UTAMU wa posho katika Bunge Maalumu la Katiba, umeathiri siasa za baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo waliojiundia kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Wajumbe
hao waliondoka bungeni kwa mbwembwe wakisusia vikao vya Bunge hilo na
kudai hawarudi ng’o, lakini jana baadhi yao walirejea kinyemela bungeni
na kwenda moja kwa moja Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalumu, kudai posho za
vikao ambavyo hawajashiriki.
Mwenyekiti
wa Bunge hilo, Samuel Sitta juzi mchana alitangaza bungeni kuwa,
amepata taarifa kuwa wajumbe wa Ukawa wamerudi lakini si katika vikao
bali wameonekana kwa Mhasibu kuchukua posho.
“Kuhusu
hilo la Ukawa kurudi, taarifa zilizonifikia hivi punde zinaeleza kuwa
wamerudi, lakini wameenda kwa Mhasibu kuchukua posho,” alisema Sitta na
kusababisha wajumbe waliokuwepo ndani ya Bunge hilo kucheka.
Wanyang’anywa tonge
Baada
ya Sitta kueleza hivyo, alimkaribisha Mjumbe Adam Malima, ambaye pia ni
Naibu Waziri wa Fedha, kutoa taarifa kuhusu hatua hiyo ya Ukawa kurudi
kuchukua posho.
Malima
alisema utaratibu wa fedha zinazolipwa na Serikali ni kwa wajumbe
wanaokuja katika kazi za Bunge hilo na kuongeza kuwa, Serikali haipo
tayari kuwalipa watu ujira ambao hawajaufanyia kazi.
“Tumezungumza
na Katibu wa Bunge na kukubaliana kwamba, wote wasio na mahudhurio
malipo yao yasitishwe kwanza, hawawezi kuchukua fedha wakati hawajafanya
kazi, hili tunaiachia Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu,” alisema
Malima.
Baada
ya Malima kumaliza kutoa taarifa hiyo, Sitta alisisitiza kuwa, wajumbe
hao hawawezi kuchukua fedha kwa kugoma kufanya kazi iliyowapeleka
Dodoma.
Washitukiwa
Akizungumza
na Habari leo jana, Katibu wa Bunge hilo, Yahaya Khamis Hamad, alikiri
kuwa baadhi ya wajumbe wa Ukawa walirudi kuchukua posho lakini
hakuwataja majina.
Alisema
juzi walitangaza wajumbe wajaze fomu kwa ajili ya malipo yao na
inavyoonekana, baadhi ya wajumbe wa Ukawa, kwa kujua wahasibu
hawawafahamu vizuri kama wapo bungeni ama ni miongoni mwa walioondoka,
walichukua fomu na kujaza kuchukua posho.
“Kabla
ya malipo yoyote, utaratibu wetu ni lazima wajumbe wajaze fomu za
malipo, jana (juzi) tulitangaza wajumbe wajaze fomu kwa ajili ya malipo,
Ukawa nao waliingia na kuna fomu walijaza, nimechukua orodha ya
mahudhurio ili kujua waliohudhuria.
Hata ya kujikimu?
“Nimeagiza
asubuhi hii fomu zote niletewe, ambaye hakuwa ndani hata kama si Ukawa
ataeleza alikuwa wapi, kama hakuwa ndani hatutamlipa mpaka Mwenyekiti
(Sitta) aidhinishe kwamba mhusika alikuwa na dharura ya muhimu akiwa
Dodoma ndio atalipwa posho ya kujikimu lakini si ya kikao,” alisema
Katibu huyo.
Alisema
mjumbe yeyote atakayelipwa posho ya kikao ya Sh 70,000 ni aliyehudhuria
kikao na kujaza fomu lakini posho ya kujikimu ya Sh 230,000, italipwa
kwa mjumbe aliyefika Dodoma kwa ajili ya Bunge hata kama alipata dharura
ya kutohudhuria vikao kadhaa.
Kwa
mujibu wa Yahaya, posho zinazolipwa ni za kuanzia Aprili 19 mwaka huu
hadi Aprili 26 na kwamba za kuanzia Aprili 18 kurudi nyuma, zote
zilishalipwa.
Hata
hivyo, alifafanua kuwa posho ya kujikimu pamoja na kwamba hulipwa
mjumbe akiwasili Dodoma, wapo wajumbe ambao hawajalipwa kutokana na
kukosekana ufafanuzi wa dharura zao lakini maelezo ya Sitta ya
uthibitisho yakitolewa, watalipwa.
Kamati ya Uongozi
Akizungumzia
kuhusu uamuzi wa Kamati ya Uongozi ya Bunge Maalumu iliyokuwa ikae
Alhamisi iliyopita kujadili hatma ya posho za wajumbe wa Ukawa, Yahaya
alisema kikao hicho hakikufanyika.
Alifafanua
kwamba sababu ya kutofanyika kikao hicho ni kutokuwa na taarifa kamili
kwa kuwa Sitta aliomba kwenda Zanzibar, kukutana na baadhi ya viongozi
wakiwemo wa Ukawa kutafuta suluhu.
Katibu alisema Kamati ya Uongozi inaweza kukutana muda wowote kuanzia sasa kwa kuwa Sitta amesharejea bungeni.
Sitta
alikwenda Zanzibar Jumatatu wiki hii, ambapo pamoja na kukutana na
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),
Seif Sharif Hamad, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi- CUF,
pia alikutana na Rais wa SMZ, Dk Ali Mohamed Shein na Rais mstaafu wa
Zanzibar, Amani Abeid Karume.
>>Habari leo
>>Habari leo
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >