Tatizo
la uwezo wa kufanya tendo la ndoa linazidi kukua miongoni wa wanandoa
na wapenzi wengi. Takwimu za kitafiti zinaonyesha kuwa karibu ndoa 4
kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliana na tatizo
hili. Aidha wanaume 6 kati ya 10 wanatajwa kulalamikia upungufu wa nguvu
za kiume na kuacha idadi ya wanawake wanaokabiliwa na tatizohilo kwa
mujibu wa uchunguzi kubaki na asilimia 13.
Pamoja
na matatizo mengine kutajwa kuchangia upungufu wa nguvu za kiume na
kushuka kwa msisimko wa tendo miongoni mwa wanandoa, uchunguzi umeonesha
kuwa utumiaji holela wa vyakula hasa vyenye mafuta ni moja kati ya
sababu zinazochangia kwa kasi tatizo hili.
Kwa
kuzingatia hilo, watafiti wa masuala ya uhusiano wa kimapenzi wamebaini
aina kumi ya vyakula ambavyo vina uwezo wa kumuongezea mtu nguvu ya
kufanya tendo la ndoa. Vyakula hivyo ni hivi vifuatavyo:
PILIPILI
Pilipili
zilizocheshwa zimetajwa kuwa na uwezo wa kusaidia msukumo wa usambazaji
damu mwilini, ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo unaoweza kumfanya mtu akawa
na hisia kali za kimapenzi. Kwa msingi huo, ni vema kwa wale
wanaokabiliwa tatizo la uwezo wa kufanya mapenzi wakatumia pilipili si
kwa wingi bali kwa kiwango stahili, ili waamshe hisia zao.
PARACHICHI
Aina
nyingine ya chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya
tendo la ndoa ni Parachichi. Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha
vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa
watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi
na kwa upande wa wanawake husaidia kuongeza majimaji yenye utelezi
sehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa
kujamiiana.
NDIZI
Wakati
unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya
uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye
muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa
kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika
tendo la ndoa.
CHOKOLETI
Ulaji
wa Chokoleti huongeza uchangamfu mwilini na, hivyo kumuwezesha mtu
anayeshiriki tendo la ndoa kuwa na mguso sahihi kwenye fikra zake, jambo
litakalomuwezesha kupokea hisia za mapenzi kwa urahisi zaidi ya mtu
ambaye anakwenda kwenye uwanja wa sita kwa sita akiwa mchovu wa mawazo.
CHAZA NA PWEZA
Aina
hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi
ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha
msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
POMEGRANATE (komamanga)
Ni
aina fulani ya matunda mekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa
kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili
na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa
kubwa.
MVINYO MWEKUNDU
Mvivyo
mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza
msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya
tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa
na tatizo la kushindwa kurudia tendo.
MBEGU ZA MATUNDA
Mchangayiko
wa mbegu mbalimbali za matunda, mfano tikiti, maboga husaidia kuondoa
ACID mwilini na kumfanya mtu ajione ni mwenye afya njema.
VANILLA
Vanila
husaidia kuamsha hamasa mwili.Mwisho wa aina hizi za vyakula ni TIKITI
MAJI ambalo linatajwa kuwa na virutubisho vingi vyenye uwezo wa
kuusaidia mwili kuwa na nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >