Shule
nyingi za msingi na sekondari zisizo za Serikali, zimetuma maombi kwa
Kamishna Mkuu wa Elimu nchini kuomba kibali cha kupandisha ada katika
mwaka ujao wa masomo.
Hatua
hiyo ni kuitikia amri ya Serikali ya kuzipiga marufuku shule binafsi,
kupandisha ada kiholela na badala yake shule zote zinatakiwa kuwasilisha
maombi ya kupandisha ada hiyo mpya kwa kamishna huyo ili yajadiliwe.
“Kwa
kweli baada ya tangazo lile shule nyingi zimeleta maombi yao hapa na
kilichobaki ni kwa kamishna wa elimu kuhakikisha anapitia maombi hayo
kwa kuzingatia vigezo mbalimbali vilivyowekwa na Serikali,” alisema Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Sifuni Mchome .
Alisema
lengo la maombi hayo ni kuondoa tabia ya wamiliki wa shule zisizo za
Serikali, kupandisha ovyo ada kwa kadiri wanavyotaka, jambo
lililosababisha shule nyingine kugeuza elimu kuwa biashara badala ya
kutoa huduma.
Lengo
la wizara hiyo ya kutaka maombi hayo na kiwango cha ada wanazotoza kwa
sasa ni kubaini shule, ambazo zinafanya biashara na zile ambazo zinatoa
huduma ya elimu kwa kuisaidia Serikali. Shule ambazo zitabainika kufanya
biashara, zitatakiwa kulipa kodi kutokana na biashara hiyo
wanayoifanya.
Profesa
Mchome aliwataka wazazi kuisaidia Serikali kwa shule ambazo hazitafuata
utaratibu huo, watoe taarifa kwa halmashauri za wilaya, wizarani ili
kuhakikisha zile ambazo zimekaidi agizo hilo, zinachukuliwa hatua.
“Hizi
shule ni nyingi ziko zaidi ya 1,000, naomba wazazi watusaidie kwa shule
ambazo zitakaidi agizo la Serikali watuletee taarifa ili tuweze
kuchukua hatua kwa shule husika,” alisema Profesa Mchome ambaye
alisisitiza kuwa wazazi wafanye vikao na shule husika kuhusu
upandishwaji ambao unatangazwa na shule husika.
Alisema
maombi ya kupandisha ada ambayo yanawasilishwa kwa Kamishna wa Elimu,
yanaweza kukubaliwa au kukataliwa kulingana na hoja mbalimbali ikiwemo
ukubali wa wazazi baada ya kufanya kikao cha uongozi wa shule, huduma
inayotolewa na shule husika.
Nia ya Serikali ni kuhakikisha kuwa upatikanaji wa elimu unaendana na uwezo wa wananchi na viwango vilivyokubaliwa.
Mpekuzi blog
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >