Habari Kali
Loading...

BAADA YA KULA BATA NA BENZEMA RIHANNA AREJEA NYUMBANI!


Staa wa Pop, Rihanna.
Los Angeles, Marekani
BAADA ya kula ‘bata’ na mwanasoka kutoka Real Madrid, Karim Benzema,staa wa Pop, Rihanna ameamua kurejea nyumbani kwake.
Juzikati, Rihanna alinaswa katika Uwanja wa Ndege wa LAX pande za Los Angeles akiwa ndani ya suruali ya kijeshi na jaketi jeusi tayari kupanda ndege kuelekea kwake, New York.Rihanna 27,alilipotiwa kuwa katika uhusiano na Benzema ambapo hivi karibuni walinaswa wakipata chakula cha jioni pande za Santa Monica.

PETER WA P-SQUARE AFUNGUKIA BIFU LAO

Peter Okoye.
PETER na Paul Okoye wamekuwa wakikwaruzana kila mara kiasi cha kuwashangaza watu ila Peter ameamua kuweka wazi kuwa, kugombana kwao kusichukuliwe kama kitu cha ajabu kwani nao ni binadamu Akizungunza na mtandao mmoja nchini humo. Peter alisema kuwa kutofautiana kwao ni jambo la kawaida na imekuwa ikitokea hivyo mara nyingi lakini baadaye maisha yanaendelea.
P-square.
“Huwa inatokea kutofautiana kwa hapa na pale kama inavyotokea kwa wengine, tunakwaruzana kisha tunaweka mambo sawa.Huwa tunazinguana ile mbaya lakini kesho yake tunaenda stejini pamoja na kufanya shoo na hakuna anayejua. “Yaani sisi ni sawa na wanandoa walioishi zaidi ya miaka 20, lazima kuna siku wanatofautiana,” alisema Peter.

DIAMOND: TAYARI NIMEMVALISHA PETE YA UCHUMBA ZARI, KUINGIA KATIKA NDOA MWAKA HUU

Diamond na mpenzi wake Zari katika Exclusive One on One Interview ya Power Breakfast ya Clouds FM na 360 ya Clouds TV.
STAA wa Bongo Fleva nchini, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' amefunguka kuwa tayari amemvalisha pete ya uchumba mpenzi wake Zarinah Hassan 'Zari' na anatarajia kupata mtoto wa kike mwaka huu.
Diamond ameyaongea hayo hivi punde katika Exclusive One on One Interview ya Power Breakfast ya Clouds FM na 360 ya Clouds TV kuelekea katika shoo ya Zari All White Party itakayofanyika leo usiku katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.
Katika mahojiano hayo ambayo Diamond ameambatana na mpenzi wake huyo, ameongeza kuwa anatarajia kuingia katika ndoa mwaka huu.
Kwa upande wa Zari yeye amefunguka kuwa bado hajajua jina watakalompa mtoto wao wa kike anayetarajiwa kuzaliwa mwaka huu ila watampatia jina zuri la Kiislam na lenye mvuto.

D’BANJ AJIGONGA KWA MPENZI WA ZAMANI

Mwanamuziki kutoka Nigeria D’ Banj.
INAVYOONEKANA bado mwanamuziki D’ Banj analo penzi la kweli kwa mpenzi wake wa zamani, Adama Indimi baada ya juzikati kujigonga kwake kwa kumtumia ujumbe mzuri mama wa demu huyo katika siku yake ya kuzaliwa.
Aliyekuwa mpenzi wa mwanamuziki D’ Banj Adama Indimi.
Jamaa alifanya hivyo kupitia mtandao wa Instagram ambapo mbali na kumtakia heri ya kuzaliwa, pia alimuelezea mama huyo kama mkarimu na mpenda watu.
Achilia mbali hilo, D’ Banj pia akaposti ujumbe mwingine, safari hii akiuelekeza kwa dada wa Adama, Meran Indimi aliyetimiza miaka 25 juzi ambapo naye alimuelezea kama mrembo na sapota wake namba moja.
Meseji hizo zilitafsiriwa kuwa ni kama jamaa anajigonga kwa Adama na amejaribu kufikisha ujumbe kupitia ndugu zake.

DIAMOND, ZARI WAFANYIWA EXCLUSIVE INTERVIEW CLOUDS TV/RADIO

Diamond na mpenzi wake Zari katika Exclusive One on One Interview ya Power Breakfast ya Clouds FM na 360 ya Clouds TV.
Diamond akimuweka sawa mpenzi wake.
Mtangazani mwenye jina kubwa wa Radio Clouds FM, Gerald Hando 'Mzee Mnoko' (kushoto) na Edson Kamoga wa 360 ya Clouds TV (kulia) wakiendelea kufanyia mahojiano Diamond na Zari.
Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo akisoma meseji za mashabiki waliokuwa wakifuatilia mahojiano hayo.
Baadhi ya wadau wa Clouds TV, Radio (kulia) wakipata kifungua kinywa kilichokuwa kimeandaliwa.
P Diamond na Zari wakiwa katika pozi na wadau wa Clouds TV, Radio baada ya mahojiano.
Wakati wakitoka.
Wadau wakiwa kwenye gari la Diamond wakati akijiandaa kuondoka mahali hapo.
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)

Tatizo la Kushindwa Kuzaa: Wema Sepetu Akubali Waganga 26 Kumtibu


Kufuatia  tatizo la kushindwa kupata ujauzito alilonalo msanii maarufu Bongo, Wema Sepetu, hivi karibuni waganga wapatao 26 kutoka sehemu mbalimbali nchini walijitokeza na kuomba kuunganishwa na staa huyo ili wamtibu.

Waganga hao wa tiba asilia pamoja na madaktari kutoka hospitali mbalimbali kwa nyakati tofauti walipigia simu  na kueleza kuwa, wanashangaa kuona Wema anakosa amani wakati wao wanaweza kumtibu na kuweza kuitwa mama kama wenzake.
 
“Unajua wapo wanawake ambao wanakosa amani kwa mambo ambayo hawastahili, hili la Wema kutopata mtoto linatibika, mpeni namba yangu kisha anitafute,” alisema mmoja wa wataalam hao aliyeomba jina lake lisiandikwe.
 
Katika kujua Wema anapokeaje ofa aliyopewa na waganga hao, alitafutwa na alipopatikana alikubali mara moja kutibiwa tatizo alilonalo lakini akatoa angalizo.
 
“Kuna watu wengi sana ukiacha ambao wamejitokeza kwenu, mimi nina meseji zaidi ya 400 ambazo nimetumiwa kwenye namba yangu ya WhatsApp na simu kibao nimepigiwa watu wakijitolea kuja kushughulikia tatizo langu, kiukweli kabisa nipo tayari.
 
“Lakini ni vizuri wakati naanza kutibiwa tayari nikawa na mwenza wangu ambaye tutakuwa tumekubaliana na pale tatizo litakapoisha, iwe rahisi kuzaa mara moja,” alisema Wema.

BAADA YA KUZIMIA KWA MIEZI MIWILI, BOBBI KRISTINA AZINDUKA

Bobbi Kristina.
Bobbi Kristina ambaye ni mtoto wa nguli wa muziki Bobby Brown na marehemu Whitney Houston, amezinduka baada ya kupoteza fahamu kwa zaidi ya miwili kutokana na kilichoelezwa kuwa ni matumizi ya dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tovuti ya MTV na kuthibitishwa na Bobby Brown na shangazi yake, binti huyo amefumbua macho na sasa hatumii tena mashine ya kumsaidia kupumua. Binti huyo alikuwa mahututi kwa zaidi ya siku 75 na alikuwa akipatiwa matibabu baada ya kukutwa ndani ya jakuzi nyumbani kwake januari 31, mwaka huu akiwa hajitambui.
Kupitia ukurasa wa Facebook, Brown aliandika: “Kweli Mungu ni mkubwa, mpenzi wangu, binti yangu amefumbua macho na kunitazama. Ndiyo, hatumii mashine ya kupumulia tena, anapumua mwenyewe ingawa bado anapatiwa matibabu.

MASTAA WANAOONGOZA KWA SKENDO ZA NGONO

Mwandishi wetu
Mastaa mbalimbali wa Bongo wamekuwa wakiandamwa na skendo huku baadhi wakiona ndiyo njia ya kujing’arisha kisanii.Skendo zao zimekuwa za aina mbalimbali lakini wengi wamekuwa wakiandamwa na skendo za ngono.Katika makala haya utaipata Top 10 ya mastaa wa kike waliondamwa na skendo za ngono. Baadhi wamekumbwa na skendo za kunaswa kwenye mitego ya kujiuza na wengine wakiingia kwenye listi hii kutokana na tabia ya kubadili wanaume kama nguo.
Jokate Mwegelo.
Kwa maana hiyo kumi bora hii itawagawa katika Kundi A na B ambapo Kundi A ni la wale ambao walikanyaga skendo ya kujiuza na Kundi B ni la waliogandwa na skendo ya ngono kwa tabia zao za kubadili wanaume.
KUNDI A
Mmoja kati ya mastaa wanaoingia kwenye kundi hili ni Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’. Huyu aliwahi kuwekewa mtego na kunaswa baada ya kukubali kujiuza kwa mwanaume aliyemtajia dau kubwa na hatimaye akaingia mkenge.
Lulu Semagongo; aliwahi kuingia kichwakichwa kwenye mtego kama wa Jack Chuz ambapo naye aliwahi kutegeshewa mwanaume na kuulizwa kama anaweza kukubali kuuza ngono kwa kiasi gani.
Wema Sepetu.
Kuashiria kuwa ndo’ zake, akitoa dau lake na mchezo ukaenda hadi gesti ambapo alifumwa laivu na mwanaume huyo kitandani.Baby Madaha; Licha ya kipindi f’lani kudaiwa kuwa kwenye uhusiano na meneja wake aitwaye Joe Kairuki, aliwekewa mtego kwa kutumiwa meseji na mwanaume kuulizwa kama wanaweza kukutana faragha na kwa kiasi gani ambapo naye alitoa dau lake.
Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’.
Hata hivyo, baadaye alishtukia mchezo licha ya mawasiliano yake na mwanaume huyo kuonekana wazi kwamba alikuwa anaelekea kuingia kingi. Isabella Francis ‘Vai wa Ukweli; Naye aliwahi kudaiwa kuyaendesha maisha yake kwa kuigiza na kujiuza pia, akawekewa mtego kama ilivyo kwa wenzake na siku ya tukio, alifika hadi ‘kiwanja’ huku akisisitiza kwamba fedha mbele. Kutokana na maelezo yake hayo, ikaonekana ni kweli huwa anafanya k’abiashara hako’ haramu.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
KUNDI B
Hili ni wale ambao wanasifika kwa katabia ka’ kubadili wanaume kama nguo.
Elizabeth Michael ‘Lulu’; Kiumri anaonekana mdogo lakini naye yumo. Huyu aliwahi kuripotiwa kuwa kwenye uhusiano wa siri na marehemu Steven Kanumba kisha baadaye akadaiwa kutoka na mheshimiwa John Komba (marehemu ambaye aliwahi kukanusha uvumi huo).
Pia binti huyo anadaiwa kuwa eti alikuwa mpenzi wa huyu bilionea wa Arusha aliyefariki dunia, juzikati aitwaye Lusekelo Samson ‘Seki’ ambaye kuna kipindi pia Husna Maulid na Lulu waliwahi kudaiwa kugombana kisa kikiwa ni mwanaume huyo.
Wema Sepetu
Ukiacha wale ambao sisi hatuwajui, Wema amekuwa na msururu wa wanaume huku staili yake ikiwa ni ile ya bandika-bandua. Wanaume ambao wengi ni mastaa waliowahi kumgusa ni Herry Samir ‘Mr Blue’, marehemu Steven Kanumba, Hartman Mbilinyi, Yusuf Jumbe, Chaz Baba, CK na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Huyu pia aliwahi kupiga picha za utupu kadhaa katika kipindi chake cha ustaa, hali inayomfanya afiti kwenye Top 10 hii.
Jacqueline Wolper.
Jokate Mwegelo; ni mwanadada anayeonekana mpole sana lakini naye hawezi kukosekana kwenye orodha hii. Ni kati ya mastaa waliowahi kuwa na uhusiano na wanaume mbalimbali wakiwemo Hasheem Thabit, Diamond aliyempora kutoka kwa Wema na wengine ambao amekuwa akifanya siri.Pia ni kati ya mastaa wanaopenda sana kupiga picha za nusu utupu, tabia inayomfanya wakati mwingine atafsiriwe kuwa anatangaza biashara.
Jacqueline Wolper; Anaingia kwenye orodha hii kutokana na ukweli kwamba amekuwa akibadili wanaume mara kwa mara huku wakati mwingine akiingia kwenye migogoro ya kugombea wanaume.Aliwahi kuingia kwenye mvutano na Husna Maulid wakimgombea mwanaume aitwaye Radjabu Mwami. Pia mwanadada huyu amekuwa akihusishwa na kale kamchezo ka’ usagaji ambapo mwenyewe amekuwa akikanusha mara kwa mara.
Agness Gerald ‘Masogange’.
Agness Gerald ‘Masogange’; Nani asiyemjua mwanadada huyu kwa kupiga picha za nusu utupu huku akidaiwa kuwa ni mmoja wa mastaa ambao wanaendesha maisha yao kwa kutegemea wanaume?Mkanda wake wa ngono uliwahi kuvuja na mwenyewe amekuwa hajali kulianika umbo lake tata.
Stara Thomas; ni staa ambaye amekuwa kwenye gemu la muziki kwa muda mrefu.  Naye anaingia kwenye orodha hii kutokana na madai kuwa, aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa siri na marehemu Adam Kuambiana. Pia hivi karibuni mwanaume aliyedaiwa kuwa ni mumewe aitwaye Raumu Ally alimfumania na mwanaume mwingine.
Hao ni baadhi ya mastaa ambao wanaingia kwenye orodha.

RIHANNA AJIACHIA FUKWE ZA HAWAII, MAREKANI

Mwanamuziki, Robyn Rihanna Fenty (27) 'Rihanna' akitembea akiwa kashika glasi ya juisi  katika fukwe za Hawaii, Marekani  jana Jumapili.
Rihanna akijiachia na marafiki zake katika fukwe hizo. Kushoto ni rafiki yake wa karibu Melissa Forde.
Picha alizoiweka Rihanna katika akaunti yake ya Instagram akijiachia katika fukwe za Hawaii.

Lulu afuta akaunti yake ya Instagram kufuatia kifo cha mtu aliyedaiwa kuwa mpenzi wake!

Muigizaji wa filamu, Elizabeth ‘Lulu’ Michael mwenye wafuasi wengi kwenye Instagram, ameamua kujiondoa baada ya kushambuliwa kwa matusi na baadhi ya watu kufuatia kifo cha mtu aliyewahi kuwa mpenzi wake.

Kufuatia kifo cha kutatanisha cha Lusekelo Samson Mwandenga ‘Secky’, watu wengi walianza kumtukana Lulu wakimhusisha pia na kifo hicho huku pia wakipost picha zinazomuonesha alipokuwa na marehemu.

Hata hivyo mujibu wa Global Publishers, familia ya Secky imeweka wazi chanzo halisi cha kifo chake.

Familia hiyo imeeleza kuwa marehemu aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba mtoto wake nyumbani kwake kisha akapelekwa hospitali na baadaye kufariki dunia akiwa huko.

Katika hatua nyingine msanii mkongwe wa filamu, William Mtitu amefunguka na kuwataka watu kuacha kumshambulia Lulu kwa kitu ambacho hahusiki nacho.

“Lulu ni msanii mdogo sana kiumri na amepitia mitihani mikubwa sana katika maisha ambayo mimi na wewe kabda tusingeiweza kuikabili plz nawaomba tumuache kwa sasa inatosha jamani kumbukeni huyu ni binadamu na moyo kama nilivyokuwa mimi na wewe hivi utajisikiaje km utasikia lulu amejizulu kwa namna yeyote ile kutokana na maneno yako ya kumshambulia mitandaoni,” ameandika kwenye Instagram.

“Kumbukeni sisi ni banadamu atuijui leo yetu itaishaje wala kesho yetu itakuwaje? Plz inatosha sasa watanzania wenzangu. MTAARIFU NA MWINGINE.”

Miaka miwili iliyopita Lulu aliwahi kukaa jela kutokana na kushtakiwa kwa kumuua bila kukusudia Steven Kanumba aliyekuwa mpenzi wake.

MASTAA BONGO MUVI NJAA TUPU!mas


Waandishi wetu
Imevuja! Uchunguzi uliofanywa na Ijumaa Wikienda umebaini kwamba mastaa wengi wa sinema za Kibongo wapo katika hali ngumu kiuchumi kutokana na soko la filamu kudorora huku wizi wa kazi zao na kusitishwa mikataba yao na makampuni makubwa ya usambazaji vikichangia.
Uchunguzi huo umebaini kwamba moja ya makampuni yaliyositisha mikataba ya wasanii ni Steps Entertainment ambao wamesababisha mastaa kibao kushindwa kutengeneza muvi kwa kuwa awali walikuwa wakipewa bajeti na Steps kisha kuwauzia kwa bei ya mapatano.
Ilibainika kwamba baada ya Steps kuachana na utaratibu huo na kudai kuwa wanachukua muvi zilizoandaliwa na makampuni binafsi za mastaa wachache kama Jacob Steven ‘JB’, Athuman Amri ‘Mzee Majuto’, Vincent Kigosi ‘Ray’ na wengine wenye makampuni binafsi.
Mmoja wa mastaa wakubwa wa filamu, Musa Issa ‘Cloud 112’ alikiri kuwepo kwa hali hiyo huku akifafanua kuwa Steps kuna wakati inakuwa kwenye kipindi kigumu.

ZARI AZUIWA KUJIFUNGULIA A. KUSINI


Imelda Mtema
Stop! Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemzuia mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwenda kujifungulia nje ya Bongo pindi mambo yatakapokuwa tayari.
                             Mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Habari zilizonyakwa na Ijumaa Wikienda kutoka kwenye chanzo cha ndani ya familia ya Diamond zilieleza kwamba, tayari jamaa huyo amemuanzishia Zari kliniki Bongo.
Mkali wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mama kijacho wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
“Yaani Diamond hataki kabisa Zari kwenda kujifungulia South Africa (Sauzi). Anataka kila kitu kifanyike hapahapa Bongo. Tayari amemuanzishia kliniki kwenye Hospitali ya AMI (ipo Masaki, Dar),” kilitonya chanzo hicho.
Akizungumzia ishu hiyo, Diamond alisema kuwa anatamani kuwa karibu na mama kijacho wake huyo hivyo ni kweli anataka mwanadada huyo ajifungulie Bongo.

Diamond au Baba Kijacho alisema lengo la kufanya hivyo ni ili iwe shangwe kwa familia nzima tofauti na atakapojifungulia nje ambapo familia italazimika kusafiri kwenda kumuona Chibu Junior.
Kwa mujibu wa Diamond, Zari ambaye ni mama wa watoto watatu akifukuzia huyo wa nne anatarajia kujifungua kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka huu.

MSHANGAO MISS TANZANIA 2014

Na Erick Evarist
Mshtuko! Siku chache baada ya kutwaa Taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu ameibua mshangao wa aina yake kutokana na utata wa umri wake, Ijumaa limesheheni data.
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akionesha cheti mara baada ya kuhitimu masomo.
Utata huo uliibuka saa chache mara baada ya shindano hilo kufanyika Oktoba 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar ambapo wadau mbalimbali walianza kuhoji.
UTATA WENYEWE HUU HAPA
Mara baada ya mrembo kutangazwa mshindi, habari za chini kwa chini zilidai kwamba Sitti alijinasibu kuwa ana umri wa miaka 18 na elimu ya (digrii mbili) (masters), mambo ambayo yaliwashtua wengi na kuanza kuhoji uhalali wa umri huo ukilinganisha na kiwango chake cha elimu.
“Mh! Haiwezekani, kama ana miaka kumi na nane atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili?” Alihoji mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini.
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akipozi.
ELIMU YA BONGO IKOJE?
Kwa mfumo wa elimu nchini ulivyo, mtoto huanza darasa la kwanza akiwa na kati ya miaka mitano hadi saba, jambo ambalo haliingii akilini kwa Sitti kwani hesabu zinakataa hata kwa mtu asiyesomea mahesabu.
Ukiachilia mbali shule ya awali (nursery) ambayo huchukua kati ya miaka miwili hadi mitatu, ukihesabu miaka saba ya elimu ya msingi (primary), miaka minne ya sekondari (ordinary level), miaka miwili ya kidato cha tano na sita (advanced level) na miaka mitatu ya shahada kwanza (bachelor degree), jumla ni miaka 16.
Mlimbwende, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
Pia kuna madai kwamba ametumia mwaka mmoja kusomea shahada ya pili (masters) huku kukiwa na muda ambao kwa kawaida huwa unapotea baada ya kumaliza kidato cha nne kwenda cha tano na baada ya kumaliza kidato cha sita kwenda chuo kikuu.
INA MAANA ALIANZA DARASA LA KWANZA AKIWA NA MIAKA MIWILI?
Kwa mantiki hiyo, kama kweli Sitti ana umri wa miaka 18, basi atakuwa alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo ni msamiati mpya kwa jamii ya Kibongo.
Mrembo, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akifurahia jambo na marafiki zake wa mamtoni.
BABA MZAZI ANASEMAJE?
Ili kuondoa utata na tafrani inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii hadi kufikia hatua ya watu kutukanana, gazeti hili lilimtafuta baba mzazi wa Sitti ambaye ni Mbunge wa Temeke, Dar kwa leseni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu alipopatikana alifunguka:
“Umri wake ni kama alivyosema mwenyewe siku ile (miaka 18), kama mnataka kujiridhisha nendeni hata huko Miss Tanzania mtaoneshwa passport (hati ya kusafiria) yake…,” alisema mzazi huyo huku akiomba aachwe kwanza ashughulikie wananchi wa jimboni kwake.
Sitti Abbas Zuberi Mtemvu akiwa na baba yake, Mhe. Abbas Zuberi Mtemvu.
TUMUAMINI MZAZI?
Hata kama tukiamini maelezo ya mzazi, maana yake ni kwamba mrembo huyo alianza darasa la kwanza akiwa na miaka miwili, jambo ambalo linazidi kuongeza utata katika sakata hilo.
AKATAA KUHITIMU MASTERS
Alipobanwa zaidi kuhusu taarifa zinazosema kuwa mwanaye amehitimu masters, mzazi huyo alikanusha na kudai kwamba mwanaye amehitimu bachelor degree (shahada).
“Kuhusu masters mnakosea, mwanangu hana masters, ana bachelor, nilimshauri achukue masters lakini akaomba nimuache ashiriki kwanza mashindano ya u-miss ndiyo aje aendelee baadaye,” alisema mheshimiwa huyo.
Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu wakati wa kutwaa taji
NI AIBU NYINGINE KWA LUNDENGA?
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari, suala la warembo kudanganya umri limekuwa ni sugu hivyo kuleta tafsiri ya aibu kwa muandaaji wa mshindano hayo, Hashim Lundenga akidaiwa kupigwa changa la macho pindi anapowapokea katika mchakato wa awali.
Pasipoti ya kusafiria ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
“Hii ni aibu nyingine kwa Lundenga kwani haiwezekani mtu akaingia akasema ana miaka kumi na nane halafu awe na elimu kama hiyo, anashindwaje kulibaini hilo mapema?” Alihoji mdau mkubwa wa urembo nchini akikumbushia kisa cha Wema Isaac Sepetu, Miss Tanzania 2006/07 ambaye naye alidanganya umri akasema ana miaka 18 wakati alikuwa na kumi na saba.
Leseni ya udereva ya Miss Tanzania 2014, Sitti Abbas Zuberi Mtemvu.
MSIKIE LUNDENGA SASA
Alipotafutwa Lundenga ili kuzungumzia suala hilo, alijibu kwa kifupi na kukata simu:
“I can’t answer that question (Siwezi kujibu swali hilo)…siwezi.”
SITTI ANASTAHILI KUWA NA UMRI GANI?
Ukiachilia mbali muonekano, baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa ukifuata utaratibu wa mfumo wa elimu Bongo, Sitti alipaswa angalau awe na umri wa miaka 23, hata kama madai ya kurushwa madarasa ni sahihi.
Muandaaji wa mshindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga akifafanua jambo
Yaani angeanza darasa la kwanza akiwa na miaka saba, angesoma shule ya msingi kwa miaka saba, sekondari miaka minne, kidato cha tano na sita miaka miwili na chuo miaka mitatu, jumla angekuwa na umri wa miaka 23 kwa sasa ambayo ni pungufu ya miaka 25 iliyotajwa kwenye wasifu wake mtandaoni huko nchini Marekani.
SITTI AMEFIKAJE HAPA?
Data zinaonesha kwamba, baada ya kumaliza kidato cha sita, Sitti alihamia jijini Dalas kwenye Jimbo la Texas, Marekani ambapo mbali na kusomea elimu ya chuo kikuu nchini humo, amewahi kuigiza filamu inayojulikana kwa jina la Lost In Abroad.
Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top