STAA wa
sinema za Kibongo, Salma Jabu 'Nisha', Jumanne iliyopita alijikuta
akizua taharuki kufuatia kuegesha gari lake nje ya Hekalu la Freemason
lililopo nyuma ya Hyatt Regency Dar es Salaam The Kilimanjaro Hotel
jijini Dar es Salaam.
Taharuki
hiyo ilikuja pale Nisha alipoegesha gari lake eneo hilo na kushuka
kisha wanafunzi na watu wengine kusitisha shughuli na kumzunguka kutaka
kujua kulikoni staa huyo kufika eneo hilo linaloaminika kuwa kila
anayekwenda ni muumini wa imani ya Freemason.
Baadhi
ya watu walimuuliza Nisha alichofuata kwenye hekalu hilo huku mwenyewe
akishindwa kujibu kwani alitupiwa maswali mfululizo.
Chanzo
chetu kilidai kuwa msanii huyo baada ya kuona amezingirwa na watu
alisimama na kuzungumza nao kisha akabadili uamuzi, alirudi ndani ya
gari na kuondoka eneo hilo ambapo baadhi ya watu walidai huenda alitaka
kuingia kwenye hekalu hilo kama mastaa wenzake ambao mara nyingi
huonekana wakiingia na kutoka.
Upande wa mbele wa Hekalu la Freemason lililopo karibu na hoteli ya Hyatt Regency Posta, Dar es Salaam.
Kufuatia
taarifa za chanzo hicho, gazeti hili lilimsaka msanii huyo na
kufanikiwa kumpata kwa njia ya simu ambapo alifafanua kuhusu suala
hilo."Aah! Dah, nyie habari hizo mmezipataje, mbona pale sijaona
mwandishi yeyote? Ukweli pale mimi nilipaki gari tu kwa ajili ya kufanya
mambo yangu maeneo yale lakini ghafla nikashangaa umati umenivaa, kila
mtu anataka kuniona laivu na kuongea na mimi.
“Wanafunzi ndiyo usiseme, sasa kutokanana na kusongwa na umati kama ule nikabadili maamuzi na kuondoka zangu,” alisema Nisha.
Kumekuwa
na dhana miongoni mwa watu kwamba, baadhi ya mastaa wenye mafanikio
Bongo wamejiunga na imani ya Freemason huku ikisemekana wanaishi kwa
kuabudu kwenye hekalu hilo mara moja kwa wiki.
Hata
hivyo, hakuna ushahidi wa moja kwa moja ni staa gani mwanachana wa
Freemason kwani hakuna aliyewahi kukiri kwamba yeye ndiye
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >