Vijana
wawili wameuawa kwa kushambuliwa na wananchi wenye hasira mkoani Geita
kwa kile kilichotajwa kuwa vijana hao walimuua mama yao wa kambo kwa
kumcharanga mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Akizungumzia
tukio hilo kaimu Afisa mtendaji wa kata ya Busanda alisema tukio hilo
lilitokea juzi katika kijiji cha Nyamtundu majira ya saa tatu usiku
ambapo Mama moja aliyejulikana kwa jina la Mwanamaila Mwanatenga (50)
aliuawa kwa kukatwa katwa mapanga na watu wasiojulikana wakati akitoka
chooni kujisaidia mara baada ya kumaliza kula.
Alisema
mara baada ya kufanya mauaji hayo walitokomea kusikojulikana na
wananchi kwa kushirikiana na jeshi la Sungusungu walianza msako wa
kuwatafuta na hatimaye waliwakamata wakijaribu kutoroka.

Watuhumiwa hao walikamatwa katika kijiji jirani cha Msasa wakiwa na damu kwenye makoti waliyokuwa wamevaa ndipo wananchi hao wakiwa na jeshi la sungusungu waliwauliza kuwa wanatoka wapi.
Watuhumiwa hao walijibu kuwa wanatoka kwenye sherehe ya harusi kwao na baada ya wanafamilia kubaini kuwa mama yao wa kambo ameuawa walianza kuwapiga hadi kuwaua na kisha wakawababua kwa moto.
Afisa huyo aliwataja waliokufa kuwa ni Makoye Nzari(25) na Masumbuko Nzari(36) wote wakiwa ni watoto wa kambo wa mama huyo.
Diwani wa kata hiyo Aliphonce Matonange amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kamanda wa jeshi la polis mkoani Geita Joseph Konyo alisema hakuna aliyekamatwa juu ya tukio hilo na kwamba uchunguzi unaendelea wa kuwabaini waliofanya tukio hilo na huku akiwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >