Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Pwani linaendesha oparesheni kali ya aina yake ya kuwasaka majambazi waliowavamia, kuwaua askari wawili na kumjeruhi mmoja na kisha kupora bunduki aina ya SMG.
Tukio hilo limetokea tarehe 30/03/2015 majira ya saa mbili usiku huko
barabara ya Kilwa Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Katika tukio hilo majambazI wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na silaha zingine waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Katika tukio hilo majambazI wapatao 8 hadi 10 wakiwa na mapanga na silaha zingine waliwavamia ghafla askari watatu waliokuwa kazini katika eneo la kizuizi cha Polisi kilichopo kijiji cha Kipara mpakani Kata ya Vikindu Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.
Majambazi hao waliwashambulia
ghafla askari hao kisha kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30
ndani ya magazine na kutokomea kusikojulikana.
Majina ya askari wa Wilaya ya Kipolisi ya Mbagala waliouawa ni kama ifuatavyo:
- D.2865 SGT FRANCIS,
- E.177 CPL MICHAEL,
Askari mwenye namba D5573 D/SGT ALLY amejeruhiwa kwa risasi kwenye
paja la mguu wa kushoto na amelazwa katika hospitali ya Temeke kwa
matibabu.
Askari huyu kabla ya kujeruhiwa alipambana vikali na majambazi hayo kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo aina ya SMG ambayo walishindwa kumpora hivyo wakatokomea kuelekea pori la Vikindu.
Askari huyu kabla ya kujeruhiwa alipambana vikali na majambazi hayo kwa kutumia bunduki aliyokuwa nayo aina ya SMG ambayo walishindwa kumpora hivyo wakatokomea kuelekea pori la Vikindu.
Katika oparesheni hiyo, nguvu na mbinu zote za kipolisi zitatumika
ambapo vikosi vya Dar es Salaam na Pwani vilianza kufanya oparesheni
hiyo mara baada ya tukio ili kuhakikisha kwamba majambazi hao
wanapatikana haraka iwezekanavyo.
Pamoja na oparesheni hiyo kali inayoendelea, Jeshi la Polisi
linachunguza ili kubaini kama tukio hili linaashiria vitendo vya ugaidi
au ni ujambazi wa kutumia silaha.
Natoa wito kwa wananchi wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam kupitia
(dhana ya polisi jamii) kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa hali na mali
kwa kutoa taarifa sahihi.
IMETOLEWA NA:
S.H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >




