Habari Kali
Loading...

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ATOA SEMINA YA UGONJWA HUO JIJINI DAR

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari wa kitanzania na wadau mbaliombakli wa sekta ya afya. Semina hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana, Hoteli ya Protea Courtyard Seaview.
Profesa Anthony Pais (kushoto), akielezea jambo kuhusu ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela(kulia), akizungumza na wadau mbalimbali katika semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akizungumza katika semina hiyo. Kampuni hiyo ilidhamini semina hiyo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira.
Profesa Pais (katikati), akiwa na wenyeji wake. Kutoka kulia ni Dk.Paul Mareale, James Rugemalira, Dk.Malina Njelekela na Benedicta Rugemalira.
ULAJI wa nyama nyekundu imeelezwa uchangia kwa kiasi kikubwa kupatwa na ugonjwa wa saratani ya matiti ambao umekuwa ni tishio duniani.
Hayo yalibainishwa na Daktari  bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti Profesa Anthony Pais kutoka Bangarole India katika semina ya siku moja kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya iliyofanyika Dar es Salaam juzi.
“Ulaji wa nyama nyekundu na vyakula vyenye mafuta unachangia kwa kiasi kikubwa kupata ugonjwa huo ambao umekuwa tishio duniani” alisema Pais.Profesa Pais alisema mfumo wa maisha wa kula vyakula bila mpangilio na kukosa kufanya mazoezi pia ni moja ya sababu inayoweza kumsabishia mtu kupata ugonjwa huo.
“Ni muhimu kujenga tabia ya kufanya mazoezi walau kwa dakika 20 kila siku itasaidia kupunguza changamoto ya ugonjwa huo.Akizungumzia ugonjwa wa saratani ya matiti alisema hauwapati wanawake pekee bali na wanaume lakini kutokana na kukuwa kwa teknojia mpya wamekuwa wakiutibu bila ya kuliondoa titi lenye matatizo.
Alisema hivi sasa dunia imekuwa ikitumia gharama kubwa kwa matibabu ya  ugonjwa wa saratani huku vikifunguliwa vituo vingi vya kutibu ugonjwa huo.
Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) , Dk.Malina  Njelekela alisema ni muhimu sasa kwa madaktari wa kitanzania kujifunza teknolojia hiyo ya upasuaji wa saratani ya matiti bila ya kuliondoa titi husika.
Mshauri  wa Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira ambaye amemleta Profesa huyo hapa nchini amesema baada ya kuona changamoto ya ugonjwa huo aliona ni vema kumleta mtalaamu huyo ili kuona namna ya kusaidia.




Alisema profesa huyo pamoja na kutoa mafunzo hayo mafupi pia atapata fursa ya kutembelea mikoa kadhaa ya kanda ya kati ili kutoa uzoefu wake kuhusu ugonjwa huo.


Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ilidhamini semina hiyo iliyofanyika Hoteli nya Protea Courtyard kupitia vinywaji vyake vya Windhoek Draught na Windhoek Lager.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top