
Adele ndiye staa wa muziki anayefunga mwaka wa 2015 kwenye headlines za burudani Marekani na dunia nzima akiwa ameuza zaidi ya nakala milion 5 za single yake mpya ‘Hello’ huku video yake ikiwa imegusa watazamaji milion 700 kwenye mtandao wa YouTUBE! Ujio mpya wa Adele kwenye kurasa za burudani umepokelewa kwa muamko mkubwa sana duniani.

Nimekutana na interview ya Adele na jarida la TIME Magazine la Marekani na ndani yake staa huyo amegusia vitu vingi ikiwemo album yake mpya 25, social media pamoja na mauzo ya juu nchini Marekani.

Hivi ni baadhi ya vitu alivyovigusia Adele na interview yake na TIME Magazine:
Mauzo ya nakala zaidi ya mamilioni Marekani: “Inashangaza kidogo na kunishitua sana. Ukizingatia mimi hata sio Mmarekani. Labda wanafikiri nina undugu na Malkia…“

Mtazamo wake kuhusu kuitwa ‘Brand’: “Kila
mtu analitumia neno hilo. Sipendi kuitwa ‘brand’ wananifanya nionekane
kama aina fulani ya bidhaa au kama packet la kripsi… msanii ni package
ya vitu vingi!“

Kwanini watu huupokea vizuri muziki wake: “Uhalisia
nilionao ni kwamba sioni aibu kuimba ukweli unaonigusa hata kama mimi
ndio mwenye makosa. Kila mtu hufanya makosa. Watu wengi hujifanya
wajasiri kwasababu wanaogopa kuonyesha udhaifu wao. Mimi najaribu kuimba
nyimbo zinazogusa vitu vya ukweli kwa mashabiki wangu kwa sababu kama
mimi hata wao wanaumizwa na vitu mbalimali maishani japo natumaini pia
nyimbo zangu zitaleta furaha kwenye maisha ya mashabiki wangu na sio
huzuni na machungu“.

Mitandao ya kijamii ina nafasi gani kwake: “Napenda
kuweka mambo yangu private… kuwa na privacy inakuwezesha kuandika
nyimbo za ukweli utakaogusa watu, waupende au wasiupende bado utakuwa
ukweli. Maisha yangu yamebadilika sana toka niachie ‘Hello’ na hiyo
inanipa changamoto, hivyo siwezi kukaa kusubiria likes milioni na kwa
picha moja… nitapata wapi muda wa kutunga nyimbo zitakazogusa watu? Huo
sio uhalisia“.

Maisha yake binafsi ya nyumbani yapoje: “Nina
maisha ya kawaida, nahisi watu wengi wangekuwa wanajua jinsi ambavyo
maisha yangu ni ya kawaida wangeshangaa. Kama sina kazi zozote huwa
nashinda tu nyumbani na familia yangu… ni muhimu kutokupagawa na hivi
vitu, ni muhimu pia kukumbuka kuishi kama watu wengine wote wa kawaida“.

Kuhusu kufanya Collabo na wasanii wengine?: “Album
yangu 25 haina collabo yoyote lakini hiyo haimanishi hakutakuwa na
collabo kwenye album yangu ijayo baada ya hii… zile tetesi za mimi
kukataa kushirikiana na Beyonce hazikuwa za ukweli, sikuweza kufanya
collabo na mtu kwenye album hii kwa sababu nilikuwa nashindwa kugawa
muda na kufanya maamuzi ya kufanya kazi na nani...”
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >