Habari Kali
Loading...

UNATAKA ANAYEKUFAA, WEWE UNAMFAA?

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
NiJumanne nyingine tunakutana tena katika safu yetu ya Maisha na Mapenzi, vitu vinavyochukua sehemu kubwa ya maisha yetu ya kila siku.
Leo ninazungumza nanyi kuhusu kutamani au kuwa na mtu anayekufaa katika uhusiano wa kimapenzi; je, wewe mwenyewe umejitathmini kama utamfaa?Ni ukweli usiopingika kuwa kila mtu maishani mwake anatamani kuwa na mwenza mzuri kitabia na kimuonekano ambaye atamfaa kimapenzi kwa shida na raha, katika kumtimizia haja zake na mengineyo.
Suala la kujichagulia mwenza kabla ya kumpata ni jema kwani hata mzazi anapomsomesha mtoto wake shule ya gharama, lengo lake huwa ni kumuandalia mazingira ya maisha bora siku za usoni. Ingawa mzazi husahau kujiuliza kama anayemuandaa yuko tayari kwa maandalizi hayo?
Ni utamaduni wa siku zote kuwa kila mmoja huchagua mwenza anayemuona anamfaa. Hata hivyo, hapa ningependa kuwazungumzia wanaume ambao asili na tamaduni za kiafrika zinawapa ufalme wa wao kuwa ndiyo wachaguzi wa wanawake wawapendao.
Kuna siku nilikuwa kijiweni na vijana wenzangu, stori kubwa ilikuwa ni kuhusu kuwa na mwenza anayekufaa, wakisema mwanaume anatakiwa kuwa makini kumpata mwanamke anayefaa, vinginevyo atachukua kimeo.
Kwamba, baadhi ya wanawake wana tabia mbaya, kiasi cha kuweza kumfanya mwanaume akajikuta akimwaga machozi kwa kuwatupa ndugu na jamaa zake kwa sababu tu ya mtu aliyemuweka ndani.
Kitu nilichogundua ni kwamba sehemu kubwa ya wanadamu, wengi wetu tunashindwa kujifanyia tathmini ya udhaifu na uwezo tulionao ili tuweze kufanya mabadiliko na maamuzi sahihi katika maisha ya kimapenzi.
Yawezekana mwanamke akawa ni mtu anayefaa lakini mwanaume akawa ndiyo kimeo, tena siyo kimeo tu bali kimeo aliyeshindikana, maana wanafunzi na wahudumu wa baa za mtaani kwao wote wanamfahamu, kama inavyoweza kuwa kwa bi dada, kwamba yawezekana madereva wa bodaboda, bajaj na hata Mangi wa dukani wanajua alama zote zilizomo mwilini mwao.
Kwa hiyo nimalizie mada yetu ya leo kwa kusisitiza kuwa ni muhimu sana kuwa makini wakati tunapofanya uamuzi wa kuwa na mwenza kwa ajili ya maisha yako ya baadaye ya kimapenzi.
Kitu cha msingi cha kukumbuka ni kwamba kuna makosa mengi ambayo binadamu anaweza kuyafanya, lakini kati ya hayo, kosa kubwa na lenye athari kubwa zaidi ni lile la kukosea kuchagua mwenza wa maisha yako!
Huu ni mwisho wa makala haya, tuungane wiki ijayo katika makala mengine.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top