
Jamani hivi wewe mwanamke kichwani kwako kuna ubongo au matope? Kila nikikuangalia sikumalizi kwa mambo ya aibu unayofanya.
Kwenye nyumba kuna siri nzito, wanawake tumekuwa tukijijali wenyewe na kusahau familia zetu.
Hivi kama huwapendi watoto wako, mumeo unamcheza shele, unapata nini shoga?
Mimacho imekutoka najua hujanielewa, nazungumza na wewe mkosa haya usiyejua vibaya. Waume zetu wakiamka asubuhi wanatuachia fedha za matumizi wakijua kabisa familia yake itakula vizuri. Lakini tukipewa mgongo tu tunayofanya ni kichefuchefu.
Jamani upatu umekuwa upatuu!, Huna unachowaza mwanamke zaidi ya utabanaje matumizi ili ibakie ucheze mchezo wa kupeana. Kwa vile akili yako unajiangalia mwenyewe, tamaa imekujaa huangalii madhara ya kuwalisha watoto wako chakula kibovu ili tu upate fedha ya upatu.
Kwa nini usiijali kwanza familia yako, unaachiwa fedha nyingi kwa ajili ya chakula. Mwanamke mkosa haya unawanunulia wanao masalo na fungu la tembele. Ili kumfumba macho mumeo asijue nini kinaendelea. Kwa vile unajua chakula cha jioni lazima ale nyumbani, unamnunulia nyama robo na kuiunga vizuri, wakati wa kula mumeo anaamini kabisa familia yake inakula vizuri.
Kwa vile viumbe wa Mungu hawajui nini kinaendelea, wao hata mboga za kuchemsha bila kitu wanakula, wanachojua ni kushiba hakuna kitu kingine. Mwanaume akiamini anachokula kila siku ndicho wanachokula wanaye, lakini upande wa pili wanaye wanaishi kama yatima, wanachokula Mungu anajua, mboga ni dagaa za kuchemsha au zilizoungwa na kitunguu cha shilingi mia kinachopikiwa zaidi ya mara tatu na nyanya masalo mabovu pengine umeomba kwa muuza genge, mbona aibu!!
Nakuuliza unamkomoa nani? Mwanao mwenyewe humpendi kwa ajili ya kubana fedha ucheze upatu, mbona tunakwenda kubaya kwa tamaa za kijinga.
Familia yako huipendi, nani aipende? Watoto hawashibi kwa kuwapikia chakula kidogo ili tu ubane za upatu. Ukimwona mwanamke kanenepa anapendeza machoni kwa watu. Lakini watoto wake wamekondeana kama wana koshakoo.
Baba ana kazi nzuri kila siku anaacha 10,000, lakini kinaliwa chakula cha elfu mbili mchana, jioni baba ananunuliwa nyama robo ili akirudi nyumbani ajue mambo yanakwenda sawa.
Hivi jamani haya ndiyo maisha tunayotakiwa kuishi? Kuzisahau familia zetu kwa ajili ya kubana fedha ya upatu. fedha unayoipata haina faida yoyote na familia hata mtoto akiumwa fedha ya panado mpaka umsubiri baba yake.
Jamani mbona mnatutia aibu wanawake wenzenu? Watoto kila chakula kibaya ndicho chao. Umekuwa mama ntilie, kuwapikia wanao masalo bora liende?
Ukiangalia watoto wako utafikiri umeachiwa na jirani umtazamie, kumbe wako. Usivyo na haya maisha unayaona ya kawaida hata mshipa wa huruma haukugongi, wala huoni aibu kwa vile wewe mwenyewe umevimbiana na kupendeza na migoldi ya pesa ya upatu.
Hebu tuzipende familia zetu, hukatazwi kucheza upatu lakini iwe fedha ya ziada si ya chakula cha familia.
Tuwapende watoto wetu ili kujenga familia bora. Yangu yameishia hapa japo limekuchoma lakini lichukuwe.
Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >