Habari Kali
Loading...

Askofu Wa Kanisa Katoliki Amjibu Migiro......Asema Viongozi Wa Dini Wana Haki ya Kuwaambia Waumini Wao Kupigia Kura Ya HAPANA Katiba Inayopendekezwa

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge mkoani Kagera, Seveline Niwemugizi amesema, viongozi wa dini wana haki ya kuwaelimisha waumini wao waweze kujua kinachoendelea wanapoona kuna mambo hayaendi sawa katika jamii.
 
Niwemugizi alisema pia wanayo haki ya kuwaambia waumini wao kuipigia kura ya Hapana, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu ni wajibu wao kufanya hivyo.
 
Akizungumza na gazeti  la  Mtazania, askofu Niwemugizi, alisema wao kama viongozi wa jamii hawawezi kuona waumini wao wanapotea halafu wanakaa kimya. Kufanya hivyo kutasababisha waingie kwenye uovu, alisema.
 
Askofu Niwemugizi ametoa kauli hiyo siku moja baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha-Rose Migiro kuwataka maaskofu wasiwafundishe wananchi jinsi ya kupiga kura bali wawaache watumie haki yao ya katiba kupiga kura kulingana na utashi wao wenyewe.
 
“Sisi ni viongozi wa dini hatuwezi kuwaona kondoo wa Bwana wanapotea halafu tukakaa kimya au kuwaacha, tutakuwa hatujatenda haki, lazima tuwaambie waweze kuondoka kwenye kundi hilo na waweze kujitambua,”alisema askofu huyo ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC).
 
Alisema hata viongozi wa serikali wanawaambia wananchi waipigie kura ya NDIYO, Katiba Inayopendekezwa kwa sababu inalinda masilahi yao na kuhoji haki hiyo ya kuwaelekeza hivyo wananchi wameipata wapi?
 
“Nimeshangaa kusikia kuwa Waziri anasema viongozi wa dini hatuna haki ya kuwaambia waumini kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa, mbona Serikali imewaambia wananchi waipigie kura ya ndiyo, haki hiyo wameitoa wapi,” alihoji.
 
Juzi, Waziri Migiro aliunga mkono kauli ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, ambaye aliwataka viongozi wenzake wa dini kuacha kuwafundisha waumini kupiga kura ya hapana, bali waumini hao wanapaswa kufanya uamuzi wao kwa utashi wao wenyewe

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top