Leo
nimekukumbuka kupitia safu hii, nataka kuzungumza na wewe, na hasa
katika suala zima la ‘ku-maintain’ ustaa wako.Ninaposema ustaa wako,
namaanisha heshima, kipaji (kazi) pamoja na mapato yako.
Juzi
kupitia gazeti la Ijumaa Wikienda tumeona jinsi gani umepiga hatua
kimaisha. Umetoka katika maisha ya kuonekana wa kawaida, sasa unapewa
heshima ambayo sidhani kama uliwahi kuitegemea kama unaweza kuipata.
Ulikuwa
mtu wa karibu na aliyekuwa shosti wako, Wema Sepetu ‘Madam’ ambaye
wakati huo alikuwa ana mkwanja mrefu kuliko wewe, jinsi fedha ilivyo
mwana haramu kwa wakati huo ilikuwa ikiwezekana kabisa Wema akakutuma
kitu, ukatii.
Jeuri
ya fedha aliyoionesha Wema wakati wa matatizo yako alipokutolea
shilingi milioni 13, inaonesha ni jinsi gani mwenzako alikuwa vizuri
kifedha. Akakuokoa kwenye kifungo na wewe ukarudi uraiani.Unakumbuka
vizuri hata baada ya yeye kukutolea fedha hizo nini kiliendelea katika
maisha yenu, starehe mwanzo mwisho.
Mlikuwa
mkiongozana na timu ya watu katika kumbi mbalimbali za starehe
mkionesha jeuri ya fedha. Najua unakumbuka Wema alivyofanya mbwembwe na
fedha nyingi kumleta msanii wa Nigeria, Omotola Jalade Ekeinde kuja
kuzindua filamu yake ya Super Star ambayo haijaingia sokoni hadi leo.
Kwa
jeuri hiyo na nyingine nyingi alizokuwa akizifanya Madam, hakuna ambaye
aliwaza kwamba siku moja ufujaji wa fedha unaweza kubadilika na kuwa
fedha za mawazo.Hakuna aliyewaza kwamba wewe ambaye ulikuwa chini yake
ungeweza kuja kuwa juu yake.
Hakuna
linaloshindikana chini ya jua na sasa kibao kimegeuka, sasa fedha
imekutembelea.Heshima ile ambayo alikuwa akiipata aliyekuwa shosti wako,
unaipata wewe.Hapo ndipo unapotakiwa kupatazama kwa makini.
Kama
umefanikiwa kufungua kampuni yako ya kuzalisha filamu, iwekee misingi
thabiti isije kuyeyuka kama ilivyoyeyuka ya huyo aliyekuwa shosti wako
(Wema).Tengeneza mazingira ya kuzalisha kazi na kuziuza kweli Watanzania
waone kwamba kuna filamu bora zinazalishwa kutoka katika kampuni yako.
Kuwa
na fedha nyingi na kutokokuwa na mipango mipya ya kuzizalisha, ni
rahisi kupotea na kurudi kule ulikotoka.Njia aliyopitia aliyekuwa shosti
wako iwe funzo kwako. Chagua njia sahihi ili uendelee kuwa makini
katika maisha yako.
Asikwambie
mtu, starehe za kupindukia huku ukiamini ‘bado zipo benki’ ndiyo chanzo
cha wengi kuporomoka.Natumai sijachelewa kuzungumza na wewe maneno haya
machache, yafanyie kazi ili usije kujifunika shuka wakati kumekucha.
Mungu akubariki!
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >