NYANI mmoja katika Jimbo la Himachal Pradesh, Kaskazini ya India, amewagawia watu pesa taslimu kutoka mtini.
Taarifa
zinasema kuwa watu waliokuwa wanajivinjari katika mji wa Shimla jimboni
humo, walianza kukimbia huku na kule wakiokota pesa zilizokuwa
zinarushwa na nyani huyo kutoka juu ya mti kwa karibu saa moja.
Walioshuhudia
tukio hilo walisema kuwa nyani huyo kwa jina Simian aliiba fedha kiasi
cha rupee 10,000 kutoka nyumba ya jirani katika eneo hilo.
Nyani huyo aliingia katika nyumba hiyo kutafuta chakula lakini alipokosa chakula akaamua kutoweka na pesa.
Jimbo la Himachal Pradesh limekuwa makao kwa wanyama wengi ambapo kuna takribani nyani 300,000
Nyani aina ya Macaque, huonekana kama wanyama wa kuabudiwa na hivyo hulishwa na wananchi.
Lakini
katika miaka ya hivi karibuni wanyama hao, wamekuwa wakizozana na
wakazi kwa sababu ya kuharibu mimea , kushambulia watu na hata kuwauma
watoto.
Maofisa tayari wametangaza wanyama hao kuwa kero kubwa kwa wakazi wa jimbo hilo.
Nyani
huyo mwanzo alionekana akiwa ameketi juu ya paa la nyumba akiwa na
bunda la noti kabla ya kuanza kuwagawia watu pesa hizo kwa kuwarushia.
Watu
walipoanza kukusanya pesa hizo, nyani huyo alikimbilia kwenye mti
mwingine. Lakini watu waliokuwa wanaokota pesa hizo walimfuata kwani
pesa haziachiki.
"Nyani
alionekana kushutushwa na idadi ya watu waliokuwa wanamfuata lakini
alipokimbilia kwenye mti mwingine, watu waliendelea kumfuata,'' alisema
mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo.
HABARI: BBC
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >