Wafanyabiashara watatu na wanachuo watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida wakikabiliwa na mashitaka ya kumdhalilisha kupindukia askari polisi wa kike na kumsababishia maumivu makali mwilini.
Mwanasheria
wa Serikali, Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Joyce Minde, kwamba
kwa pamoja, washitakiwa hao walimfanyia unyama askari huyo kwa kumvua
nguo zote na kumwacha mtupu kisha kumshambulia na kumsababishia maumivu
makali mwilini.
Waliopandishwa
kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Joyce Minde, ni Jasmin Iddi (40),
Abdallah Hamduni (26), Ramadhani Bakari (32) wote wafanyabiashara wa
mjini hapa pamoja na dereva, Saidi Saidi (50) .
Wengine
ni Aurelia Adolf Mushi (20), Grace Daniel Paul (21), Happiness Kiluvya
(23), Jackline John (20) na Constansia Masaki (21) wanaodaiwa ni
wanachuo katika moja ya vyuo vya elimu ya juu mjini Singida.
Mwanasheria
wa serikali, alidai wakati wote wa kitendo hicho cha udhalilishaji,
polisi huyo, alikuwa akichukuliwa picha za video huku akiwa mtupu na
kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Tukio
hilo inadaiwa lilifanyika Februari 14, mwaka huu saa 11.30 jioni ambako
kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka, inadaiwa polisi huyo wa kike
alikutwa akiwa na mume wa mshitakiwa, Jasmin wakiwa kando ya Ziwa
Singidani wakivinjari siku hiyo ya Wapendanao.
Hata
hivyo, mume ambaye jina halikupatikana, inadaiwa alitoroka. Mutta
alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa kitendo walichofanya washitakiwa ni
kinyume na Kanuni ya Adhabu 138 A kifungu cha 16 cha Mwenendo wa Makosa
ya Jinai kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002. Wote walikana
mashitaka.
Mpekuzi blog
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >



