Serikali imepoteza jumla
ya Sh48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa
badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.
Hata hivyo, jumla ya
watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi
kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada
ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini
Dar es Salaam.
Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo
11,884 yalikuwa na thamani ya Sh 47.4 bilioni wakati magari gari 2019
zenye thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa
tozo.
Makontena
hayo yalitolewa katika bandari kavu ni MOFED 61, DICD 491, JEFAG 1,
450, AZAM 295, PMM 779, AMI 4384, TRH 4,424 ambazo kodi yake ni zaidi
ya sh.bilioni 47.
Magari 2019 yalitolewa bila kulipa kodi katika kampuni za TALL 309, CHICASA 65, FARION 18, SILVER 97, MASS 171, HESU 1359 na kunyima nchi kodi yenye thamani zaidi ya Tsh.bilioni moja (1).
Waliotiwa
mbaroni na jeshi la polisi baada ya kukamatwa leo ni John Elisante,
Leticia Masaro, Christina Temu, Merina Chawala, Adnan Ally ,Masoud
Seleman na Benadeta Sangawe.
Wanaotafutwa kwa tuhuma za kusababisha upotevu wa kodi za serikali katika bandari ya Dar es Salaam ni Happygod Naftal, Nathan Edward, Aron Lusingu, Amani Kazumari, John Mushi, Valentine Sangawe, Benasweet Kamaina, Zainab Bwijo.
Mpekuzi blog
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >