BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Naendelea kuelezea jinsi wanafunzi wanavyoweza kushinda vishawishi vya kuingia kwenye mapenzi.
Ni
wajibu wa mwanafunzi kugomea zawadi inayokuja kwa mlango wa nyuma, kwa
vile watafiti wanasema watu tisa kati ya kumi wanaosaidia husaidia ili
wajisaidie ni mmoja tu anayesaidia kwa maana ya kusaidia.
(3)
- MAZINGIRA MAGUMU –Mazingira magumu yametajwa sana na baadhi ya
wanafuzi kuwa yanashawishi kufanya mapenzi, lakini ukweli unabaki kuwa
mwanadamu kamili mwenye kujitambua hawezi kuuza utu wake kwa kukwepa
adha. Mwanafunzi hana budi kupambana na shida za kitambo ili atafute
raha ya muda mrefu.
Kujilegeza
kokote kwa lengo la kujiokoa na mateso hakujawahi kuwa na matokeo
mazuri kwa mtu au taifa lolote duniani zaidi ya maangamizi. Mwanafunzi
lazima afahamu kuwa kukubali kuwa mtumwa wa mapenzi ya mtu hakutamuokoa
bali kutamfelisha masomo na kisha kutelekezwa na pengine kuambulia
magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI.
Ili
kuweza kushindana na mazingira magumu ni vema mwanafunzi akafikiria
faida za kusoma na kufaulu na hasara za kufanya mapenzi na hivyo kuweka
akilini sababu za kuvumilia shida hizo kwa muda kwa faida ya muda mrefu
kwenye maisha.
(4) - MABADILIKO YA MWILI-
Ni
jambo linaloshawishi, kwani mwili unapofikia wakati wa kubalehe huleta
usumbufu kwa watoto na kuwafanya wawe na tamaa ya kufanya mapenzi.
Lakini tamaa hizi ni rahisi mno kuzishinda, tofauti na zile zitakazokuja
baada ya mtu kuanza mapenzi. Njia pekee ya kuzishinda ni kuepuka
vishawishi vyote na kuwa na maamuzi sahihi kama tunavyoendelea
kujifunza.
(5) - KULAGHAIWA –
Laghai
kubwa kabisa ambayo inachukua nafasi ya kwanza kwa sasa ni ya ahadi za
uchumba. Wasichana wengi wamejikuta wakiingia katika uhusiano wa
kimapenzi na wanaume waliowachukulia kama wachumba wao. Ukweli ni kwamba
matapeli wengi wa kimapenzi hutumia mwanya huu kuwadanganya wanafunzi
na kuwaharibia masomo yao. Kama wewe ni mwanafunzi, usikubali kabisa mtu
akuite mchumba na akiwa na sababu ya kufanya hivyo mwelekeze kwa wazazi
wako lakini wewe usizungumze naye kwa kuwa umri wako bado mdogo.
(6) MALEZI YASIYO NA MAADILI-
Wazazi
nao wanaweza kuchangia mwanafunzi kujiingiza katika mapenzi, kuna
baadhi yao hudiriki kuwatumia watoto wao kama mitaji kwa kuwauza kwa
wanaume kwa lengo la kujipatia mahitaji yao. Lakini wengine hushawishi
kwa matendo yao, yaani kufanya matendo ya kihuni mbele za watoto na
hivyo kuwafanya waone kama mapenzi si kitu cha hatari kwa vile baba na
mama wanafanya.
Ushauri
kwa mwanafunzi ni kuwa makini na kukataa kila vishawishi hata kama
vinatoka kwa wazazi wao. Inaaminika kwamba kila mwanadamu ana haki ya
kusimamia anachokiamini hasa kinapokuwa cha kweli, la sivyo kuacha
maadili kwa sababu ya mtu mwingine hakuna tofauti na kuuza utu.
Lakini
njia nyingine nzuri kwa mwanafunzi kujitambua kuhusu upotoshaji wa
wazazi kitabia ni kuangalia malezi na mafanikio ya watoto wengine ambao
wanaheshimika katika jamii na kuiga tabia zao ikiwa pamoja na kuwaomba
ushauri walimu na watu wenye busara sehemu anayoishi.
(7)
- KUKOSA MIPAKA- Kuna wanafunzi ambao hawaheshimu mipaka ya uhusiano
kati ya wanaume na wanawake. Utakuta chumba cha wavulana, wasichana
wanaingia kwa uhuru hadi usiku wa manane na wakati mwingine kuwa tayari
kushikanashikana hadi sehemu nyeti za miili yao.Tabia hii haipendezi
kwani inaweza kuleta hisia za kimapezi.
Inashauriwa
kuwa wanafunzi wa jinsia tofauti lazima wawe na mipaka ya uhusiano kwa
kuheshimiana. Haifai wanafunzi wa jinsia mbili tofauti kukumbatiana
hovyo na inapotokea wakawa pamoja basi wazingatie sababu za msingi za
umoja wao na si vinginevyo.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Wednesday, 26 November 2014