BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Watu
wengi wamekuwa wepesi kukimbilia kwa rafiki zao ili kuomba msaada wa
mawazo ya nini wafanye kwenye mapenzi. Imani iliyojengeka kwa watu wengi
katika jamii yetu ni kuwa, ushauri ni kitu muhimu sana kwa kila hatua.
Kwa
mtazamo wa haraka haraka unaweza kuishia kwenye ukomo huo wa fikra na
kuamini juu ya ushauri wa mtu kukufikisha mahali sahihi kwenye mapenzi.
Unapokerwa na mpenzi wako unakimbilia kushauriwa na wakati mwingine hata
unapotaka kuoa au kuachana na umpendaye, unamuomba rafiki yako ushauri.
Je,
umeshawahi kufikiria hasara za kuomba ushauri wa kimapenzi kwa rafiki
yako? Hebu ungana nami wiki hii ili nikumegee kidogo hasara za ushauri.
1. UTARAHISISHA MAMBO
Mara
nyingi washauri huwa si wao wanaokabiliana na mambo, hivyo ni rahisi
kwao kupima vitu kwa juu juu tu na kushauri kirahisi rahisi.
“Vipi
kakupiga namna hii, aaa huyu si mwanaume kwa kweli ni bora ukaachana
naye.” Anasema ni bora kuachana naye kwa sababu haumizwi na kuachana,
unayeachana ni wewe anayekushauri.
“Mkubali
tu bwana unalaza damu, hiyo tabia yake ya uhuni atabadilika, shosti
unataka kuacha bahati ipite?” Kwa mshauri ni rahisi kusema hivyo lakini
kumbuka ukubwa wa tatizo hatimaye utakabiliana nao wewe. Hii ina maana
kwamba, unapofikiria kuhusu ushauri ufikirie pia kuhusu kushauriwa jambo
kirahisi, ukiuvaa mkenge mwenye kuumia utakuwa ni wewe.
2. UTAKUGEUZA
Ulimwenguni
kuna aina zaidi ya 1000 za mapenzi na kila mmoja anatajwa kupenda kwa
staili yake. Mapenzi ni kama chembe hai nyekundu zilizopo kwenye damu ya
mwanadamu ambazo zinaelezwa na wataalamu kuwa hazifanani hata kidogo.
Uzoefu unaonesha kuwa, washauri wengi hushauri kwa uzoefu wao, lakini
je, ni sahihi uzoefu huo uwe msaada kwa mtu mwingine?
Jibu
ni hapana, kinachotokea mara nyingi kwenye ushauri ni mtu kumfanya
mwenzake awe kama yeye alivyo, yaani apuuze, aamue na apende kama staili
yake, jambo ambalo haliwezekani kabisa kwenye mapenzi. Vipi Juma ageuke
ghafla awe kama Hassan kwenye suala la mapenzi? Ushauri ni muhimu
lakini upime kama unalingana na matakwa yako.
3. UTAKUONDOLEA UJASIRI
“Kwa
maelezo hayo mumeo ni malaya sana, naona itakuwa vigumu kumbadilisha,
ni bora ukaanza maisha yako kwa sababu kuna siku hali itakuwa mbaya.”
Huu
ni ushauri ambao unaweza kumuondolea mtu ujasiri wa kukabiliana na
tabia ya mumewe hadi kufikia hatua ya kumsaidia akaachana na tabia zake
mbaya.
Ushauri
huondoa ujasiri wa kukabili tatizo hasa pale anayekushauri
atakapolipeleka suala lako kwenye njia ngumu isiyokuwa na ufumbuzi.
Ikumbukwe kuwa, anayeamini kushindwa ni mshauri lakini wewe kama
mwanamke unaweza kusimama kutetea penzi lako na kuliweka sawa mpaka
jamii ikasema: “Jamani huyu dada kamrekebisha kweli mumewe, hakuwa hivi
alikuwa mlevi lakini sasa kaacha pombe.
4. UTAKUNYIMA FURSA
Kwenye
mapenzi kuna fursa nyingi za mafanikio ambazo unaweza usizipate ukiwa
mtu wa kusikiliza sana ushauri wa watu. Kuna wakati ambao unatakiwa
usimame wewe kuamua kumpenda mtu ambaye jamii inaona kama utapotea.
5. UTAKUPOTOSHA
Ni
wazi kwamba kipimo cha uelewa kinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi
mwingine. Ifahamike kuwa, uhodari wa mambo nao hutofautiana, mtu anaweza
kuwa mahiri katika siasa na akaaminika kwenye jamii, lakini ukimpelekea
suala la mapenzi anakuwa hajui kitu, hivyo ni rahisi kukupotosha.
Uchunguzi
unaonesha kuwa, wapenzi wengi hupotoshwa na rafiki zao wasiokuwa na
uelewa wa kutosha juu ya tatizo au suala husika la kimapenzi. Ni vyema
kuwa makini unaposhauriwa.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Saturday, 19 April 2014