Stori: Mwaandishi Wetu/Risasi MchanganyikoMWANAUME mwenye imani ya Kirasta ambaye jina lake halikuweza kunaswa mara moja, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akinyolewa rasta zake bila ridhaa yake kufuatia kudakwa akidaiwa kutaka kuiba kwenye duka moja.
Kwa mujibu wa mashuhuda, rastaman huyo alipofika kwenye duka hilo alijifanya kutaka kununua bidhaa mbalimbali kwa kuulizia bei zake lakini mtu mmoja dukani humo aliyekuwa akimlia ‘rada’ kwa mbali aligundua kuwa jamaa hakuwa mteja bali mkwapuzi.
“Ilikuwa kufumba na kufumbua, jamaa akiwa
katika hatua ya mwisho kukwapua, akaitiwa mwizi na kudakwa hapohapo huku
kipondo kikianza kumshukia mwilini.
“Alitolewa nje ya duka, watu wakajaa wakisema apigwe mawe hadi kufa, wengine apelekwe Kituo cha Polisi Msimbazi, lakini kuna mtu akasema hakuna haja ya adhabu zote hizo, kwa kuwa ana nywele za kirasta dawa ni kumnyoa.
“Huwezi amini, jamaa alijitetea kuwa yeye si mwizi lakini wembe wa
Gillete ulinunuliwa, watu wakaanza kumnyoa nywele kwa kukata yale mabutu
ya kirasta,” alisema shuhuda mmoja.“Alitolewa nje ya duka, watu wakajaa wakisema apigwe mawe hadi kufa, wengine apelekwe Kituo cha Polisi Msimbazi, lakini kuna mtu akasema hakuna haja ya adhabu zote hizo, kwa kuwa ana nywele za kirasta dawa ni kumnyoa.
Mwisho wa tukio hilo, rasta huyo aliachiwa kwa vile iliaminika kuwa, adhabu aliyopewa ilimtosheleza kama si kumtia adabu.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wamiliki wa maduka Kariakoo alisema changamoto kubwa ya biashara maeneo hayo ni wizi wa mara kwa mara.
“Hapa tunaibiwa kila siku. Kuna siku tunawakamata siku nyingine wanafanikiwa bila kukamatwa. Wanatupa hasara sana hawa watu.
“Mfano akikuibia suruali ya shilingi elfu thelathini maana yake amekata faida ya suruali kama tano. Sasa hapo huo umeme wa Tanesco tutalipaje na vibarua tutalipaje?” alihoji mfanyabiashara huyo bila kutaja jina lake.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >





