BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ndugu
zangu, hivi karibuni binti mmoja mwenye umri wa miaka 20 alijikuta
kwenye wakati mgumu baada ya jamii inayomzunguka kubaini kuwa anatoka
kimapenzi na ‘mbaba’ mwenye umri zaidi ya miaka 65. Wakati
watu wakijiuliza inakuwaje mzee mzima kutoka na kibinti hicho, taarifa
zikazagaa kuwa, si penzi la kawaida tu bali wawili hao wanatarajia
kuoana hivi karibuni. Kweli Ijumaa iliyopita mzee huyo alimchukua
‘mtoto’ jumlajumla na sasa wanaishi kama mke na mume, watu wamebaki
midomo wazi! Lakini
kila linalotokea lina sababu zake na kwa hili nimeona nilizungumzie
leo. Uchunguzi unaonesha kwamba siku hizi vibinti vidogodogo
vimecharukia sana mapenzi ya watu wazima.
Wapo ambao wanafikia hatua
ya kuolewa na vijibabu vikiwemo vya kizungu, ukiuliza unaambiwa bora
maisha huku wengine wakishadadia kuwa, vijana wa siku hizi ni pasua
kichwa tu. Mapenzi yao yametawaliwa na usanii.
Huenda hayo
yanayosemwa yana ukweli na yawezekana ndiyo maana leo hii tunaona kuna
ndoa nyingi zinazofungwa huko mitaani kwetu ambazo anayeoa ni kama vile
anamuoa mwanaye au mjukuu wake. Inashangaza sana!
Lakini kama umekuwa
ukijiuliza kwa nini haya yanatokea, leo nitakupa sababu saba ambazo
zinawafanya wasichana wadogo kuingia kwenye mapenzi na watu wazima na
wengine kuolewa kabisa.
1. Wanajua kupatiliza wanawake
Katika
uchunguzi uliofanyika kwa kuzungumza na baadhi ya wasichana, imeonesha
kuwa wengi wao wanapapatikia watu wazima kwa kuwa wanajua namna ya
kumpatiliza mwanamke. Wanajua kujali, kubembeleza na kuwafanyia wapenzi
wao vitu ambavyo wanavitaka kwa wakati bila longolongo.
Inaelezwa
kuwa, watu wazima wanawachukulia wapenzi wao kama watoto hivyo kuchukua
nafasi ya kuhakikisha wanakuwa ni wenye furaha wakati wote.
2. Wanajua kuhudumia
Inasemekana
kuwa, mtu mzima anapoingia kwenye uhusiano, anakuwa mwenye msimamo
unaoweza kufanya mambo yakaenda kama alivyopanga. Akisema anakupenda
anamaanisha kweli na atakuwa tayari kwa gharama yoyote kuhakikisha
uhusiano au ndoa inadumu.
Linapokuja suala la fedha, watu wazima
wanaonekana si wabahiri. Wanajua kuhudumia ili mradi tu wapewe penzi
lenye ujazo unaostahili. Hapa ndipo panapowagusa wengi.
Katika
wasichana 10 niliowauliza sababu za baadhi yao kupenda watu wazima, 9
walisema ‘wazee’ siyo bahiri na wanajua kuhudumia na kumfanya mwanamke
aishi maisha ya raha mustarehe tofauti na vijana ambao mwanzo wanaweza
kuanza kwa kujifanya wanajua kuhudumia lakini baadaye wanageuka kuwa
‘marioo’.
3. Wanajiamini
Asilimia kubwa ya wanawake ulimwenguni
kote wanapenda kuwa na wapenzi/waume wenye msimamo na wanaojiamini. Hata
hivyo inaonesha kuwa, watu wazima ni wenye msimamo na wanajiamini zaidi
kuliko vijana na ndiyo sababu ya baadhi ya wasichana kuwashobokea. 
4. Wamepevuka
Watu
wazima ni watu waliopevuka kiakili na kimwili hivyo wana uwezo wa
kuwafanya wapenzi wao nao wakapevuka kadiri siku zinavyokwenda. Ndiyo
maana baadhi yao wakishaolewa au kuwa kimapenzi na watu wazima
wanabadilika katika maamuzi. Hicho ni kitu kinachowafanya baadhi yao
kupenda kuwa na watu wazima.
5. Wameshafanya makosa mengi, wamejifunza
Mtu
mzima ni lazima atakuwa amepitia uhusiano na watu wengi. Atakuwa
amepata uzoefu mkubwa kwani atakuwa amefanya makosa mengi na kupitia
hayo atakuwa amejifunza, hawezi kuyarudia.
Kwa maana hiyo mwanaume
mwenye umri umri mkubwa akiingia kwenye uhusiano na kabinti ni vigumu
kukakwaza, kila atakalotaka kulifanya ambalo atahisi atamkosea ni rahisi
kuliacha hivyo kumfanya msichana aliyeingia kwenye uhusiano naye
kutopokea samahani za kila mara kwa mara.
6. Hawaigizi
Ni kweli
wapo watu wazima wale tunaowaita mafataki ambao wanapomtokea binti mdogo
lengo lao si kuoa bali ni kuonja penzi kisha huingia mitini.
Hata
hivyo, uchunguzi unaonesha watu wazima wengi wanajua kupenda na
wanaposema hivyo wanamaanisha kweli, hawaingizi sanaa na ndiyo maana ni
wepesi wa kuhudumia, kubembeleza na kuchukua nafasi ya ‘ubaba’. Hicho
kinawafanya wasichana wengi kukimbilia huko.

7. Hawana wivu wa kijinga
Wapo
ambao wana wivu kweli lakini uchunguzi unaonesha kuwa, watu wazima
wengi hasa wale walio kwenye uhusiano hawana wivu wa kijinga unaoweza
kuwa kero.
Hawana tabia ya kupiga simu kila mara na kuuliza uko wapi,
hawana maswali kama vile; ‘yule uliyekuwa unaongea naye ni nani’, kwa
kifupi watu wazima wakipata kile wanachokitaka hawana ile kumfuatilia
mtu licha ya kwamba wakibaini wanamegewa wanaumia sana na ni wepesi wa
kuchukua maamuzi magumu. Ni
hayo tu kwa leo lakini siku zijazo tutaona madhara ya msichana kuingia
kwenye uhusiano au kuolewa na mwanaume ambaye kiumri anaweza kuwa baba
au babu yake
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out:
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Filed Under:
mapenzi
Wednesday, 26 November 2014