Stori:Haruni Sanchawa na Deogratius Mongella
Wakati sakata lake la kumdhalilisha Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo likiwa bado halijapoa, Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima la jijini Dar, Josephat Gwajima anadaiwa kuokolewa na Sikukuu ya Pasaka baada ya jana kuripoti polisi na kuruhusiwa kuondoka hadi sikukuu zimalizike.
Habari za ndani ya jeshi la polisi zilieleza kuwa jana, majira ya asubuhi ya saa 1:00, Gwajima aliripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar lakini hakuhojiwa baada ya kueleza kuwa bado hali yake kiafya ni tete.
Ilielezwa kwamba mchungaji huyo alifika kituoni hapo akiwa na wasaidizi wake waliokuwa wanamsaidia kutembea ambao waliingia naye ofisini.
“Walikaa kituoni hapa kwa takribani nusu saa ambapo baadaye aliruhusiwa akapumzike hadi sikukuu (Pasaka na Karume Day) zitakapomalizika ndiyo ataripoti tena kituoni,” alisema askari mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini kwa kuwa siyo msemaji.
Katika kumdodosa itakuwa siku gani atakayoripoti, askari huyo alisema itakuwa ni kuanzia Jumatano kwani sikukuu zitaisha Jumanne.
Hata hivyo, wakati sakata hilo likiwa linaendelea, Kardinali Pengo Jumapili iliyopita alinukuliwa akisema amemsamehe Mchungaji Gwajima na kuwataka waumini wake waendelee kumuombea. Msamaha huo aliutoa mbele ya waumini katika Kanisa la St Joseph, Dar es Salaam, siku mbili baada ya Gwajima kuhojiwa na polisi.
Mchungaji Gwajima anadaiwa kutoa kauli za kumkashifu kiongozi huyo kwamba amewasaliti viongozi wenzake wa Kikristo kwa kuwataka waumini wa dini hiyo kuamua wenyewe suala la Katiba Inayopendekezwa kinyume na msimamo wa waraka wa kupinga katiba hiyo uliotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania (CCT).
Baada ya kutolewa kwa waraka huo ulioagiza waumini kuipigia kura ya hapana katiba hiyo, Kardinali Pengo alinukuliwa akisema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuzuia wananchi kuikubali au kuikataa katiba hiyo huku akisisitiza waachiwe uhuru wa kuamua.
Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili ya Matawi wiki iliyopita, Kardinali Pengo, bila ya kumtaja jina alisema: “Natumia nafasi hii kueleza juu ya maneno ambayo yalitolewa na mchungaji fulani, sikumbuki anaitwa nani… nasema nimemsamehe kutoka ndani ya moyo wangu wote, anaweza kuwa na sababu zake ila nimemsamehe kabisa.
“Sina ghadhabu wala chuki ila kinyume chake, naomba tumwombee yeye na watu wote waliokuwa wamehusika pengine nyuma yake ili Mungu aweze kutulinda na kutudumisha katika hali ya amani ya taifa letu.”
Alisema hatua ya polisi kumkamata ni sehemu ya kutekeleza utaratibu wa jeshi hilo tu, lakini yeye kwa nafsi yake ameshamsamehe.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >