Kufanya
kazi sehemu moja au kuzungumza na mwanamke mwenye mvuto kunaweza
kumfanya mwanaume apoteze umakini wake, hii ni kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa na Jarida la New Study.
Wanaume
wanaofanya kazi kwenye makampuni yenye ‘visura’ wengi, ufanisi wao ni
wa kiwango cha chini kulinganisha na wasiokuwa kwenye mazingira hayo,
sehemu ya utafiti inaeleza.
Sababu
ya kuwepo kwa hali hiyo ni uchunguzi kubaini kuwa, akili za wanaume
wenye kuvutwa na sura wakati wakifanya mambo hukabiliwa na mgongano wa
hisia mbili, za kazi na mapenzi.
Kuwepo
kwa vitu hivyo viwili kwa wakati mmoja ndani ya akili ya mwanaume,
utafiti wa kitaalamu uliochapishwa na Jarida la Journal of Experimental
and Social Psychology, umebaini kuwa mwanaume ana hatari kubwa ya
kufanya vibaya kikazi kwa sababu wakati akifanya kazi yake atakuwa pia
akifanya kaziya kushawishi au kuimarisha hadhi yake mbele ya mwanamke
aliyemvutia.
Ukichunguza,
utabaini kuwa, tabia za wanaume (si wote) hubadilika pindi wanapokuwa
mbele ya wanawake warembo, hii ikiwa na maana kuwa, kama mwanaume ni
mwenye maneno mengi na mpayukaji kwa mfano, hujikuta akilazimika
kushusha sauti yake, kuongea kwa unyeyekevu na busara lengo ni kutaka
kumvutia msichana.
Hali
hiyo inapojitokeza ndiyo inayotajwa kudhorotesha umakini wa mtu na
kumfanya afanye kazi zake kama ‘msanii’ anayeigiza na hivyo kuathiri
utendakazi wake.
Wakati
nafanya uchunguzi wangu kwa kuoanisha na ule wa watafiti wengine wa
kimatafa ukiwemo wa Dr. Irva Hertz-Picciotto, kutoka Chuo cha Carifonia
Marekani, nilibaini pia viashiria vingine vya ufanisi duni wa kimasomo
kutoka shule za jinsia moja na zile za mchanganyiko, ambapo uchunguzi
unaonyesha kuwa wavulana wanaosoma shule huku wakiwa na uhusiano wa
karibu na wasichana warembo huathirika kisaikolojia.
Hata
hivyo, upo ushahidi mwingine kwamba kiwango cha kufaulu cha shule
mchanganyiko kuwa chini kuliko wa shule za wasichana au wavulana peke
yao, katika kulithibitisha hili mazingira ya shule na malezi
yanazingatiwa.
Katika
kumbukumbu iliyowashangaza wanasaikolojia na watafiti wa chuo cha
Radboud cha Netherland ni pale mmoja wao aliposhindwa kukumbuka na
kumwelekeza msichana mwenye mvuto aliyekutanishwa naye ramani ya eneo
analoishi, jambo ambalo wenzake walisema lilitokea kwa sababu alikuwa
kwenye mhemko wa hisia za kimapenzi.
Utafiti
wao huo ulihusisha pia watu wengine na matokeo yalionyesha udhaifu
mwingi kwa wanaume, huku wanawake wakiwa na kiwango kidogo cha
kuathirika kwa kukutanishwa na wavulana wenye mvuto.
Ingawa
si jambo la hatari sana kufikia hatua ya kulitangaza moja kwa moja kuwa
ushirikishwaji wa wanaume na wanawake warembo katika ofisi, masomo na
kazi mbali mbali una madhara lakini kitaalamu imebainika kuwa ni vema
kundi linaloathirika ambalo ni sawa na asilimia 19 ya wanaume wote
likapewa elimu ili kupunguza zaidi madhara ya kisaikolojia.
Changamoto
hii, inamtaka kila mwanaume kupima mwenyewe mhemko wa nguvu za warembo
kwa kujiuliza maswali ambayo yatamuwezesha kujua kama yuko kwenye kundi
la wanaume wanaoweza kuathirika kisaikolojia kwa kufanya kazi na
wanawake wenye mvuto au la! Lengo likiwa ni kuchukua hatua za kujikinga
na madhara ya kisaikolojia.
Mwanasaikolojia
Dr George Fieldman anakumbusha kitu muhimu alichokipa jina la
‘Reproductively Focused’ kuwa ndiyo sumu kali inayowadhuru wanaume wengi
wanapokutana au kukutanishwa na wanawake wenye mvuto. Inaelezwa kuwa
wanaume wanaovamiwa haraka na hisia za kimapenzi ndiyo wanaoweza kupata
madhara ninayoyaeleza kwa kiwango kikubwa.
Itaendelea wiki ijayo.
Itaendelea wiki ijayo.
Zipo
njia nyingi za kitaalamu za kupima ili kubaini kuwa mwanaume
anakabiliwa na tatizo hili au la! Lakini pamoja nazo ni hii ya kujibu
maswali, ambayo imeonekana kuwa ni rahisi zaidi kwani haihitaji mtaalamu
wa kumuongoza mhusika bali ni kwa mtu mwenyewe kutafakari na kupata
majibu kama urembo wa mwanamke unaweza kumuathiri kiutendaji. Maswali ya
kujiuliza ni haya:
>>Je una uwezo wa kuongea na mwanamke bila kushika shika vitu? Kwa mfano kuingiza mikono mfukoni, kuchezea simu, kalamu au hata kujipapasa mwenyewe.
>>Je Unaweza kutazamana naye usoni kwa zaidi ya sekunde 36 bila kuona aibu? Unaweza kutembea hatua nne mbele ya mwanamke bila kuhisi mwili wako ni mzito?
>>Je unajiamini unapokuwa na mazungumzo na mwanamke hasa mkiwa wawili tu, au mpaka uwe na mtu mwingine?
>>Je umewahi kuwa na ukaribu na wanawake warembo wangapi na kati yao ni wangapi uliwatongoza?
>>Je una uwezo wa kuongea na mwanamke bila kushika shika vitu? Kwa mfano kuingiza mikono mfukoni, kuchezea simu, kalamu au hata kujipapasa mwenyewe.
>>Je Unaweza kutazamana naye usoni kwa zaidi ya sekunde 36 bila kuona aibu? Unaweza kutembea hatua nne mbele ya mwanamke bila kuhisi mwili wako ni mzito?
>>Je unajiamini unapokuwa na mazungumzo na mwanamke hasa mkiwa wawili tu, au mpaka uwe na mtu mwingine?
>>Je umewahi kuwa na ukaribu na wanawake warembo wangapi na kati yao ni wangapi uliwatongoza?
Baada
ya kujiuza maswali hayo sahihisha kulingana na majibu yako. Endapo
utakosa yote fahamu kuwa wewe ni miongoni mwa watu wanaoweza kupata
athari ukipewa nafasi ya kufanya kazi na wanawake warembo. Kumbuka kuwa
jibu la mwisho lazima idadi yake isizidi nusu, endapo umewahi kuwa na
urafiki wa karibu na wanawake warembo 10 kwa mfano na kati ya hao watano
au zaidi uliwatongoza, utambue kuwa unaviashiria vibaya vya kupata
madhara tunayoyazungumza.
madhara tunayoyazungumza.
Ifahamike
pia kwamba watu wanaotafunwa na ‘virusi’ hivyo vinavyoletwa na mvuto wa
wanawake warembo ndiyo hao ambao hutumia vyeo au nafasi zao vibaya kwa
kuajiri au kutoa nafasi za
upendeleo kazini kwa wanawake wasiokuwa na sifa za kufanya kazi husika na hivyo kujikuta ofisi, wizara na hata biashara zinakosa tija.
upendeleo kazini kwa wanawake wasiokuwa na sifa za kufanya kazi husika na hivyo kujikuta ofisi, wizara na hata biashara zinakosa tija.
Wakati
nafanya uchunguzi kuhusu tatizo la kushirikiana kikazi na wanawake
warembo ambapo niliwahoji baadhi wanafunzi, wafanyakazi na
wafanyabiashara maswali niliyoandika hapo juu, wengi walibainika kuwa na
tatizo hili, hata hivyo changamoto iliyokuwepo ni juu ya swali lao la
msingi kwamba wafanye nini wasiathiriliwe kisaikolojia baada ya kuwepo
kwa dalili za tatizo?
Jibu la swali hili ni dogo nalo ni kujitambua na kuwa makini.
Jibu la swali hili ni dogo nalo ni kujitambua na kuwa makini.
Inashauriwa
kuwa watu wenye matatizo haya wanatakiwa kudhibiti mawazo yao ya
kimapenzi mara wakutanapo na wanawake warembo na kusimamia vitu halisi.
Jambo la mwisho ni kujiamini na kutenda yale wanayofahamu.
Katika
hali ya kawaida tatizo la mvuto wa wanawake hugusa zaidi hisia, hivyo
mara nyingine ni vigumu kwa mtu kuweza kuzuia msukumo usitokee, lakini
kwa aliyejitambua itakuwa rahisi kwake kutoendeleza mawazo ya kimapenzi
sambamba na kazi.
Wakati
mwingine ni suala la mtu mwenyewe kuamua kusimamia kazi na kupuuza hisia
za kimapenzi zilizotokana na mvuto wa mwanamke mrembo, kwa vile si
lazima kila mawazo au hisia zinazotokea ziendelezwe.
Hebu
tujiulize ni mara ngapi huwa tunawaza au kuhisi vibaya na tukaacha
kufanya kama tulivyofikiri kabla? Je hakuna vipindi ambavyo huwa
tunawaza kuua, kuacha wake zetu na hata kufanya mapenzi na ndugu na
mambo mabaya kama hayo na tukayapuuza mawazo hayo? Ikiwa tumeshafanya
hivyo tufahamu kuwa nguvu kubwa iko kwenye uamuzi wetu.
Nikimalizia
somo hili ni kwamba, mara nyingi wanaume wenye aibu na hofu mbele ya
wanawake ni wale wanaodhani kuwa wanakasoro fulani ambazo zinaweza
kuwakosesha penzi na hivyo kuamua kujikarabati kwa unyenyekevu, sauti za
chini, hongo, kutembea kwa madaha na wakati mwingine kujifanya ni watu
wa tofauti sana kwenye jamii, jambo ambalo huweza kuathiri mwenendo wao
na kuwa watu wa kuigiza igiza mambo yasiyoendana na uwezo wao halisi au
kile wanachokifahamu.
Nimalizie mada hii kwa kufafanua kuwa lengo la makala haya si kuzuia ushirika kati ya wanaume na wanawake warembo bali kufundisha watu kuhusu madhara yake ili ukiwapo urafiki uwe ni ule wenye tija, usioathiri ufanisi wa kazi.
Nimalizie mada hii kwa kufafanua kuwa lengo la makala haya si kuzuia ushirika kati ya wanaume na wanawake warembo bali kufundisha watu kuhusu madhara yake ili ukiwapo urafiki uwe ni ule wenye tija, usioathiri ufanisi wa kazi.
KUMBUKA;
ingawa somo hili linawahusu zaidi wanaume lakini kwa upande mwingine
linawagusa wanawake ambao hufanya kazi na wanaume watanashati na wenye
mvuto!
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >