Upo
katika muundo upi wa mapenzi? Wewe na mpenzi wako mahusiano yenu
yakoje? Niyafuraha na upendo au ni yale yanaokutegemea zaidi ili yawepo?
Ni
ndoto ya kila mmoja kuwa katika mahusiano yaliyotawaliwa na furaha na
amani. Mahusiano yenye kila aina ya amani na uchangamfu.
Ila
kwa bahati mbaya ni wachache sana walifanikiwa katika hilo. Wengi
mahusiano yao ni kizungumkuti. Visa na maudhi kwa kwenda mbele. Amani na
upendo wamebaki kuvisikia kutoka kwa wengine, kwao ni kitendawili. Wewe
upo katika mahusiano ya namna gani?
Unaridhika
na jinsi mapenzi wako alivyo kwako. Japo huenda akawa hakupi fedha
kutokana na sababu kadhaa lakini ni kweli anaonesha kukujali? Anakupigia
simu mara ngapi? Hata kama salio hana je, hata kuku’beep’ tu
inashindikana!
Je, wewe ndiyo kila siku umekuwa mwenye kutaka kuonana naye huku yeye akiwa hana habari? Upo katika mapenzi ya namna hiyo?
Mpenzi
wako anakupa sababu yakufurahi au ndiyo vile kila siku huwa unajutia
uamuzi wa kuwa naye. Kila siku yeye kwako anahitaji fedha ukiacha kumpa
basi humpendi. Je, mpenzi wako ni wa aina hiyo?
Jamani, tunapaswa kuelewa kuwa mapenzi ni raha na faraja sana. Unapokuwa hauko katika mapenzi ya namna hiyo unapaswa kujiuliza
Hapo
huenda ukawa umedondokea katika mikono ya wasanii wa mapenzi. Ambao wao
kwao mapenzi huwa na misimu kama ligi za mpira. Leo anaweza kujifanya
anakupenda sana ila kesho hata ‘sms’ yako hajibu. Na akijibu basi ni kwa
maneno ya mkato mno. Kama siyo ‘thanks, basi itakuwa ‘poa tu’. Ni vyema
ukajiuliza muundo wa mapenzi uliyopo ili kuweza kuchukua hatua
zinazofaa kabla mambo hayajazidi kuharibika zaidi.
Kuwa
na mpenzi ambaye hakupi raha na furaha ni kupoteza muda tu na kujipa
‘stress’ za bure. Ni wewe ambaye kila siku umekuwa ukilia tu. Ni wewe
ambaye kila siku unaomba msamaha kwa makosa ambaye anakufanyia wewe.Hayo
mapenzi kweli?
Kulilia
penzi la mtu asiyeonesha kukujali wala kutambua thamani yako ni
kujiingiza katika utumwa. Utumwa ambao mwisho wake nikukuachia majuto
makuu ya kukaa kwa muda mrefu katika mahusiano na mtu ambaye mwisho wenu
utakuwa ni ule ambao hukuutegeamea. Mwisho wa kutengana haliyakuwa huku
ukiwa amekupotezea muda pengine na thamani yako machone pa wengi.
Yangalie vizuri matendo yake juu yako. Angalia maneno yake. Je, yanakufanya ufurahi? Ni matendo ya wapendanao?
Maisha
yako yanahitaji furaha ili uweze kuishi kwa amani. Na asilimia kubwa ya
furaha inatakiwa kusababishwa na mpenzi wako. Sasa vipi unapokuwa
katika mahusiano na mtu anayekukera na kukufanya ujute? Kweli utakuwa na
furaha? Ni kitendawili. Kama si kuambulia msongo wa mawazo pamoja na
sura kukunjika kwa hasira za kila siku!
Kuwa
katika mahusiano na mtu ambaye hapendi kukuona na furaha ni kujimaliza.
Kwa sababu atafanya utendaji wako wa kazi kushuka,uchangamfu ukupotee
kutokana na karaha zake. Ni ngumu mno kupata hata maendeleo kama huwi
mtu wa furaha na uchangamfu. Na pia ni ngumu sana kuwa mtu wa furaha
kama uko katika mahusiano na mtu wa vituko na visa visivyo kwisha.
Kila
siku unamwambia neno moja. Kila siku wewe ndiye unamtafuta. Chunguza
vizuri mahusiano yako. Kisha jibu swali hili, Upo katika mahusiano ya
namna gani?
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >