Habari Kali
Loading...

Picha 4 za ajali iliyotokea Tabata Dar na kuua watu asubuhi ya leo

Moja ya taarifa iliyosambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari asubuhi ya leo march 9 2016, ni pamoja na hili tukio la ajali ya magari matatu ambayo ni gari la abiria aina ya DCM, Lori la mchanga na gari lingine lililokuwa limebeba ng’ombe kugongana katika eneo la Tabata, Dar es salaam.
Hadi sasa hakujawa na taarifa za uhakika kuhusiana na chanzo cha ajali ikiwa ni pamoja na vifo na majeruhi, millardayo.com inaendelea kufuatilia undani wa tukio hili na endelea kukaa karibu ili kila litakalonifikia niweze kukusogezea.
Na hizi ni picha nne za kwanza kutokea katika eneo la tukio…..
IMG-20160309-WA0006
Mashuhuda wakiangalia ajali eneo la Tabata, Dar
IMG-20160309-WA0007
Garia la abiria likiwa limeharibika baada ya ajali
IMG-20160309-WA0008
Hapa ni gari la abiria likiwa limeharibika baada ya ajali kutokea

Picha: Raisi Magufuli Amtembelea Maalim Seif katika Hoteli ya Serena kwa ajili ya kumjuilia hali yake.

Rais Magufuli akisalimiana naKatibu mkuu waCUF Maalim Seif Sharif Hamad   ndani  ya  Serena  Hoteli  alipoenda  kumjulia  hali  leo march 9
Rais Magufuli akisalimiana naKatibu mkuu waCUF Maalim Seif Sharif Hamad   ndani  ya  Serena  Hoteli  alipoenda  kumjulia  hali  leo march 9

Interview na Akothee, Mkenya mwingine aliyefanya kolabo na Diamond Platnumz

Akothee amekua msanii wa kwanza Kenya kufanya kolabo na mwimbaji Mtanzania Diamond Platnumz, ni Mwanamke mwenye historia ndefu ya maisha ya kuanzia kuwa Dereva Taxi Mombasa Kenya kabla hajaolewa na Mzungu na kwenda Ulaya kisha baadae akarudi Kenya baada ya ndoa kuvunjika.
Anasema ‘Mimi huwa napenda raha sana, kuna wakati Diamond alikuja Mombasa mwaka 2013 ambapo nilikua miongoni mwa watu waliokwenda kuchukua watu wake Airport nikajiuliza kwanini siku moja nisifanye wimbo na huyu kijana wa bongo? kweli nimefanikiwa kurekodi naye hatimaye, siwezi kusema kama Diamond kanitoza pesa kurekodi naye ila ngoma imechukua gharama kubwa’
Tazama hii video hapa chini akijieleza zaidi kisha video ya wimbo wenyewe chini ya hii video.

Unaweza kuyatazama hapa matokeo yote ya kidato cha nne 2015/16

Baraza la mitiani Tanzania NECTA limetangaza Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2015 , ambapo  ufaulu  unaelezwa kushuka  kwa 1.85%  toka  69.75%  mwaka 2014  hadi 67.91%  mwaka  2015.
Matokeo yote unaweza kuyatazama >>HAPA

Sentensi sita za NECTA kuhusu matokeo ya mitihani ya kidato cha nne 2015

February 18 baraza la mitihani Tanzania NECTA wametangaza matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2015 yafuatayo ni maneno matatu waliyosemwa na katibu mtendaji wa baraza la mitihani Tanzania NECTA Dk Charles Msonde.
“Katika mkutano maalum wa baraza wa 110 uliofanyika February 17 2016, baraza la mitihani Tanzania lilipitia taarifa ya matokeo ya kidato cha nne na maarifa uliofanyika tarehe 2 hadi 27 November 2015 na kuidhinisha kutangaza rasmi kwa matokeo hayo katika mitihani ya kidato cha nne 2015”
“Jumla ya watahiniwa 448382 waliandikishwa kufanya mtihani huo, wasichana ni 229144 na wavulana 219238 kati ya hao watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 394o65, wakati watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 54317”
“Watahiniwa wa shule asilimia 96.71 walifanya mitihani na watahiniwa 14749 ambao sawa na asilimia 3.29 hawakufanya mtihani, watahiniwa wa kujitegemea 49333 sawa na asilimia 90.82 lakini watahiniwa 4984 sawa na asilimia 9.18 hawakufanya mtihani”
“Watahiniwa wa mtihani wa maarifa 19547 waliosajiliwa, lakini watahiniwa kati ya wale waliosajili 16162 sawa na asilimia 82.68 walifanya mtihani, lakini watahiniwa 3385 kati ya hao hawakufanya mtihani”
“Kwa jumla ya watahiniwa 272947 sawa na asilimia 67.53 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha nne wamefaulu mtihani, wasichana waliofaulu ni 131913 sawa na asilimia 64.84, wakati wavulana waliofaulu ni 141034 sawa na asilimia 71.09”
“lakini mwaka jana watahiniwa waliofaulu walikuwa  196805 sawa na asilimia 68. 33 hivyo ufaulu ukilinganisha na matokeo ya mwaka jana, ufaulu umeshuka kwa asilimia 0.8 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2014”

Mrembo Jokate kwenye U Heard ya Soudy Brown, comments za instagram kaziona..?

Mrembo Jokate leo ndio aliyesikika kwenye U Heard ya Soudy Brown.
Soudy anasema Jokate alipost video akijiachia kucheza mdundo wa remix ya ‘Zigo’ ya AY Feat. Diamond Platnumz alafu zikafatia comments mbaya.
Jokate amesema alirekodi video hiyo akiwa gym, comment hazikumpa shida, kikubwa yeye ana love ya nguvu na muziki wa AY, mambo mengine ya comments mbaya mitandaoni haimpi shida.


Mambo matatu kutoka kwa Rais wa TFF leo, ruhusa ya Azam FC kwenda Zambia, Yanga kutofanya uchaguzi na msiba wa kiongozi …

January 28 Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Jamal Malinzi alifanya mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya shirikisho hilo na kutangaza msiba wa aliyekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF na Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Simiyu Epaphra Swai.
Malinzi pia ametumia fursa hiyo kuomba radhi vilabu 15 vya Ligi Kuu kufuatia lile sakata linalopingwa na Simba la kuwapa ruhusa Azam FC kucheza mechi za kirafiki na kuahirishiwa baadhi ya michezo yao ya Ligi, kitu ambacho Simba wanahofu ya kuwa kuahirishwa kwa mechi hizo kunaweza kutengeneza mazingira ya kupanga matokeo.
“Kiukweli naomba nivitake radhi vilabu vyote 15 vya Ligi kwa kosa lililofanyika la kuwaruhusu Azam FC kwenda Zambia kucheza mechi za kirafiki, najua maamuzi yamefanyika mimi nikiwa Burundi, lakini kama kiongozi nakiri kosa kufanyika na naviomba radhi vilabu vyote, kuhusu Yanga kutofanya uchaguzi ukweli ni kuwa Yanga hawapo juu ya sheria na wanapaswa kuheshimu katiba yao na ya TFF” >>> Jamal Malinzi
swai
Epaphra Swai

Breaking News: CUF Wagoma Kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar

Azimio La Baraza Kuu La Uongozi La Taifa Kuhusu Tangazo La Mwenyekiti Wa Tume Ya Uchaguzi Ya Zanzibar La Kuitisha Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar

Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28 Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam. 
Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha uchaguzi wa marudio.

Baada ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20 Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:

1. KWAMBA Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umeshafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015, ambapo kwa upande wa uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani ulikwisha kamilika na washindi wote kupewa shahada za kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali. 
Kwa upande wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, matokeo yalikwisha bandikwa nje ya vituo vya majumuisho vya majimbo yote 54. Kilichokuwa kinaendelea baada ya hapo ni kuhakiki matokeo hayo kutoka majimboni na kazi hiyo ilikwishakamilika kwa majimbo 40 na katika hayo, matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa majimbo 31 yalikwishatangazwa kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jecha Salum Jecha, kutangaza isivyo halali kwamba ameufuta uchaguzi huo.

2. KWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.

3. KWAMBA linatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali wa marudio.

4. KWAMBA sababu kuu ya Baraza Kuu kufikia maamuzi haya ni kutokana na matamko yote mawili ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha, kutokuwa halali na kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984. 
Hakuna kifungu chochote cha Katiba ya Zanzibar au Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar kinachotoa uwezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar na hata kwa Tume yenyewe kufuta uchaguzi au kuitisha uchaguzi wa marudio.

5. KWAMBA linazipongeza na limetiwa moyo sana na taasisi na jumuiya zote za kimataifa na kikanda zikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Madola (The Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Marekani na Uingereza kwa msimamo wao wa kuungana na Wazanzibari na kutetea haki yao ya kidemokrasia na maamuzi halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kutaka mchakato wa uchaguzi huo ukamilishwe na matokeo yake kutangazwa.

6. KWAMBA linazipongeza na kutiwa moyo pia na taasisi za hapa nchini zikiwemo taasisi na jumuiya za kidini, taasisi za haki za binadamu, vyombo huru vya habari, vyama vyengine vya siasa na Wazanzibari na Watanzania wote wanaopenda amani na demokrasia kwa msimamo wao wa kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea kusisitiza haja ya kuheshimu na kufuata Katiba na Sheria za nchi yetu na pia haja na umuhimu wa kutunza amani ya nchi yetu kwa kutaka haki itendeke. 
Baraza Kuu linazihakikishia taasisi na jumuiya hizo zote na pia kuwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwamba CUF itaendelea kusimama kidete katika kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi yetu na pia kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.

7. KWAMBA limesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuandika barua na kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kutaka vyama vya siasa vishiriki uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 bila ya kujali kwamba uchaguzi huo ni haramu na unakiuka matakwa ya Katiba ya Zanzibar na Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984.
 Baraza Kuu halikutarajia mtu mwenye hadhi ya Ujaji kufanya kazi ya kutumikia maslahi ya watawala ambao wameamua kuvunja Katiba na Sheria za nchi yetu na kukanyanga misingi ya haki na demokrasia huku akishindwa kukemea uhuni mkubwa uliofanywa wa kubaka demokrasia na haki za watu.

8. KWAMBA limesikitishwa na kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, kukwepa dhamana na wajibu wake kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuiacha njiani kazi aliyoianza ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi Zanzibar.
 Baraza Kuu linamtaka Rais Magufuli kujitathmini na kujiuliza anajiweka vipi na kutoa taswira gani mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa kutokana na kutosimamia ahadi yake aliyoitoa mbele ya Watanzania wakati akilizindua Bunge jipya kwamba atafanya kazi na vyama vya CUF na CCM ili kuupatia ufumbuzi mkwamo huu.

9. KWAMBA linalaani matumizi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na usalama vya Jamhuri ya Muungano na Vikosi vya SMZ dhidi ya wananchi wasio na hatia na ambao wamekuwa watulivu licha ya vitendo vingi vya uchokozi wa makusudi na hata mashambulizi ya hujuma dhidi yao yanayofanywa na makundi ya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi kadhaa kisiwani Unguja.

10. KWAMBA linaitaka jumuiya ya kimataifa na hasa taasisi zinazosimamia haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa kauli na matendo ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na kuchukua hatua dhidi ya watu walio nyuma ya maamuzi na utekelezaji wa matukio hayo.

11. KWAMBA linawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu wa hali ya juu na kuwa watulivu licha ya machungu makubwa waliyoyapitia na wanayoendelea kuyapitia tokea pale maamuzi yao yalipopinduliwa na CCM kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha. 
Baraza Kuu linatoa wito kwa Wazanzibari wote kuungana pamoja chini ya chama chao cha CUF walichokipa ridhaa halali kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015 kutetea maamuzi yao waliyoyafanya kupitia sanduku la kura kwa njia za amani.
Baraza Kuu linawasisitiza tena Wazanzibari kwamba waendelee kutunza amani ya nchi yetu na kutambua kwamba kutunza amani si udhaifu bali ni jambo linaloipa nguvu jumuiya ya kimataifa kufuatilia haki za kidemokrasia za wananchi wa Zanzibar.

12. Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawatahadharisha CCM na watawala wasiowajali na kuwaheshimu wananchi kwamba zama za utawala wa mabavu usioheshimu Katiba na Sheria za nchi hazina nafasi tena katika dunia ya leo. Baraza Kuu lina imani kwamba HAKI ITASHINDA.

LIMETOLEWA NA:
BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
DAR ES SALAAM
28 JANUARI, 2016

Siasa Majibu yamenifikia kutoka ndani ya kikao cha Uchaguzi wa Meya wa Kinondoni Dar..

Vichwa vya habari mfululizo vilisukuma habari Magazetini kuhusu ishu ya kukwama kwa uchaguzi wa Mameya wa Manispaa ya Ilala na Kinondoni Dar es Salaam… uchaguzi huo kwa mara ya kwanza uliahirishwa kutokana na mivutano mbalimbali ikiwemo pingamizi lililowasilishwa Mahakamani.
Mahakama ilitoa mwongozo kwamba Uchaguzi huo uendelee na Mameya wapatikane kazi ianze, ripoti kutoka ndani ya kikao cha Madiwani wa Kinondoni Dar imenifikishia taarifa kwamba Diwani wa Ubungo, Boniface Jacob amechaguliwa kuwa Meya wa Kinondoni na Diwani wa Tandale (CUF) Jumanne Amir Mbunju amechaguliwa kuwa Naibu Meya.

BONIFACE II 

src-milardayo--http://millardayo.com/fnc1601/

Unaweza kuyatazama matokeo yote ya kidato cha pili 2015/16

Tayari Serikali kupitia Baraza la mitiani NECTA imetangaza Matokeo ya kidato cha pili mwaka 2015  324,068 sawa na 89% kati ya wanafunzi 363,666 waliofanya mtihani wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu kwa mwaka 2016.
Matokeo yote unaweza kuyatazama hapa>>http://www.necta.go.tz/matokeo/ftna2015/html/index.htm

Unakumbuka ile mishemishe mapokezi ya Mbwana Samatta baada ya ushindi wa Afrika? (+Video)

Staa wa soka kutoka Mbagala Dar es Salaam, Mbwana Samatta ameteka vichwa vya habari kila kona Tanzania na nje ya mipaka baada ya kutangazwa kuwa mchezaji bora wa soka Afrika kwa mwaka 2015.
Ushindi huo aliupata Nigeria, akatua na Tuzo mkononi usiku wa manane Uwanja wa ndege JNIA Dar es Salaam lakini zile mishemishe kwenye mapokezi yake unaweza kujikumbusha hapa mtu wangu.

Kama ni mpenda soka, zisikupite mechi hizi kali za weekend hii …

Baada ya kusimama kwa Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa zaidi ya siku 10, weekend ya January 16 na 17 inaendelea kama kawaida kwa michezo nane kupigwa, lakini hii sio michezo pekee itakayopigwa weekend ya January 16 na 17. Ligi Kuu Hispania na Uingereza zitaendelea kama kawaida kwa michezo kadhaa kupigwa. Hii ni ratiba mtu wangu ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara, Uingereza na Hispania kwa mechi zitakazopigwa January 16 na 17.
Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania bara zitakazochezwa Jumamosi ya January 16 na 17
sd
Mechi hizi za Ligi Kuu soka Tanzania bara zitachezwa saa 16:00
sd1
Hii ni ratiba ya mechi za Ligi Kuu Uingereza kwa saa za Afrika Mashariki January 16
  • Tottenham Vs Sunderland Saa 15:45
  • Bournemouth Vs Norwich Saa 18:00
  • Chelsea Vs Everton Saa 18:00
  • Man City Vs Crystal Palace Saa 18:00
  • Newcastle Vs West Ham Saa 18:00
  • Southampton Vs West Brom Saa 18:00
  • Aston Villa Vs Leicester Saa 20:30
January 17
  • Liverpool Vs Man Utd Saa 17:05
  • Stoke Vs Arsenal Saa 19:15
sd2
Ratiba ya Ligi Kuu Hispania kwa saa za Afrika Mashariki
  • Sevilla Vs Málaga Saa 18:00
  • Celta de Vigo Vs Levante Saa 20:15
  • Villarreal Vs Real Betis Saa 22:30
  • Real Sociedad Vs Deportivo de La Coruña Saa 00:05
January 17
  • Valencia Vs Rayo Vallecano Saa 14:00
  • Real Madrid Vs Sporting de Gijón Saa 18:00
  • Getafe Vs Espanyol Saa 20:15
  • Las Palmas Vs Atl Madrid Saa 20:15
  • Barcelona Vs Ath Bilbao Saa 22:30
Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top