INASIKITISHA! Johanitha
Robert Mulokozi (31) amekuwa kitandani kwa miaka mitatu kutokana na
kuugua ugonjwa wa kupooza mwili mzima.Mama huyo mwenye mtoto mmoja
amekuwa akisumbuka na ugonjwa huo uliomfanya akose raha licha ya kupata
matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Johanitha Robert Mulokozi amekaa kitandani kwa miaka mitatu kutokana na kuugua ugonjwa wa kupooza mwili mzima.
Akizungumza
na waandishi wetu nyumbani kwake Nyan’gandu, Kivule, Ilala jijini Dar
es Salaam, mama wa mgonjwa huyo, Valentina Emmanuel (51) alisema kwa
miaka mitatu anashindwa kupata usingizi kutokana na kumuuguza mwanaye
huyo na kukosa uwezo wa kumsafirisha kwenda India kwa matibabu.
Akisimulia
huku akilengwalengwa machozi Valentina alisema: “ Tatizo la mwanangu la
kupooza mwili mzima lilianzia pale alipodondoka chini baada ya kupata
taarifa za kifo cha baba yake mwaka 2011.
“Sikutegemea kama mwanangu
angekuwa hivi kwani alikuwa akiishi vizuri na alikuwa akiendelea na
maisha yake hasa baada ya kupata mtoto ambaye anamtegemea.
“Baada
ya kupata tatizo hili nilimpeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
alilazwa pale kwa matibabu lakini hali bado ikawa mbaya.
“Ninachoweza kusema mimi ni kwamba sikukata tamaa, niliendelea kufanya
juhudi kuokoa maisha yake licha ya kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili
kwa muda wa miezi sita pasipo kupata nafuu na kuamua kumrudisha
nyumbani.
Johanitha Robert Mulokozi akiwa nyumbani kwao Kivule, Ilala jijini Dar es Salaam.
“Baadaye
nilipata wazo la kumpeleka katika Hospitali ya Regence jijini Dar na
nilipofika pale na kuwaelezea tatizo la mwanangu, walimpima na madaktari
walibaini kuwa tatizo lake linaweza kutibika nchini India, nikaambiwa
nitafute shilingi milioni kumi na tatu. Nilishika kichwa na kuanza
kulia.
“Nililia kwa sababu nilijiuliza, nitapata wapi fedha hizo
niokoe maisha ya mwanangu. Niliamua kumfuata Meya wa Manispaa ya Ilala,
Jerry Silaa na kumuelezea tatizo langu.
“Namshukuru
sana baba yule (Jerry) kwani baada ya kumpa maelezo na kumuonesha barua
ya safari ya India aliingiwa na huruma , akaniandikia hundi ya shilingi
milioni sita (6,000,000/), hivyo nina upungufu wa shilingi milioni saba
ili mwanangu aweze kupelekwa India kwa matibabu,” alisema mama huyo
huku akifuta machozi kwa kanga yake.
Mgonjwa hakuweza kuzungumza na gazeti hili na badala yake wakati wote wa mahojiano na mama yake alikuwa akilia wakati wote.
Yeyote
aliyeguswa na tatizo la mama huyu na angependa kumsaidia mchango
anaweza kuwasiliana naye kwa namba ya simu, 0714599104,