipiga  kipapai  tena,"  alifunguka  staa  huyo  wa  wimbo  wa  Summer Tyme.

Alisema  ushirikina  umeifanya  tasnia  ya  sanaa  kudumaa  kwa  kiasi  kikubwa  na  kwamba  imani  hiyo  imesababishwa  na  wsanii  wasio  na  elimu....

"Wasanii  wachawi  wapo  wengi  tu.Yaani  unamuona  msichana  mzuri  au  mvulana  mtanashati  msanii  kumbe  anakesha  kwa  waganga.

"Wengi  wanasafiri  sana  kwenda  mikoani  kuloga  wenzao.Sanaa  imejaa  uchuro  mtupu. Kama  si  kuelemewa  na  ushirikina  basi  tungekuwa  mbali  sana.

"Ushirikina  umesababisha  pia  fitina, majungu  na  visilani  miongoni  mwa  wasanii. Hatupendani  kwa  sabab  ya  mioyo  ya  kichawi," Alisema  Baby  Madaha

MAKALA: CHEGE CHAPA NYINGINE


Said Nassoro ‘Chege Chigunda’.
NAPOTAJA makundi yanayofanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva bila kupepesa ni lazima utalitaja Kundi la TMK Wanaume Family. Ndani yake kuna vichwa vingi ambavyo vinaunda kundi hilo na kati yao ni Aman James ‘Mheshimiwa Temba’ na Said Nassoro ‘Chege Chigunda’.
Vijana hawa wamefanya mabadiliko makubwa katika muziki ndani na hata nje ya kundi. Kuna kazi za pamoja ambazo wameimba kama vile Tunafurahi na nyingine nyingi. Kuna wakati utawasikia wakitoa wimbo kwa pamoja na wakati mwingine utamsikia mmoja-mmoja (solo).
Wakati huu, Chege ameachia wimbo wa Chapa Nyingine ambao ni miongoni mwa nyimbo ambazo zinafanya vizuri sana kwa sasa katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni.

Ukiachana na Chapa Nyingine tayari ameshawahi kufanya nyimbo nyingine kali ambazo zilitikisa Bongo kama Take Away remix ambayo aliimshirikisha Diamond Platinumz.
Katika makala hii Chege anafunguka zaidi juu ya wimbo huo na maisha yake kimuziki kwa ujumla:
Nini maana ya Chapa Nyingine?
Chapa Nyingine ni wimbo ambao umetokana na shoo tulizokuwa tukipiga tukiwa jukwaani. Ilikuwa kila tukitaka tupigiwe biti na Dj tunamwambia Chapa Nyingine na yeye anapiga nyingine tena na tuliposhuka jukwaani mashabiki wakaupenda sana msemo wa Chapa Nyingine, ikatubidi tupange na kuona ni ‘idea’ nzuri tunaweza kuifanyia kitu, ‘then’ tukaifanyia kazi na imekuwa kama unavyoiona na kuisikia.
Yule ambaye nimemshirikisha ni mwanamuziki mpya na ni mdogo wangu wa mtaani anaitwa Gift nilimsikia akiimba vizuri nikaamua nimshirikishe kwenye huu wimbo.

Vipi kuhusu kufanya kolabo nyingine na Diamond?
Nafikiri tumeshafanya na imeshatoka ambayo ni Uswazi Take Away Remix. Ikitokea nafasi nitafanya naye kazi nyingine lakini kwa sasa nipo natengeneza wimbo mpya na Temba na utatoka hivi karibuni.

Game ya sasa unaionaje?
Inaelekea pazuri kwa sababu ushindani kwa sasa ni mkubwa sana na muziki umekuwa ukitutengenezea pesa vizuri kila siku, ninachokiomba kwa serikali kama ikituchekia vizuri suala hili itakuwa ni ajira ya kudumu.

Kitu gani unakipenda katika muziki?
Kikubwa zaidi ninachokipenda ni pale unapotoa kazi na kupokelewa vizuri na mashabiki, hilo ni jambo kubwa sana la kumshukuru Mwenyezi Mungu.

Maisha ya kimuziki unayaonaje?
Ni magumu kwa kweli! Tofauti yake ni kwamba unapokuwa mtu maarufu matatizo yanakuwa mengi yaani huwezi kuwa huru, unakuwa mtu wa kukaa sehemu za kuchagua na mbaya zaidi huwezi kupanda hata daladala.
Malengo yako katika muziki ni yapi?
Kikubwa kwa sasa ni kufika mbali sana. Nimekuwa nikijitahidi kila kukicha kuhakikisha nafanya vizuri katika muziki kwa kutoa nyimbo zangu sambamba na video zenye ubora wa hali ya juu ili mashabiki wangu wafurahie na kwa hilo nadhani ninapoelekea kwa sasa ni pazuri.
Vipi kuhusu kufanya kolabo nje ya nchi?
Unajua hiyo huwa inatokea tu mtu kufanya kolabo na mwanamuziki wa nje ya nchi, kwa upande wangu bado sijaipanga akilini mwangu, kwani naamini chochote kinaweza kufanyika bila hata ya kufanya kolabo na mtu yeyote wa nje ya nchi na ukakubalika kimataifa zaidi.

Sikiliza hapa Ngoma Mpya ya TID ft Jay Moe – Chumvini

tid-jay
Sikiliza hapa ngoma Mpya kutoka kwa TID akimshirikisha Jay Moe ngoma inaitwa CHUMVINI

STORI JUU YA MASTER JAY NA MKEWE WA NDOA NA MSANII WA BONGO FLEVA ANAEDAIWA KUTEMBEA NA MKE WA MASTER JAY,,



Ingawa kuna fununu ambazo si rasmi kuhusu uhusiano wa kimapenzi kati ya Master Jay na Shaa,hapa kuna stori tofauti ambayo Soudy Brown anai-amplify kuhusu mke wa Master Jay kutoka na msanii wa Bongo fleva,hapa utamsikia Master Jay na msanii anayesemekana kumchukua Mke wa Master Jay.
88.1 Clouds Fm inasikika ukiwa Mwanza.
Bonyeza play kusikiliza.

BABY MADAHA AUMBUKA..

Baby Joseph Madaha ambaye aliwahi kutangaza kuacha fani ya maigizo na muziki amejikuta akiumbuka kwa mashabiki wake kutokana na kuendelea kukomaa katika gemu kwa kuachia kazi mpya na kuandaa matamasha mbali mbali.
Staa wa muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha akiwa kwenye pozi.
Msanii huyo alitoa uamuzi huo kwa madai kuwa alichoshwa na skendo za kila kukicha ambazo wakati mwingine zimekuwa zikimshushia hadhi katika jamii, ikiwemo skendo ya kunaswa kwenye mtego wa kujiuza ilioandliwa na Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ ya Global.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Baby Madaha alisema hawezi kupinga kama alizungumza hayo isipokuwa tangu atoe kauli hiyo amejikuta akizidi kupata mafanikio makubwa katika muziki.
“Naweza kusema nimeumbuka kwa kile nilichoongea, maana nimejikuta nashindwa kutekeleza nilichowaambia mashabiki wangu sababu dili zinakuja, siwezi kuziacha,” alisema Baby.

LINAH KUFUNGA NDOA HIVI KARIBUNI NA HUYU MPENZI WAKE

MSANII mwenye sauti mwanana anayetesa kwenye Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’, amefunguka kuwa, ndoa yake na mpenzi wake Nagari Kombo ‘Kaka wa Bongo’ inanukia. Linah akipozi na mpenzi wake Nagari Kombo wakati wa utoaji tuzo za Kili.
Linah alisema hayo wikiendi iliyopita aliponaswa akijiachia na Kaka wa Bongo katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar ambapo mpango mzima wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 – 2014 ulikuwa ukifanyika.

Msanii mwenye sauti mwanana anayetesa kwenye Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’.
“Sina haja ya kuendelea kumficha mpenzi wangu, kwani kwa sasa anatambulika kwa kila mtu na hasa ndugu zangu wa karibu, kitu cha kusubiriwa kwa sasa ni tarehe ya ndoa yetu tu,” alisema Linah.
Lina akiwa na mpenzi wake.
Kaka wa Bongo alijizolea umaarufu siku za nyuma baada ya kuingia uwanjani na kumkumbatia mchezaji, Ricardo Kaka wa Timu ya Taifa ya Brazil iliyokuwa ikichuana na Taifa Stars katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top