Habari Kali
Loading...

MTOTO KUFIA MAHABUSU POLISI MAZITO YAIBUKA

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Denis Mtima na Gabriel Ng’osha
LILE sakata la mtoto wa miezi 6 (pichani) kufia mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Kova, Mbezi Kwamsuguri, Dar linaendelea! Safari hii, mama wa mtoto huyo, Meradi Meshack  ameibua mazito akiwataja polisi jamii kuwa ndiyo chanzo cha kifo cha mwanaye.
Mtoto Thomas wa miezi 6 aliyefia mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Kova, Mbezi Kwamsuguri, Dar enzi za uhai wake.
Awali ilibainika kuwa, mtoto huyo aliyefariki dunia Novemba 18, mwaka huu wakati mama yake akiwa amewekwa kituoni hapo kama mhalifu, polisi wa kituo hicho walitajwa kuhusika.
Akizungumza na waandishi wetu, mama huyo alisema  yeye na mtuhumiwa wake aliyemtaja kwa jina la mama Na walikuwa wakidaiana fedha za upatu ambazo alikuwa akimdanganya kuwa wanachama wenzake bado hawajatoa.
Mama wa mtoto huyo akilia kwa uchungu msibani.
Baada ya usumbufu wa muda mrefu ndipo wakapishana maneno, mwanamke huyo akampeleka polisi akidai alitaka kumpiga. “Nilifuatwa na polisi jamii wawili na si polisi wenyewe. Mimi nilikuwa na mume wangu, niliwaambia mwanangu anaumwa nitakwenda kesho lakini hawakukubali, wakanitukana na kunichukua kwa mabavu huku mwanangu akiwa na hali mbaya na walimuona.
Ndugu na majirani waliofika kumfariji mfiwa(mama wa mtoto), Meradi Meshaki, (kulia).
“Shangazi yangu na mume wangu walinifuata wakitaka kuniwekea dhamana, wale polisi jamii wakakataa, wakanitupa mahabusu. Mwanangu akazidi kuwa na hali mbaya zaidi maana hali ya hewa mle mahabusu ilikuwa ni nzito sana.Baba wa marehemu Thomas, aliyefahamika kwa jina moja la Paschal (aliyekunja mikono).
“Usiku nilipitiwa na usingizi, niliposhituka usiku wa manane nikamuona akikohoa na kupumua kwa shida, baadaye akalegea na kuwa kama amelala, nikawaita wale polisi jamii lakini hawakuja. “Ndipo alfajiri, mmoja wao akaja, akanitazama kisha akaondoka zake. Akaja mwingine, akamshika mwanangu  akawa kama ameshtuka, akaniambia niondoke haraka nimpeleke hospitali.Waombolezaji wakiwa msibani hapo.
“Kumbe wakati anasema hivyo alishajua mwanangu amefariki dunia, inauma sana kwa kweli! Nilitoka na kilio kwani nilishampoteza mtoto wangu na wao sikuwaona tena! Walikimbia! Huu ni ukatili wa hali ya juu,” alisema mwanamke huyo.
Naye mjumbe wa eneo hilo, Rashid Sultan alisema taarifa za kifo cha mtoto huyo alizipata na kuwatupia lawama polisi jamii waliojichukulia uamuzi wa kumweka mahabusu mwanamke huyo tena akiwa na mtoto mchanga wakati kituo hicho ni kidogo na hakilazi wahalifu nyakati za usiku na hutakiwa kufungwa saa 12 jioni.
Inadaiwa kuwa, chanzo cha mtoto huyo kufariki dunia ni kukosa hewa huku akiwa anasumbuliwa na kifua. Hadi Uwazi linakwenda mitamboni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camilius Wambura hakuwa akipatikana kwenye simu yake ya mkononi ili kuelekeza anachokijua.
Marehemu alizikwa Novemba 19, mwaka huu kwenye Makaburi ya Mbezi Kwamsuguri jijini Dar. Mungu ailaze pema peponi roho yake. Amina.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top