Ni kweli kabisa kuwa penzi kati ya mwanaume na mwanamke hupitia
mabadiliko mbalimbali kwani mtu hukutana na vitu mbalimbali na mawazo
mbalimbali yanayoweza kumpa sababu ya yeye kubadilika. Katika ulimwengu
wa sasa ambapo mtu akifikia umri wa miaka 25 tayari amekwishakuwa na
wapenzi zaidi ya 3 ni vigumu kabisa mtu kushindwa kuanza kulinganisha
utamu wa penzi alilopata huko nyuma kabla yako na lile unalompa
sasa.Katika ulinganishaji huo lazima kuna vitu Fulani utakavyopungukiwa
kama vile sura, rangi ya ngozi yako,urefu au ufupi kwa mwili wako,
ukubwa wa uume au uke wako,uwezo wako wa kifedha,uongeaji wako,hasira
zako ,utamu wako katika tendo la ndoa na vitu vinginevyo. Iwapo unaamini
kuwa hilo ni jambo la kweli basi lazima uamini pia kuwa penzi lako
litapimwa kwa kadri siku zinavyoenda.
Ndugu mpendwa napenda nikuambie kuwa pamoja na ukweli kuwa mpenzi wako
ulienae sasa au yule utakayempata tayari ameshakuwa na wapenzi
wasiopungua watatu basi inakupasa uamini kuwa sio atakuwa analinganisha
utamu wa penzi lako na wapenzi waliotangulia bali pia atakuwa anaangalia
kama wewe pia una dalili za kuweza kumuumiza kama alivyoumizwa na
wapenzi waliotangulia.Hivyo ni muhimu sana katika mwenendo wako
ujitahidi usisababishe maumivu katika moyo wa mpenzi wako.Jambo lolote
lile linaloleta huzuni au kumkosesha raha mwenzio linaweza kuonekana
kama tishio.
Katokana na hali halisi ya uanadamu tumeumbwa na tabia ya kujilinda na
maumivu au kukwepa watu ambao ambao wanaweza kutuumiza ni muhimu uepuke
mambo ambayo yanwaweza kuonekana kama tishio kwa mpenzi wako.Kutokan na
umuhimu wa mtu kujilinda bila wewe kujua mwenzio atakuwa makini
kuangalia maneno ,mwenendo na matendo yako kuangalia kama una mbegu
yenye uwezo wa kuzaa maumivu yatakayoumiza moyo wake.
Kama vile utamu wa vyakula na matunda vilivyo na utofauti kadhalika ili
uweze kumfurahisha na kutunza penzi lako ni muhimu uwe na uwezo wa
kuleta utamu katika maeneo mbalimbali ya uhusiano wenu.Kwa maneno
mengine ni muhimu utumie akili yako kujua maeneo yanayoleta utamu mwingi
zaidi kwa mpenzi wako na kufanya kazi hiyo na bila kuacha maeneo
mengine yaletayo utamu wa kiasi kidogo.
Ili uweze kufanikiwa katika hilo kwanza lazima utambue kuwa kila mmoja
wetu anapendelea vitu tofauti tofauti kama vile kuna wengine hawawezi
kula chakula bila pilipili kadhalika kuna watu wengine ambao hawawezi
kuendeleza uhusiano unaokuwa na mapungufu fulani. Kwa mfano huo wa
pilipili ningependa kusisitiza kuwa inakupasa uwe makini sana katika
vitu ambavyo wewe unapendelea lakini mwenzio hapendelei kwani hapo
ukishindwa kutimiza haja za mwenzio unaweka uhusiano wako
hatarini.Pamoja na kusema hayo pia ni muhimu ukumbuke kuwa upo uwezekano
wa kutokea mabadiliko katika vitu ambavyo unapendelea au mwenzio
anapendelea.Usipokuwa makini utashindwa kwenda sambamba na madiliko
yanayotoke na baadae ukaanza kuona penzi linapungua siku hadi siku na
unapomuuliza mpenzi wako utashangaa kuona anakuwa mkali.Kwanini anakuwa
mkali? Anakuwa mkali kwani anauona uzembe wako katika kufuatilia
mabadiliko ya utamu wa penzi lenu na kwa kuwa hukuwa makini anaona kama
vile ulikuwa humjali kwa makusudi kabisa kumbe sivyo.Jambo hili
nimeliona katika mahusiano yangu mimi mwenyewe.KWkuwa nimekuwa muwazi
sana wapenzi wangu wengi wamekuwa hawajazoea hali hiyo na kushidwa
kunifurahisha katika maeneo kadha na badala ya wapenzi hao kuona ni
nafasi ya wao kujifunza mambo mapya wakaniona kuwa ni wa ajabu na mkali
jambo ambalo sio la kweli.
Nakumbuka kuwa na uhusiano na dada mmoja mwenye umri wa miaka 24 na
dada huyo aliniambia wazi kuwa hajawahi kuachwa na mwanaume yeyote yule
kati ya wanaume sita walionitangulia(wakati naazisha ushusiano nae
alikuwa hajvunja na kuzika uhusiano aliokuwa na handsome Fulani).Siku
moja dada huyo baada ya kufanya kosa fulani na kuadhibiwa aliniuliza
anifanyie nini ili nijue ananipenda na mimi nikamwambia ninachohitaji
sana ili nijione ananipenda ni heshima.KWA wengi hilo linaonekana jambo
rahisi sana lakini ukiliangalia undani wake ni refu na pan asana.Kwa
kweli dada huyo alijitahidi sana kuonyesha mapenzi kwangu kwani
alidiriki kutoroka kwao na kumhonga mlinzi ili aje kuwa name hadi
alfajiri na kwa hilo tu nilimpenda sana.Pamoja na juhidi zake nyingi
sana alishindwa kuwa mkweli na muwazi jambo ambalo lilipelekea mimi
kuamua kumuacha kwani tayari huko nyuma nilikuwa nimeumizwa vibaya sana
na mtu wa aina hiyo.La kushangaza dada huyo alikataa kwa kusema hataki
kuachwa na mara kadhaa alikuja nyumbani kwangu na nilipokuwa sipokei
simu zake wakati ananisubiri nyumbani alianza kulia hadi majirani
wakaingilia kati.NI kweli unaweza kumpenda sana mpenzi wako lakini
usipokuwa makini unaweza kuharibu uhusiano huo wewe mwenyewe.
Umuhimu wa kujali tofauti za utamu unaongezeka zaidi kutokana na mambo
mengi tofauti tunayokutana nayo katika mitandao na tamthilia .Katika
maeneo hayo niliyotaja upo uwezekano wa mtu kujiona sio mzuri wa kutosha
au hana uwezo wa kipesa wa kutosha au hapendwi kikamilifu. Hisia
zinazojitokeza wakati wa kuangalia tamthilia au kuona mambo fulani
kwenye mtandao zina nguvu za kumbadilisha mtu na tabia zake au mwenendo
wake.
Changamoto kwako ni kwamba jitahidi kuleta utamu wa kutosha katika
maeneo mengi zaidi ya uhusiano wako ili umpe sababu za kufurahia kuwa
nawe kama mpenzi.
Tahadhari kwako, uonapo mpenzi wako hataki kufanya mabadiliko mazuri
unayomweleza kuwa ni muhimu kwako jua kuwa hana penzi la kweli kwako.
Pamoja na hilo pale kuwa mpenzi wako anatamani mambo yanayohitaji uwezo
mkubwa wa kifedha kuliko uwezo wenu na hajali uboreshaji wa penzi bila
kuhusisha pesa basi tambua kuwa mwenzio ni mpenzi wa fedha na sio mpenzi
wako.
Nimuhimu katika uhusiano wa kimapenzi kuwepo kwa mfumo unaoleta utamu
tofauti tofauti. Hali ya kupata vitu au mambo tofauti huleta uchangamfu
na mshikamano ambao husaidia katika kukuza penzi kati ya watu wawili
wanaopendana.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >