Meneja
wa Diamond Platnumz, Babu Tale, anaamini kuwa fujo kwenye show ya
msanii wake huyo jijini Stuttgart nchini Ujerumani ilipangwa itokee.
“Sisi
tumefanya kazi na promoter wa Nigeria, wao wenyewe kwanza ile advertize
wakati wanamfuata Diamond hotelini hawakuwa wanaongea vizuri,” Tale
ameiambia Bongo5. “Mmoja ni Mnaigeria mmoja sijui ni Msenegali.Ilikuwa
imepangwa tu itokee, sometime vitu vingine vinapangwa tu ili vitokee,
yaani kwa sababu, sio tumepanga itokee, imepangwa itokee, vitu vingine
vinatokea for a reason,” ameongeza.
Kama
isingekuwa polisi wa Ujerumani leo tungekuwa tunaongea habari nyingine
kwakuwa Diamond Platnumz aliponea chupuchupu kushambuliwa na mashabiki
wenye hasira jijini Stuttgart nchini humo baada ya kuingia ukumbini saa
10 Alfajiri wakati mashabiki hao walikuwa wakimsubiri tangaa saa 4
usiku.
Show hiyo ilikuwa ifanyike usiku wa kuamkia Jumapili.
Katika
tukio hilo lililoandikwa na vyombo vya habari vya nchini Ujerumani,
promota wa show hiyo ambaye ni Mnaijeria alikimbia eneo la tukio na DJ
wa show kupewa kipondo cha paka mwizi.
Story kutoka Ujerumani inasema:
Majira
ya saa 10 alfajiri Mwanamuziki nyota wa Bongo Flava Nasib Abdul aka
Diamond Platnumz alijukuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na
polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya mashabiki waliokuwa na hasira
kuchoka kusubiri show. Mashabiki hao waliokuwa wamelipa tiketi kwa Euro
25 kama kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini
walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 alfajiri ndipo Diamond
alipopelekwa jukwaani na promota wake raia wa Nigeria anajiita kama
Britts Event.
Hapo
ndipo washabiki walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha
chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki Diamond na promota wake.
Kilichowakera zaid mashabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa
katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo
vya muziki ma-Djs walishambuliwa na wapo Hospitalini kwa sasa.
Moja
wa Djs hao alipoteza Laptop yake ,mwanadada DJ Flor alipatwa mshtuko wa
moyo na kukimbizwa hosptali. Mashabiki hao walimpa kipigo DJ Drazee
naye yupo hoi hospatali. Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio hilo
la aibu halijawahi kutokea,kuwa msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa
Ujerumani ni kitu cha hatari kwani mashabiki wa Ujerumani wanaheshimu
sana muda wao.
Mpaka
sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia
itamfungulia mashtaka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia
anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Kupitia Instagram Diamond alidai kusikitishwa na tukio hilo.
Kiukweli
nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS
iliyoandaa show ya Stuttgart Germany… kinachoniuma na kunisikitisha
zaidi ni jins watu walivyoamua kujitolea kuja kwa wingi kutusupport
vijana wao, halaf mwisho wa siku promoter anatupeleka wasanii kwenye
show saa kumi alfajiri… najua ni kiasi gani mmeumia na kuwa
disappointed… lakini naomba mtambue kuwa halikuwa ni kosa langu, coz
mimi ni mgeni tu, na nafata maelekezo ya promoter…hivyo nisingeweza
kujiamulia kuja muda ninaoutaka mimi….
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >