CHEREKO chereko!
Siku chache baada ya supastaa ‘grade one’ wa sinema za Bongo, Wema
Sepetu ‘madam’ kummwaga King of Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’,
mama mzazi wa mwigizaji huyo, Mariam Sepetu ameangusha sherehe ya nguvu
kama ishara ya kuonesha ‘amekunwa’ na tukio hilo, Ijumaa Wikienda
linashuka nayo mstari kwa mstari.Kwa mujibu wa chanzo makini, kutokana na mama huyo kutobariki uchumba wa mwanaye na Diamond ambaye pia anajulikana kwa jina la Dangote kwa muda mrefu, habari za uchumba huo kuvunjika zilipochapishwa kwenye Gazeti la Ijumaa ‘Kubwa’ toleo lililopita, moyo wake ulijawa na furaha.
“Mama Wema alichukizwa kwa kiasi kikubwa na
mapenzi ya wawili hao kutokana na kile alichoamini kuwa, Diamond hakuwa
na mapenzi ya dhati kwa mwanaye zaidi ya kutegemea nyota yake impe
mafanikio ndiyo maana akafanya pati hiyo fupi nyumbani kwake Sinza-Mori,
Dar,” kilisema chanzo hicho.
SHEREHE ILIVYOKUWAChanzo hicho kilizidi kumwaga unga kwamba, sherehe hiyo ilikuwa ni ya aina yake kwani mama Wema aliwaita mashosti zake, wakaandaa ‘menu’ ya ukweli kabisa, wakasherehekea lakini bahati mbaya Wema hakuhudhuria.
“Wema hakuweza kuhudhuria sherehe hiyo
kutokana na kubanwa na majukumu mengine. Bi mkubwa aliwaita marafiki
zake, wakafungua shampeni, wakala, wakanywa na kucheza muziki kufurahia
Dangote kupigwa chini,” kilisema chanzo hicho.
MAMA NA CHUKI YA MUDA MREFUChanzo hicho kilizidi kumwaga ubuyu motomoto kuwa, mama Wema alipiga cherekochereko za kutosha siku hiyo kwani alikuwa akimchukia Diamond kwa muda mrefu.
“Mama Wema chuki zake kwa Diamond
hazitaisha kamwe kwa kuwa hampendi tu kutokana na kuona mwanaye hasongi
mbele kimaendeleo kama alivyo Diamond ambaye akiachana na Wema mambo
yake hayamwendei vizuri kama anavyokuwa na mwanaye.”
MAMA WEMA ANENA
Baada ya wanahabari wetu kunasa maelezo hayo ya chanzo, walimvutia waya mama Wema ambaye alikiri kufanya sherehe fupi baada ya mwanaye kummwaga Diamond.
“Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona ndugu yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa mwanangu,” alisema mama Wema.
TUJIKUMBUSHEBaada ya wanahabari wetu kunasa maelezo hayo ya chanzo, walimvutia waya mama Wema ambaye alikiri kufanya sherehe fupi baada ya mwanaye kummwaga Diamond.
“Mimi naona huu ndiyo mwisho wa Wema na Diamond na siku zote nasema hakuna uhusiano ukadumu bila baraka za wazazi, niseme tu, sitaki kumuona ndugu yeyote wa Diamond kwangu, kama mahari wakatoe kwa Penny siyo kwa mwanangu,” alisema mama Wema.
Kumwagana kwa Wema na Diamond safari hii, ni mara ya nne. Awali walimwagana, wakarudiana, wakamwagana tena, Diamond akatua kwa Jokate Mwegelo, wakarudiana tena na Wema, wakaja mwagana tena, Diamond akatambaa na Penniel Mungilwa ‘Penny’, wakamwagana, karudiana na Wema, sasa wamemwagana tena.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >





