Habari Kali
Loading...

USINZIBE MDOMO: MIGOMO INACHOCHEWA NA MAJIBU MEPESI

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Wananchi wakiwa katika maandamano.
IJUMAA iliyopita ilikuwa ni siku kubwa ingawa haikuwahi kuwekwa katika kalenda hapo kabla. Ilikuwa ni siku ambayo umma kwa upana wake, ulitambua jinsi gani sekta ya usafirishaji ilivyo muhimu. Nina uhakika, mamia ya watu walipata hasara ya mamilioni ya shilingi.
Wananchi wakilala chini kuepuka athari za mabomu ya machozi.
Hii ilitokana na mgomo wa madereva wa mabasi ya mikoani na daladala. Chanzo ni wito wa serikali wa kuwataka madereva hao kurejea shule, katika harakati za kudhibiti ongezeko kubwa la ajali za barabarani zinazoua mamia ya abiria kila mwaka.
Historia, inaonyesha migomo ni silaha ya mwisho inayotumiwa na watu wanaoamini hawatendewi haki na mamlaka zilizo juu yao. Lakini wakati wao wakifanya migomo kwa ajili ya kudai wanachoamini ni stahiki yao, mamia kwa maelfu wanaoathirika, ni wasio na hatia kabisa.
Ingawa kiasili migomo ni haki na inatokea kila mara sehemu mbalimbali duniani, hapa kwetu, imekuwa sehemu ya maisha katika miaka ya karibuni. Sekta nyingi zinagoma kwa madai mbalimbali, lakini mgomo mbaya zaidi kuliko huu wa juzi, ni ule wa madaktari uliosababisha vifo vya ndugu, jamaa na wapendwa wetu wengi.
Ingawa migomo siku zote ni mibaya kwa sababu wanaoathirika siyo walengwa, lakini angalau inatoa ishara kwa wenye mamlaka juu ya kuamka kwa wanaogoma.
Na mamlaka yenye kufikiri chanya, ni lazima izione dalili hizi kama zisizo njema kwake, kwa sababu migomo huambukiza, kutoka sekta hadi sekta, idara hadi idara, jamii hadi jamii na mwisho, mtu hadi mtu. Inapotokea kila kada ya watu kuamini kuwa mgomo ndilo suluhisho pekee la matatizo yaliyo mbele yake, kitu cha ukweli cha kukitaraji, ni anguko kubwa!
Ni wakati wa mamlaka kujifunza, kutoka mgomo mmoja hadi mwingine. Mara nyingi makosa ya mamlaka zetu huwa ni jinsi zinavyotoa majibu mepesi kwa maswali magumu na hili ndilo hasa linalotoa hamasa ya kufanyika kwa migomo.
Kuna watu kule kwenye mamlaka zetu wanadhani wao wana akili kuliko tulio mitaani kiasi kwamba hata wanaposhauriwa vizuri, hawataki kusikiliza na kubakia na kauli dhaifu ya kuwa hii ni amri ya serikali, bila kujua kuwa sisi ndiyo serikali yenyewe na wao ni watumishi wetu tu!

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top