Habari Kali
Loading...

Magazeti Stori za Magazeti ya Tanzania January 15 zilivyosomwa Redioni CloudsFM (+Audio)


Mzee Edward Lowassa amesema anajiandaa kwa uchaguzi 2020, mafuriko yaikumba Mwanza huku mtoto mmoja akifariki…. Tundu Lissu asema viatu vya nafasi ya Dk. Slaa ni vikubwa CHADEMA, CUF wasema wanaheshimu mazungumzo ndio maana wako kimya kuhusu ishu ya Zanzibar.
Jeshi la Polisi latoa mbinu tano za kuepukana na wizi watu wanapotoka kuchukua fedha Benki, Serikali imesema itawanyang’anya viwanda na mashamba kwa walioshindwa kuviendeleza.
Askari Polisi mmoja na watu wengine watatu wafikishwa Mahakamani Dar kwa tuhuma za wizi wa magari, wananchi wa Manyara wampiga Askari na kumpora bunduki kwenye mnada, elimu ya bure ni kaa la moto Dar, walimu wakosekana na vifaa vyaibiwa.. Serikali yaagiza watuhumiwa wa kesi za kuozeshwa mtoto wa miaka 13 wachukuliwe hatua.
Pingamizi la Serikali kupinga kesi ya David Kafulila latupiliwa mbali Mahakamani Tabora.
Stori zote ziko kwenye uchambuzi wa sauti pia kutoka Powerbreakfast Clouds FM.

Mbunge Joshua Nassari kaamua kuufata mzigo yeye mwenye China…(+Audio)

Kwenye hii kasi ya Rais Magufuli speed haiko kwa Mawaziri tu hapana speed ipo mpaka kwa wabunge …acha ni kusogezee hii ya mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari kwenye ahadi zake za kuendelea kuwa hudumia wananchi wake, wapate huduma nzuri kwenye hospitali ya wilaya ya Meru.
Zile milioni zake 90 zilizokuwa zitumike kununua gari la mbunge zimeanza kufanya kazi mtu wangu, tayari yupo china kaamua kuufata mzigo mwenye kabisa…kutana nae hapa kwenye maneno yake; – Mbunge Joshua Nassari
Bonyeza Play kumsikiliza Joshua Nassari


URA yafanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi, kwa kuichapa Mtibwa Sugar kwa goli hizi (+Pichaz)



Fainali ya 10 ya michuano ya Kombe la Mapinduzi imemalizika visiwani Zanzibar, kwa kuzikutanisha timu za Mtibwa Sugar ya Tanzania dhidi ya klabu ya URA ya Uganda. Mchezo huo uliopigwa katika dimba la Amaan ulichezwa ukiwa na presha ya kawaida kutokana na idadi ya mashabiki kuwa ya kawaida.
DSC_6246
Mchezo ulianza kwa Mtibwa Sugar ya Tanzania, kuanza kwa kucheza mpira mzuri, lakini URA walionekana kucheza kwa nidhamu, kwani dakika ya 16 kipindi cha kwanza Julius Ntambi alipachika goli la kwanza kwa URA lililopelekea Mtibwa kurudi kipindi cha pili wakiwa na presha kubwa ya kutaka kusawazisha goli hilo.
DSC_6237
Kipindi cha pili URA walionekana kuwa makini na kucheza kwa tahadhari, kwani Mtibwa walikuwa hawakauki golini kwa URA kusaka goli la kusawazisha, wakati mashabiki wakiwa na imani kubwa Kombe hilo kubaki Tanzania kwa Mtibwa Sugar kusawazisha, Peter Lwassa akitokea benchi alikuja kupachika goli la pili dakika ya 85 ns 88 akaongeza la tatu lililofanya mashabiki wa Mtibwa waanze kutoka uwanjani.
DSC_6254
Kujiamini kupita kiasi kwa URA kuliwafanya Mtibwa Sugar kupata goli la kufutia machozi dakika ya 90, baada ya Jafari Salum kumpora mpira kipa wa URA Brian Bwete na kupachika goli la kufutia machozi na kufanya mchezo umalizike kwa URA kuibuka na ushindi wa goli 3-1. Hii ni fainali ya pili ya Mtibwa Sugar kupoteza, baada ya mwaka jana kupoteza dhidi ya Simba.
DSC_6148
DSC_6198
DSC_6190

Mbabe wa unga ‘El Chapo’ anavyofanya Mexico hawalali… stori gerezani mambo yako hivi !!

Niligundua uzito wa ishu ya Joaquin “El Chapo” Guzman pale ambapo mpaka Rais wa Mexico, Rais Enrique Pena Nieto  alipost Tweet ya ushujaa wa kumkamata El Chapo !!
EL-CHAPO-III
Sasa leo ni kama siku ya tano hivi tokea El Chapo amekamatwa, kutoka ndani ya gereza la Altiplano Mexico ambako jamaa amefungwa kwa sasa, taarifa iliyonifikia ni kwamba ndani ya siku tano tayari kahamishwa kwenye vyumba nane tofauti ndani ya gereza ili kuhakikisha kama kuna mpango unasukwa kumtorosha basi usifanikiwe.
el chapo iii
Kingine ni kwamba sakafu za gereza zimeimarisha kuhakikisha mchezo wa kwanza kutoboa sakafu alioufanya miezi sita iliyopita haujirudii, vilevile kuna ulinzi zaidi ya kawaida, camera za CCTV zinamfatilia kwa kila sekunde kila anachokifanya.

Hasira za mashabiki wa Cristiano Ronaldo baada ya kushindwa Ballon d’Or…

Usiku wa January 11 Staa wa Barcelona Lionel Messi aliandika historia nyingine baada ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or kwa mara ya tano akiwashinda wapinzani wake Cristiano Ronaldo pamoja na Neymar.
Mashabiki wa Cristiano Ronaldo katika mji wa Madeira alipozaliwa staa huyo hawakufurahishwa na ushindi wa Messi..walichofanya waliamua kwenda kwenye sanamu lake lililopo katikati ya mji na kuanza kulichafua kwa kuandika jina la Messi.
mes
Sanamu la Cristiano Ronaldo likionyeshwa kwa nyuma lilivyochafulia huku likiandikwa jina la Messi
Mashabiki hao walichafua sanamu hilo lililowekwa mwaka 2014 kwa kutumia rangi nyekundu wakiandika jina lake pamoja na namba 10 ambayo imekuwa ikitumiwa na Messi kama ishara ya kuchukizwa na kushindwa kwa staa wao Ronaldo.
tt
Ronaldo na mtoto wake wakiwa mbele ya sanamu hilo baada ya kulizindua mwaka 2014

Jipya la Dr. Shein kuhusu uchaguzi mkuu Zanzibar na mengine…(+Audio)

Leo Jan 12 2016  Zanzibar ilikuwa ikiadhimisha miaka 52 ya mapinduzi,  ambapo Rais Dr. Ali Mohamed Shein alipata time ya kuwahutubia wananchi wake na haya ndio aliyoyalenga zaidi.

Huu ndio mpango ambao Adidas wangependa utokee kwa Pep Guardiola na Lionel Messi

Gazeti maarufu la michezo Hispania la Marca, January 12 limepamba headlines zake za gazeti kwa kumuandika kocha anayetajwa kuwa ghali kwa sasa duniani Pep Guardiola na mshindi wa tuzo tano za Ballon d’Or Lionel Messi. Gazeti hilo limewaandika Messi na Pep Guardiola kuwa Adidas inataka kuwaona wakijiunga na klabu ya Man United msimu ujao.
Adidas ambayo ni kampuni ya kijerumani inayojihusisha na utengenezaji vifaa vya michezo duniani, ndio kampuni inayodhamini klabu ya Man United kwa sasa, Pep Guardiola pamoja na Lionel Messi, hivyo inatajwa kuwaweka pamoja ni kuitangaza biashara yao kwa pamoja, tofauti na sasa Messi akiwa FC Barcelona anavaa viatu vya Adidas lakini jezi analazimika kuvaa ya Nike.
CYMGQflWkAA-eKY
Marca limekuwa ni gazeti mahiri la kufichua stori nyingi za ndani za michezo kutoka Uingereza, mpango wa Adidas unaonekana kuwa mgumu, hususani ukizingatia Pep Guardiola anahusishwa kwa karibu na kujiunga na Man City msimu ujao, lakini Lionel Messi nae hapewi nafasi kubwa kuwa anaweza akaondoka FC Barcelona kwa siku za karibuni.

Michezo Hivi ni vitu vitano ambavyo vingeweza kutokea kama Messi na Ronaldo wangekuwa wanacheza timu moja …

Siku moja baada ya ushindi wa tuzo ya tano ya Ballon d’Or wa mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayaeichezea klabu ya FC Barcelona ya Hispania Lionel Messi, ambaye alikuwa anashindana na Neymar na Cristiano Ronaldo katika tuzo hiyo. January 12 nimekutana hii kutoka sokkaa.com. Mtandao huo umeweka vitu vitano ambavyo vingetokea kama Messi na Ronaldo wangekuwa wanacheza timu moja.
5- Hili ni moja kati ya vitu vinavyotajwa kuwa kama Ronaldo na Messi wangecheza timu moja, basi wachezaji wachanga na chipukizi wangeshindwa kuchagua nani awe Role model wao, Ronaldo na Messi wote wana majina makubwa lakini hii ingeweza kuleta shida kwa wachezaji chipukizi.
Ronaldo-n-JESSE
4- CR7 na LM10 wangecheza timu moja basi mabeki wa timu pinzani wangekuwa wanaoneshwa kadi  nyingi katika mchezo mmoja, kwani kuwakaba wachezaji hao ni kazi ngumu sana. Kwa sasa wanacheza timu tofauti na wanasumbua ngome za ulinzi wa timu pinzani.
Messi-fouled
3- Timu pinzani ingekuwa ni ngumu kuandaa au kujua ni mbinu ipi sahihi kuwa kaba wachezaji hao. Ronaldo ambaye anacheza Real Madrid na Messi wa FC Barcelona, kama wangekuwa timu moja basi makocha wa timu pinzani wangekuwa  na wakati mbadala kutunga mbinu za ulinzi wa wachezaji hao.
zidane-n-Ronaldo
2- Uwepo wao kwa pamoja ndani ya kikosi kimoja kingeweza kuleta moral kwa wachezaji na makocha wa timu zao, uwepo wa safu imara ya ushambuliaji wa Lionel Messi na Ronaldo, inaweza kusaidia wachezaji kupata hali ya kujituma na kucheza vizuri na mastaa hao ambao wote wamewahi kushinda tuzo ya Ballon d’Or.
Messi-new-contract
1- Kama Ronaldo na Messi wangekuwa ndani ya kikosi kimoja, basi klabu ingekuwa inachangamoto kubwa ya ulipaji wa mishahara ya wachezaji hao, kwa sasa Messi analipwa mshahara wa euro milioni 20 na Ronaldo analipwa mshahara wa euro milioni 17 kwa mwaka, sasa pata picha hali ingekuwaje kama wangekuwa klabu moja.

Cheki pichaz za Party ya Samatta na zawadi aliyopewa na Serikali kwa kutwaa tuzo …

IMG_20160112_232125
Zawadi ya Samatta kwa Waziri mkuu ikipokelewa na waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
Headlines za Mbwana Samatta kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani ya Afrika, bado inazidi kuleta furaha kwa wapenzi, mashabiki, watanzania na viongozi wa serikali kwa ujumla. Usiku wa January 12 Mbwana Samatta alifanyiwa party iliyopewa jina la Samatta Party. Party ilifanyika na serikali kutangaza kumpatia zawadi ya kiwanja Kigamboni na siku kadhaa mbele atakabidhiwa hati.
IMG_20160112_232228
Mkuu wa idara ya Vodacom kanda ya Pwani Harrieth Koka akiwa katika picha ya pamoja na Samatta
IMG_20160112_232252
Mshindi wa Big Brother Afrika Idris Sultan akiwa na Samatta
IMG_20160112_231625
IMG_20160112_231648
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba Zacharia Hans Pope kushoto na mwandishi wa habari za michezo Saleh Ally
IMG_20160112_231728
IMG_20160112_231754
Samatta katikati, kushoto waziri wa michezo Nape Nnauye na waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi
IMG_20160112_231815
IMG_20160112_232012
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akithibitisha serikali kumzawadia fedha na kiwanja maeneo ya Kigamboni.
IMG_20160112_231838
IMG_20160112_231857
Samatta akiwa na waziri Nape na Lukuvi pamoja na mama na baba yake.
IMG_20160112_231916
IMG_20160112_231936
Thomas Ulimwengu alikuwepo pia kumsapoti Samatta
CHANZO CHA PICHA: VODACOM

VIDEO: Rais John Pombe Magufuli akiwaapisha Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu, Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli akiwaapisha Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu Ikulu Jijini Dar es Salaam, 01 Januari, 2016.

Wananchi Kupanga Nauli za Mabasi Yaendayo Kasi


MAMLAKA ya Udhibiti,Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), inatarajia kukusanya maoni ya wananchi juu ya viwango vya nauli za mabasi yatakayotoa huduma ya usafiri wa haraka Jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imetolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa SUMATRA kwa vyombo vya habari kwenda kwa wananchi  ambapo ofisi hiyo itawaalika wadau wote wa usafiri hususani wananchi kuchangia maoni kwenye mkutano utakao fanyika januari 5 kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3 na nusu asubuhi.

Mamlaka  pia inapokea maoni ya wananchi kupitia anuani ya ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo ambayo ni S.L.P 3093 au kwa barua pepe ambayo info@sumatra.go.tz ambapo kabla ya kufikia uamuzi wadau wanatakiwa kutoa maoni ya kuridhia viwango vya nauli  kwa mujibu wa sheria ya Sumatra.

Maoni ya maandisi yatapokelewa kwenye ofisi ya Mkuregenzi Mkuu iliyopo Jengo la Mawasiliano House Makutano ya barabara ya Ali Hassani Mwinyi na Nkumo kuanzia Saa 4 asubuhi hadi saa 9 alasiri mwisho wa kupokelewa maoni hayo ni Januari 13 mwaka huu.

Mamlaka hiyo imepokea maombi ya nauli kutoka kampuni ya UDA-RT inayolenga kutoa huduma ya mpito ya usafirishaji jijini Dar es Salaam katika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi wa Dart.

Maombi yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ni Safari kwenye njia za pembeni (feeder route) shilingi 700 ,safari kwenye njia kuu (trunk route) shilingi 1200 na njia zote mbili ni 1400 ambapo wanafunzi watalipa nusu nauli anayotoa mtu mzima.
Mpekuzi blog

Picha: Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Atoa Semina Elekezi Kwa Makatibu Wakuu na Manaibu wao


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na Makatibu Wakuu pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wakati akifungua Semina Elekezi kwa Makatibu hao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top