DIWANI wa
Kata ya Sinza kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
jijini Dar, Renatus Pamba ‘Mr. Simple’ anadaiwa kumshushia kipigo denti
wa Chuo cha Ubaharia cha EMI jijini Dar, Alpha Mohamed (18) mpaka
kumsababishia kupoteza fahamu, Risasi Jumamosi limenyetishiwa.
Kwa
mujibu wa mjomba wa Alpha, Aboubakar Ramadhan, tukio hilo lilijiri
Agosti 29, mwaka huu nyumbani kwa diwani huyo, Sinza-White Inn ambapo
chanzo cha kipigo hicho kikidaiwa kuwa ni denti huyo kukutwa akipiga
stori na binti wa diwani aliyejulikana kwa jina la Mage.
Naye
Alpha mwenyewe akizungumzia tukio hilo kwa wanahabari wetu, alisema
siku hiyo usiku alipigiwa simu na Mage ya kumtaka wakutane ili amjuze
kilichojiri kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwa rafiki yao mmoja
(hakutajwa jina) kwa kuwa Mage hakwenda kwenye shughuli hiyo.
Denti
huyo aliendelea kuanika mambo kwamba, muda mchache baada ya kukutana na
Mage nje ya nyumba yao, alishangaa kumwona kijana mmoja anatokea na
kumwambia anaitwa na diwani huyo nyumbani kwake.
“Mwanzoni
nilisita wito huo lakini kwa vile sikuona kama nilikosea chochote
niliamua kwenda kwa diwani huyo lakini nikashangaa baada ya kuingia tu,
geti likafungwa na kuanza kupelekwa mzobemzobe mpaka sebuleni.“Nilimkuta
diwani pale sebuleni ambapo alianza kunishambulia kwa kunipiga fimbo za
fagio la njiti huku akisema natembea na Mage.
“Alinipiga
kuanzia saa 6 usiku hadi saa 9 maeneo ya kichwani, mgongoni na kifuani.
Hali ilivyokuwa mbaya sana, alikwenda chumbani kwake, nami nikajikaza
na kupiga simu nyumbani, lakini akaja, akazichukua simu zangu na
kuzizima huku akisisitiza kwamba atanipiga zaidi,” alisema Alpha.
Mjomba
wa Alpha yeye anasema baada ya kupokea simu ya anko wake huyo, hakujua
alikuwa katika nyumba gani zaidi ya kumsikia akiomba msaada, hivyo
walianza kumtafuta bila mafanikio kwa kuwa simu zake zote zilikuwa
hazipo hewani.
“Tulimtafuta
sana huku tukimpigia simu mara kwa mara. Ilipofika saa 9 usiku sasa,
kuna mtu akatutonya kwamba, Alpha alionekana akiingia kwa diwani huyo.
“Tulikwenda
kwa diwani, tukamkuta Alpha hajitambui hata kidogo. Mwili ulikuwa
umevimba, hasa sehemu za kichwani huku mguu wake mmoja
umeteguka.“Tulimchukua Alpha na kumpeleka Kituo cha Polisi Kijitonyama
‘Mabatini’ jijini Dar ambapo alipewa PF 3 kwa ajili ya kwenda kupata
matibabu, tulimpeleka Hospitali ya Palestina (Sinza).
“Pale,
madaktari walitwambia Alpha ameathirika zaidi ndani kwa ndani hasa
sehemu za kifuani na mgongoni,” alisema mjomba huyo.Naye mama mzazi wa
Alpha, Zanura Ramadhan alisema familia imefungua jalada la kesi lenye
Kumbukumbu Na. KN/RB/7748/2014 SHAMBULIO na wamefanikiwa kumkamata
kijana ambaye alimw ingiza kwa diwani siku ya tukio.
Diwani
huyo alipotafutwa kwa njia ya simu na gazeti hili na kusomewa mashitaka
yake, alisema na yeye amefungua mashitaka katika Kituo cha Polisi
Urafiki-Ubungo akimtuhumu Alpha kutaka kumbaka binti yake.
“Nikwambie
tu, yule Alpha alikuwa na binti yangu Mage usiku na alitaka kumbaka
hivyo nimefungua mashitaka na amekamatwa,” alisema diwani
huyo.Alipoulizwa kuhusu madai ya kumpiga Alpha, alikana na kusema
hakumpiga yeye bali msaidizi wake wa nyumbani (yule aliyemtuma akamwite
Alpha)
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >