Akizungumza
jijini jana, Mratibu wa Mradi wa Prepare ambaye pia ni Mwanasaikolojia
wa Kituo cha Afya na Utafiti Muhimbili, Lusajo Kajula alisema kuwa
katika matokeo ya utafiti uliofanyika vijana wengi walionekana kufanya
ngono ya uke, mdomo pamoja na njia ya haja kubwa.
“Asilimia
6.3 ya vijana wanafanya ngono ya njia ya haja kubwa (kinyume na
maumbile) wakati asilimia 93.7 hawajawahi kufanya ngono na utumiaji wa
kondomu ukiwa ni mdogo kwa vijana wadogo waliojiingiza kwenye vitendo
vya ngono,” alisema Lusajo
“Asilimia 68 ya wale walioanza kufanya ngono hawajui kutumia kondomu wakati asilimia 32 hutumia kondomu.”
Lusajo
alifafanua kuwa utafiti huo umebaini kuwa chanzo kikuu cha vijana hao
kujiingiza kwenye vitendo vya ngono wakiwa na umri mdogo ni pamoja na
kupata vishawishi kutoka kwa marafiki na hata barabarani kwa wanaume
ambao hawana maadili. (Vicky Kimaro na Prisca Musa)
“Lishe
duni ni kishawishi kikubwa, wazazi wajitaidi kuwapa watoto wao mlo
mzuri na kuhakikisha wanashiba ikiwezekana wawafungashie vyakula vya
kula shule kuepuka kupata ushawishi kwa wauza chipsi kwa kuwa imeonekana
wauza chipsi wanaongoza kuwarubuni vijana.
Alisema
utafiti huo umeshirikisha vyuo vikuu vya Makerere, Cape Town, Limpopo,
Afrika Kusini, Bergen, Oslo, Norway, Maastricht, Uholanzi, Sussex na
Uingereza umebaini kuwa wazazi wa kitanzania wanawalea watoto wao katika
mazingira ya ukali huku wakiweka mafumbo katika elimu ya afya na uzazi.
“Nchi
nyingi za Afrika zinatumia ukali katika malezi, Tanzania inaongoza kitu
ambacho kinasababisha watoto wawaogope wazazi wao hata kuwauliza
maswali yanayohusu mabadiliko ya maumbile yao, mfano mzazi anamwambia
mwanae usitembee na mwanaume, ukijaribu tu utapata ukimwi na utakufa,
sasa pale unamjengea mtoto maswali, unatakiwa umueleze wazi kujamiiana
na nini, na athari zake kwa uwazi.
Lusajo
alisema kuwa mradi huo ulitekelezwa kwenye shule 38 kutoka Manispaa ya
Kinondoni zilizochaguliwa ka kutumia sampuli mtawanyiko zilizopangwa
katika makundi mawili kuendana na ukubwa wa shule ambao ulihusisha jumla
ya wanafunzi 6,000.
Aliongeza
kuwa mradi huo ulipunguza uwezekano wa vijana wadogo wavulana na
wasichana kuanza ngono na uongeza uwezekano wa kutumia kondomu kwa wale
walionza kwa kuwa wasichana waliopata mwingiliano ukilinganisha na wale
ambao hawakupata mwingiliano.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >