Hatimaye Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewatoa hofu Watanzania kuhusu afya yake kwa kueleza kuwa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa uchunguzi wa matatizo yake ya uti wa mgongo.
Kardinali Pengo pia amegusia nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu ujao
kwa kuwataka watanzania kumchagua rais fukara kuliko anayetafuta nafasi
hiyo kwa rushwa.
Alitoa kauli hiyo katika mahafali ya Saba ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Dar es Salaam jana.
Alisema maradhi ya uti wa mgongo ambayo yamekuwa yakimsumbua kila
yaligundulika Agosti mwaka 2013 baada ya kufanyiwa uchunguzi wa afya,
Ujerumani.
“Hospitali ya Ujerumani ndiyo waligundua kuwa nyuzi mbili ndani ya uti
wa mgongo zimechanika zinabana mashipa ya neva, kwa hiyo zikawa
zinanisababishia maumivu ya mgongo.
“Kule Ujerumani walizirudisha katika nafasi yake lakini kwa bahati mbaya
hawakufunga huku wakitegemea kuwa mambo yatakwenda vizuri kwa njia ya
kawaida.
“Lakini kwa sababu ya kurukaruka nikajiona kama nimepona ila baada ya
muda kidogo maumivu yasio ya kawaida yalirudi tena,” alisema kiongozi
huyo wa kiroho.
Alisema maumivu yalipozidi Juni mwaka jana alisafiri kwenda Hospitali ya Manipal, Bangalore, India kwa uchunguzi zaidi.
“Walinihudumia vizuri na kwa sasa naendelea vizuri … kwa wale wanaojali
uhai wangu nilipokwenda mara ya mwisho kwenye uchunguzi waliniambia kila
kitu kimekaa kwenye nafasi yake.
“Madaktari walinielezea kuwa nisishangae maumivu ya mara kwa mara kwa sababu operesheni ilikuwa kubwa.
“Kwa sababu operesheni ya sasa itachukua muda kati ya miaka miwili hadi
mitatu niweze kujisikia mzima kabisa. Kwa sasa naendelea vizuri sina
tatizo zaidi,” alisema.
Kuhusu Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, Kardinali
Pengo alisema ni kitu kibaya kama viongozi wanaowania nafasi ya urais
wanatoa rushwa.
“Uongozi wa Taifa hauwezi kununuliwa kwa gharama yoyote… wanaoelekea
kutoa rushwa baadaye watataka sisi wananchi tulipe zile gharama ambazo
walikuwa wametugawia katika kutoa rushwa, afadhali waache kabisa.
“Ni vizuri tupate rais anayekuwa fukara lakini anayependa nchi yetu na
hatatudai gharama ya kumchangua kama si hivyo gharama inaweza kuwa kubwa
ikatusababishia matatizo,” alisema.
Kardinali Pengo pia alizungumzia matukio ya ugaidi na kuwataka
wanaosambaza ujumbe fupi wa vitisho kuacha mara moja tabia hiyo kwa vile
inawaweka wananchi katika hofu.
“Wanaweza kusababisha taharuki na mikanganyiko na kuleta madhara kwa wengi kwa kitu ambacho hakipo.
“Kama kuna hofu ya usalama sehemu yoyote inabidi tuwaachie wataalamu wa
usalama waweze kuishughulikia kwa namna wajuavyo,” alisema.
Hata hivyo, aliitaka serikali kupitia Idara ya Usalama kuwa ya kwanza
kuwahakikishia wananchi kuwa hakuna matukio hayo amani na utulivu
viendelee kuwapo.
Pia aliwashauri wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Josesph kuwa wasisome kwa ajili ya kuajiriwa na serikali tu.
“Kuna nafasi za wataalamu wa sayasi na sanaa za kujiajiri katika chuo
hiki … Chuo kikuu kizuri ni kile kinachoandaa wanafunzi kujiajiri,”
alisema.
Mkuu wa Chuo hicho, Padre Aru Raji alisema chuo kinazidi kupanuka na
mwaka huu kinatarajia kufungua Chuo Kikuu Sumbawanga na Chuo cha Afya na
Tiba, Boko, Dar es Salaam.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >