Habari Kali
Loading...

Binti Mdogo toka Mtwara Ashinda milioni 50 za Shindano la TMT

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Mshiriki kutoka Mtwara, Mwanaafa Mwinzago ameibuka kidedea katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
 
Katika shindano hilo ambalo washiriki 10 walikuwa wakizitolea macho Shilingi milioni 50, Mwanaafa aliweza kuzoa kura nyingi zaidi na hivyo kujiwekea kibindoni mamilioni hayo na kuwatimulia vumbi washiriki wengine.
 
Awali kabla ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotions, Johnson Lukaza alitoa ahadi kwamba kampuni hiyo itajitolea kumsomesha mtoto Mwanaafa ili aweze kufanikiwa kufikia malengo yake.
 
Mwanaafa ndiye mshiriki mdogo kuliko wote katika shindano hilo lililoandaliwa na Proin Promotions ambapo miongoni mwa majaji watatu, wawili walikuwa waigizaji maarufu nchini, Single Mtambalike ‘Ritchie Rich’ na Yvonne Cherie ‘Monalisa’. Jaji Mkuu alikuwa Roy Sarungi.
 
Mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwanaafa aliangua kilio cha furaha kuonesha kutoamini kwamba amefanikiwa kunyakua mamilioni hayo huku akihaha huku na kule kumtafuta mama yake jukwaani.
 
Hata baada ya kuitwa na kukabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 50 na Mwenyekiti wa Proin Promotions, Mwanaafa aliendelea kububujikwa machozi ya furaha kuonesha kabisa kutoamini kinachotokea usiku huo.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top