Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Ernest Mangu amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa.
Miongoni
mwa makamanda wa mikoa waliofanyiwa mabadiliko ni pamoja na aliyekuwa
kamanda wa Mkoa wa Simiyu, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Charles Mkumbo
anakwenda kuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza na nafasi yake
kuchukuliwa na aliyekuwa afisa mnadhimu mkoa wa Manyara Kamishna
Msaidizi wa Polisi (ACP) Gemini Mushi.
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)
Valentino Mlowola anakwenda kuwa Kaimu Kamishna wa Intelijensia makao
makuu.
Aliyekuwa
kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria
Nzuki amehamishwa makao makuu kuwa mkuu wa polisi jamii na nafasi yake
kuchukuliwa na aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ufundi Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Lucas Mkondya.
Wengine
ni aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi
Mwandamizi wa Polisi (SACP) Godfrey Kamwela amehamishiwa Polisi Makao
Makuu na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Njombe Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fulgence Ngonjani.
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
(SACP) Ulrich Matei amehamishiwa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwa mkuu
wa utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kigoma Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jafary Mohamed.
Aidha,
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ferdinand Mtui aliyekuwa
mkuu wa operesheni maalum polisi makao makuu ameenda kuwa Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kigoma.
Zaidi
ya hao wengine waliyohamishwa ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi
mkoa wa Tanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Frasser
Kashai amehamishiwa Polisi makao makuu na nafasi yake kuchukuliwa na
aliyekuwa mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa Kamishna Msaidizi wa Polisi
(ACP) Zuberi Mwombeji.
Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Kihenya Kihenya amehamishiwa polisi makao makuu na nafasi yake
kuchukuliwa na aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya ya kati Ilala, Dar es
Salaam Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrew Satta.
Kwa
mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi, mabadiliko
hayo ni ya kawaida katika kuhakikisha kwamba usalama wa raia na mali zao
unaendelea kuimarika.
Imetolewa na:
Advera Bulimba-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >