
Acha
kabisa! Fainali ya lile shindano kubwa la mrembo wa Miss Tanzania 2014
limechukua nafasi usiku wa kuamkia jana, Jumapili ambapo Ijumaa Wikienda
lilikuwepo ndani ya eneo la tukio kukukusanyia matukio yote yaliyojiri
mbele na nyuma ya pazia hivyo lina full story.
Warembo 30 walioshiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, wakionesha shoo ya kufa mtu.
WAREMBO 30
Baada ya
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania na Mkurugenzi wa Lino
International, Hashim Lundenga ‘Anko’ kukaribisha wageni waalikwa,
warembo 30 walioshiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania, walionesha
shoo ya kufa mtu kupitia kwa msanii wa nyimbo za asili, Wanne Star.
Vanessa Mdee akifanya makamuzi jukwaani
VANESSA AFUNIKA Kabla ya mambo mengine
kuendelea, Vanessa Mdee alifunika kwa bonge la shoo alilokamua ,
akisindikizwa na wacheza shoo wake wawili ambao walikamua ile mbaya.
MVUTO KWENYE PICHA Aliyeibuka kidedea kwenye kipengele hicho ni Evelyn Bassah huku Kipengele cha Top Model, mrembo Jihan Dimach akijitwalia taji.
Warembo walifanikiwa kuingia Top Five.
KIPAJI Katika Kipengele cha Miss Talent
(kipaji), taji lilikwenda kwa Nicole Sarakikya, Elizabeth Tarimo
akaibuka kidedea kwenye Kipengele cha mwanamichezo mwanamke (Sports
woman) huku Miss Personality ikitwaliwa na Salama Saleh.
KIFUTA JASHO Baada ya kuenguliwa warembo 15, wale top 15 waliosalia walilamba Sh. laki saba kila mmoja kama kifuta jasho.
TOP 5 Washiriki waliofanikiwa kuingia kwenye Tano Bora ni Jihan Dimach, Siti Mtemvu, Dorice Mollel, Nasreen Abdul na Lilian Kamazima.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia shoo.
WAVALISHWA KAMA NDEGE TAUSI Bila shaka unawajua
ndege tausi hasa wale wanaoonekana pale Ikulu ya Magogoni. Warembo hao
walioingia Top 5 walikuwa wamevalishwa kama ndege huyo isipokuwa rangi
kwa namna walivyoonekana jukwaani.
MREMBO AMWAGA KIFARANSA Wakati wa kipindi cha
maswali na majibu, mrembo Siti Mtemvu aliwaacha watu midomo wazi
aliposema atajibu kwa Kiingereza lakini baada ya kumaliza kumwaga
ung’eng’e, akamalizia kwa kutema Kifaransa.
Meza ya majaji ikijipanga kutoa uamuzi wa mwisho katika kinyang'anyiro hicho.
MWINGINE ACHEMKA Naye mrembo mwingine, Nasreen
Abdul alijikuta akichemka kujibu maswali hivyo kuzomewa hasa pale
alipochanganya kati ya maneno tourism (utalii) aliloulizwa na terrorism
(ugaidi).
JIHAN ALA SHANGWE
Kwenye ‘segmenti’ ya maswali na majibu, mrembo Jihan alijikuta akipokea shangwe la kufa mtu kwa kujibu vizuri kwa ung’eng’e.
Siti Mtemvu (Miss Tanzania 2014 ) akiwa na anyedaiwa ni baba yake, Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu.
VITUKO VYATAWALA Vituko vilivyojiri vilikuwa
vingi kwa mfano katika shoo ya msanii Vanessa Mdee aliyetumbuiza katika
shindano hilo, alijikuta akiachia ‘nido’ moja nje wakati akicheza na
kuchafua hali ya utulivu, akaibua zomeazomea ya ‘weweeeee’.
nyuma ya pazia
Kituko kingine ni cha mtangazaji maarufu
Bongo, Gardner G. Habash kutinga ukumbini akiwa ameongozana na kale
kabinti ambako katika siku za hivi karibuni, amekuwa akionekana akiwa
beneti nako bila Lady Jaydee kujua.
Ommy Dimpoz akipiga shoo katika fainali hizo
Baada ya shoo kali ya Ommy Dimpoz, washiriki walioingia fainali,
walipanda tena jukwaani ambapo Mkurugenzi wa Lino International, Hashim
Lundenga naye alipanda jukwaani na kuanza kuwatangaza washindi, kuanzia
namba tano mpaka namba moja.
Nasreem Abdul alishika nafasi ya tano, nafasi ya nne ikaenda kwa Dorice Mollel.
TOP THREE
Jihan Dimach
alitangazwa kuwa mshindi wa tatu (second runner up) wakati Lilian
Kamazima, alishika nafasi ya pili (first runner up).
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania na Mkurugenzi wa Lino International, Hashim Lundenga ‘Anko' (kushoto) akisimamia shoo.
Nafasi ya kwanza, ilishikwa na Siti Mtemvu, mrembo kutoka Temeke
ambaye alitawazwa kuwa Miss Tanzania 2014 na kuvalishwa taji na Miss
Tanzania 2013, Happiness Watimanya.
Pia Siti alijishindia shilingi milioni 18 za Kitanzania kama zawadi
kwa ajili ya mshindi wa kwanza huku Lilian na akiondoka na shilingi
milioni 6 za Kitanzania na Jihan akiambulia milioni 4.2.
MSHINDI ALIJULIKANA MAPEMA?
Swali kubwa ambalo wadau wengi wa mashindano ya umiss Tanzania walijiuliza usiku huo ni kwamba, je, mshindi alijulikana mapema?
Mashabiki wakipigia debe na kutoa sapoti kwa Mrembo Siti Mtemvu katika kinyang'anyiro hicho.
Viashiria vya mapema vilionesha kwamba, Siti ambaye inadaiwa ni mtoto
wa Mbunge wa Temeke (CCM), Abbas Mtemvu angeibuka mshindi kutokana na
jinsi alivyokuwa akishangiliwa kwa nguvu huku wapambe wake wakiinua
vipeperushi vyenye picha ya mshiriki huyo, hali ambayo haikuwepo kwa
wenzake.
Waandishi: Issa Mnally, Gabriel Ng’osha na Musa Mateja