NI
mshangao! Sherehe ya kicheni pati ya staa wa filamu Bongo, Lucy Komba
imewashangaza waalikwa wengi baada ya kutawaliwa na vitu vingi vya
kiasili tofauti na matarajio ya wengi.
Sherehe
hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Makumbusho
ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida, wake wa
viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movies
walihudhuria.
Miongoni
mwa matukio ambayo yaliibua mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi
mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye
magurudumu matatu (guta) akiwa na wapambe wake ambao walikuwa peku
miguuni.
Kwenye
guta hilo lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa nyasi juu,
Lucy alikaa ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika nyungo ndogo
kuashiria asili ya Mtanzania.
Kama
hiyo haitoshi, Lucy aliwaacha hoi waalikwa kutokana na vazi lake ambalo
ni tofauti na wanavyovaa wengine katika sherehe kama hiyo kwani
alitinga kipensi kifupi kwa ndani chenye rangi ya bendera ya Tanzania
huku kwa nje kikifunikwa na kitambaa chepesi.
“Ama
kweli hii ni ya aina yake, hebu angalia nguo yake alivyoitengeneza kwa
kweli inavutia sana, full utamaduni,” alisikika mmoja wa watu
walioudhuria sherehe hiyo.
Ulipofika
wakati wa kufungua shampeni, nayo ilikuwa ya aina yake. Aliandaliwa
pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara ambayo
aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni
waalikwa.
Baadhi
ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji kutoka
nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha alipoona
waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na wengi.
Lucy
Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye
Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye
kuangusha nyingine Denmark.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >