Kuanzia
siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye kiwanda cha burudani Tanzania
imehusu fujo zilizotokea Ujerumani kwenye show aliyokwenda kufanya
Diamond Platnumz huko Stuttgart.
Kilichotokea
ni kwamba saa kumi alfajiri ndio promota alimpeleka Diamond kwenye
ukumbi kunakofanyika show. Kwa nini ilitokea akamchelewesha? nini
kilitokea baadae? hizi hapa chini ni kauli za Diamond mwenyewe kwenye
exclusive na millardayo.com
1. ‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo lilikua ni hela, balance
iliyokua imebaki ni balance ndogo kama EURO 3500 hivi ambazo ni zaidi
ya milioni 7 za Tanzania, ninavyojua Mapromoter wengi wa nje wakifanya
show huwa wanauza na vinywaji wenyewe na wanapata hela nyingi
sana kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so nahisi labda walivuta muda
ili waendelee kuuza vinywaji zaidi’
2.
‘Walichelewa kunipeleka kwenye show, walinifata kwenye mida ya saa tisa
usiku na wakawa hawana hela yangu iliyobaki, nikawaambia siendi kokote
mpaka wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500 wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio tukaenda kwenye show’
3.
‘Tukafika kwenye show saa10 kasoro, kweli hata ningekua mimi shabiki
ningekasirika ningefanya vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja na
wametoka kwenye miji na nchi jirani, niliwaambia
wanipeleke nikafanye show ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi sana
nje lakini Mapromota walikua waogawaoga kunipeleka ndani’
4.
‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje, nikamwambia promota atupeleke ndani
tungefika kwenye stage ingetulia baada ya sisi kuimba manake ni vitu
tunakutana navyo kwenye muziki lakini promota walikua waogawaoga, askari
wa Ujerumani karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti ukawa mkubwa’
5. ‘So dakika ya mwisho tukaona hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini, kiukweli
nimesikitishwa sana manake nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara
yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart, imenisikitisha manake watu
walikua kuniona alafu mwisho ikashindikana kuwafikishia
walichokitarajia’
6.
‘Nafikiri October tutakua na show nyingine na itafanyika kulekule,
nilikua nazungumza na uongozi wangu kwamba wanataka show nyingine na
tayari wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’
Unaweza kumsikiliza Diamond mwenyewe kwa kubonyeza play hapa chini.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >