Tufahamu
kwamba si kila mwanaume unayekutana naye na ukampenda anafaa kuwa
mumeo. Wengine wana mapungufu makubwa ambayo bila kuyabaini na ukaingia
kichwakichwa, utakutana na matatizo makubwa.
Kwa
maana hiyo basi, sifa hizi sita ambazo nitazizungumzia leo endapo
utaziona kwa huyo ambaye macho yako yameganda kwake, fanya maamuzi
sahihi ya kumkubalia.
Anakupenda kwa maana ya kukupenda
Unapoingia
kwenye maisha ya ndoa, unatarajia kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa
mwenza wako. Wapo wanaume ambao wanaonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya
kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga.
Wanachotaka
wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na demu flani bomba au kuonja
tu penzi kisha kuanza visa ili muachane.Kwa nini ni vizuri kumpata
mwanaume mwenye mapenzi ya dhati? Hii inatokana na ukweli kwamba kinyume
na hivyo, maisha yatakuwa ya migogoro kila siku. Atakufanyia mambo ya
kukuumiza kwa kukusaliti bila kujali maumivu utakayopata. Hii yote ni
kwa sababu hana mapenzi ya kweli na wewe.
Ndiyo
maana unashauriwa kwamba, kabla hata ya kumuonjesha penzi kisha kufanya
maamuzi ya kumruhusu aende kwa wazazi wako ili mfunge pingu za maisha,
ni vyema ukawa na uthibitisho kwamba anakupenda kwa moyo mmoja.
Hili la tabia ndo’ kila kitu
Linapokuja
suala la ndoa, tabia inakuwa kitu cha awali sana kuangaliwa. Hii ni kwa
sababu, wapo wanaume ‘handsome’, wenye kazi nzuri na kipato kizuri
lakini wanakosa sifa ya kuitwa mume kutokana na tabia zao chafu.
Hakuna
mwanamke anayeweza kudiriki kumpa nafasi mwanaume kuwa mume wake wakati
ana tabia chafu. Endapo utaangalia uzuri wa sura kisha ukafanya maamuzi
ya kuolewa naye, utakuwa umejichimbia kaburi.
Awe anaota mafanikio
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanawake. Wengi hawapendi kabisa kuolewa na mwanaume ambaye hana kazi.
Mwanaume
anatakiwa kuwa dereva katika safari ya kusaka mafanikio, sasa kama
atakuwa ni mtu wa kukaa kijiweni, kupiga mizinga, mvivu asiyependa
kujishughulisha kwa namna yoyote, huyu hafai kupewa nafasi ya kuitwa
mume.
Ile
dhana ya kukubali kuolewa na mwanaume yoyote ili mradi upate heshima ya
kwamba umeolewa, imepitwa na wakati. Mwanaume sahihi ni yule mwenye
malengo maishani, anayefikiria nini cha kufanya kwa ajili ya maendeleo
yake, mkewe na watoto wao.
Wa shida na raha
Wapo
wanaume ambao siyo wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua maisha siku
zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.
Kwa
mfano, unaweza kuingia kwenye maisha ya ndoa lakini kwa bahati mbaya
ukawa huna kizazi, mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na wewe anatakiwa
kukuvumilia na kuwa upande wako.
Yule ambaye atakuwa anaungana na
dada zake kukushambulia kwa kutozaa, hafai kuwa na wewe kwani yapo mengi
yanayoweza kutokea yanayohitaji kuvumiliana.
Kimsingi
uvumilivu kwa mwanaume utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati
kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanaume mwenye mapenzi ya dhati ni
lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina
yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.
Anayejua thamani ya mke
Wapo
wanaume ambao hawajui thamani ya mke na ukiwachunguza utabaini hawafai
kuwa waume za watu. Mume sahihi ni yule anayejua kwamba mke ni kitu cha
faraja kwenye maisha yake.
Yule anayeamini kwamba, bila mke maisha
yake hayawezi kuwa yamekamilika. Wapo ambao wanaamini hata bila wanawake
wanaweza kuwa na maisha mazuri.
Mwanaume
mwenye dhana hii, ukimpa nafasi kwenye moyo wako na ukaingia naye
kwenye maisha ya ndoa, lazima atakuwa mguu ndani, mguu nje. Hataona
hatari kukupa talaka hata kwa jambo dogo tu ambalo mnaweza kuongea na
mkalimaliza.
Ndiyo
maana nikasema, mwanaume sahihi wa kumpa nafasi ya kuwa mumeo ni yule
anayejua thamani ya mke, anayeweza kuvumilia yote akijua mke ndiye
anayekamilisha maisha yake.
Asiye na tamaa za kijinga
Unaweza
kuwa na mpenzi wa kawaida ukiwa na malengo ya kumfanya awe mumeo katika
siku za baadaye. Huyu ukigundua ana tamaa, huna sababu ya
‘kumpetipeti’.
Wanaume wenye tamaa za kijinga ndiyo ambao
wakishaingia kwenye maisha ya ndoa wanakuwa wepesi kusaliti. Hao
hawastahili kuitwa waume za watu.
Mwisho
kabisa naomba niseme kwamba, licha ya sifa hizo 6, yapo mambo mengine
ambayo ukiyaona kwa mwanaume ambaye ulikuwa unahisi anafaa kuwa mumeo,
ni vyema ukapingana na mawazo.
Mwanaume asiyepitwa na sketi,
asiyependa kumsikiliza mwenza wake, anayependa kufanya maamuzi bila
kutaka kumshirikisha mwenza wake, anayekuwa upande wa ndugu zake
unapokuwa kwenye matatizo, asiyejali familia yake, anayekuona wewe si
lolote, asiyethamini na kuwaheshimu ndugu na marafiki zako, huyo kaa
naye mbali kabisa.