Habari Kali
Loading...

CHADEMA wamtaka Rais kutokusaini Muswada wa sheria ya Uhalifu wa Mtandao

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewataka wadau wa habari na taasisi mbalimbali, zikiwemo za kimataifa kuangalia kwa makini na kujadili baadhi ya vifungu vilivyopo katika muswada wa habari ili kuishawishi serikali kutousaini kwa kuwa unalenga kubana uhuru wa vyombo vya habari nchini.
 
Akizungumza Dar es Salaam jana, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, alisema miswada yote ya hati ya dharura, hasa ya miamala ya kielektroniki na mitandao ya jamii isisainiwe ili iweze kurudiwa bungeni.
 
“Wadau na taasisi mbalimbali za kimataifa wazipime ili waone kama zinafaa, wakati hayo yakiendelea tunamtaka Rais Kikwete asisaini sheria hizi, hasa ile ya makosa ya mitandaoni,” alisema Mnyika.
 
Alisema miswada yote iliyopelekwa kwa hati ya dharura inapaswa irudishwe tena bungeni ili iweze kujadiliwa na wabunge kwa kushirikiana na wadau wa habari.
 
Kwa mujibu wa Mnyika, kwakuwa miswada hiyo haijapelekwa kwa hati ya dhati, hivyo wananchi wanapaswa kuibua mijadala ili kuhoji upungufu wake.
 
Alisema endapo muswada wa habari utapitishwa kutakuwa na utaratibu wa kuwa na Bodi ya Ithibati ambayo inataka kila mwandishi awe na elimu ya shahada, hali itakayosababisha waandishi wengi kupoteza kazi.
 
Akizungumzia muswada wa takwimu, alisema serikali ina mpango wa kutoa madaraka makubwa kwa Ofisi ya Takwimu (NBS) pamoja na kuzuia mikataba ya gesi na mengineyo kupitia sheria hiyo.
 
“Haki ya kupata taarifa imetolewa sehemu moja, hili ni kosa na wana lengo la kutumia sheria hizo mbovu kuwaadhibu wanahabari,” alisema Mnyika.
 
Alisema endapo Rais akisaini muswada wa sheria ya kielektroniki, atakuwa amefanya kosa kwa sababu wakati unapitishwa bungeni akidi ilikuwa haijatimia.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top