Habari Kali
Loading...

NJIA BORA YA KUISHI NA MARAFIKI WA MWENZI WAKO-2

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== > Uhali gani msomaji wangu wa kona hii murua, ni matumaini yangu uko sawa. Kwa wewe ambaye afya yako inaleta mushkeli, nakuombea upone haraka na kurejea kwenye majukumu yako ya kila siku.
Ni siku nyingine nzuri tunapokutana kujadiliana kile tulichokuwa tumeanza kukijadili wiki iliyopita. Mada iliyopo mezani ni njia bora za kuishi na marafiki wa mwenzi wako.
Kwa lugha nyepesi namaanisha kama wewe ni mwanaume, unawezaje kuishi na marafiki wa kike wa mwenzi wako na kama wewe ni mwanamke, unawezaje kuishi na marafiki wa kiume wa mwenzi wako?
Wiki iliyopita, tulijadili kwamba jambo la kwanza ni kujiheshimu na la pili ni kujiwekea mipaka. Leo tunaendelea na njia nyingine za namna ya kuishi vizuri na marafiki wa mwenzi wako.

3. EPUKA KUKUTANA NAO MKIWA PEKE YENU
Mathalani wewe ni mwanamke na kuna rafiki wa kiume wa mwenzi wako anakupigia simu na kukushawishi ukutane naye sehemu fulani, tena mkiwa wawili tu huku akikusisitiza kwamba mwenzi wako hapaswi kujua, hiyo ni dalili kwamba ana nia mbaya na wewe.

Kama kweli unampenda mwenzi wako na haupo tayari kumpoteza, unapaswa kumueleza kuhusu suala hilo na kwa pamoja mjue namna ya kukomesha tabia hiyo.
Endapo ukikubali kuanza kuwa unakutana naye katika mazingira yaliyojaa utata, utakuwa unahatarisha uhusiano wako.
Kwa mfano siku ikatokea ghafla mwenzi wako akakukuta ukiwa na rafiki yake, katika mazingira yaliyojaa utata, tena mwenyewe akiwa hana taarifa yoyote juu ya kukutana kwenu unategemea utakuelewa vipi?

4. KUWA NA MSIMAMO
Kuna usemi ambao siku hizi umezoeleka kwamba kwa mwanamke kutongozwa ni suala ambalo haliepukiki. Wanaume wengi wana hulka ya kupenda kutongoza bila kujali anayemtongoza ni nani.
 Hata kama anajua kabisa huyu ni mke wa rafiki yake, atajaribu kumtongoza na kumchombeza kwa maneno ya kimapenzi.
Endapo mwanamke atakosa msimamo, ni dhahiri atakubali kwa kuamini kwamba anapendwa sana na mwisho itakuwa ni kumsaliti mwenzi wake ambaye ndiye aliyemfanya akafahamiana na huyo anayemtongoza. Huu ni ulimbukeni wa hali ya juu kwa sababu unapotongozwa hulazimishwi kukubali.

Mwanamke mwenye msimamo, anaweza kukabiliana vyema na hila za wanaume, wakiwemo marafiki wa karibu wa mume wake bila kusababisha usaliti wa aina yoyote. Kama kweli unampenda, kuwa na msimamo na usiwe mwepesi wa kukubali kila unapotongozwa.

5. DUMISHA UAMINIFU
Njia kubwa kuliko zote ambayo inaweza kuufanya uhusiano wako na mwenzi wako kuwa salama muda wote, ni kudumisha uaminifu katika mapenzi yenu, bila kujali kama mwenzi wako yuko na wewe au yupo mbali.
Jiwekee nadhiri kwamba utampenda, kumlinda na kumheshimu siku zote na kwamba huwezi kumsaliti hata iweje.
 Ifanyie kazi nadhiri yako na hakika, hakuna kitakachokuyumbisha.
Kwa leo tuishie hapa, kwa mada nyingine tukutane wiki ijayo.
Kwa maoni, ushauri, nicheki kwa namba za hapo juu.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top