Maambukizi
haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalamu huitwa
simple cystitis au Bladder infection na maambukizi hayo yakitokea sehemu
za juu za mfumo wa mkojo huitwa pylonephritis au kidney infection.
Ugonjwa
huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia coli. Tatizo hili
husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida
ni kwenye utumbo mpana, na hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja
kubwa.
Lakini
watu wengine wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na
fangasi japokuwa kuna visababishi vingine vichache.Bakteria wa
Escherichia coli hawapo peke yao huambatana na waitwao staphylococcus,
saprophyti cus, pseudom onas, enterobacter n.k.
Maambukizi
katika njia ya mkojo lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo na si
pengine popote. Wapo wanawake wamekuwa wakiniuliza kuhusu tatizo la
kutokwa na uchafu ukeni na kudhani ni ugonjwa huu, huo ni ugonjwa
tofauti kabisa na huu tunaouchambua leo.
Tunapozungumzia
maambukizi katika njia ya mkojo, tuna maana ni kutoka eneo la nje la
utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo.Kama
maambukizi yako eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo, kitaalamu
huitwa Lower Urinary Tract Infect na ikihusisha eneo la juu ya kibofu
jina hubadilika na kuitwa, Upper Urinary Tract Infection.
Mara
nyingi maambukizi haya kwa wanawake hutokea wakati wa kujisafisha,
kutonawa vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani chafu. Matumizi ya
pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bakteria wa
asili wa eneo la uke na kukaribisha bakteria wanaosababisha maradhi
kuzaliana kwa wingi.
Upungufu
wa homoni ya kike iitwayo Oestrogen husababisha bakteria wasababishao
maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi.Matatizo haya ya
maambukizi licha ya kuwapata zaidi wanawake, huwakumba pia watoto wadogo
kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi, njia ya
mkojo na haja kubwa vipo jirani.
Watoto
wa kiume ambao hawajatahiriwa nao hupata maambukizi rahisi kutokana na
viungo vyao vya uzazi kuwa vifupi na wanaponawa maji yasiyo salama kwa
watoto wa kiume huwa rahisi bakteria kubaki katika ngozi inayoning’inia
(govi), hivyo kusababisha tatizo hili.
Lakini
pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambuzi
kutokana na sababu ambazo tumezitaja hapo juu ambapo pia ni rahisi kwao
kuambukizwa Ukimwi kama watafanya ngono zembe na ndiyo maana
tunasisitiza tohara kwa wanaume.
Maambukizi
yanayoshambulia mfumo wa mkojo zaidi ni bakteria wanaoishi katika mfumo
wa haja kubwa kusafiri kwa bahati mbaya na kujikita katika mfumo wa
mkojo. Bakteria wengine waambukizao njia ya mkojo ni wale watokanao na
magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia na trimonas na fangasi
wanapojamiiana bila kutumia kinga.
Ili
kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo, mara kwa mara, ni vema
kutumia kinga yaani kondomu na kwa mwanamke kila anapomaliza kufanya
ngono akojoe ili kuondoa bakteria walioingia au waliokaa katika tundu ya
mkojo wakisubiri kuingia.Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu,
unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya
kutosha huchangia tatizo hili.
Uwepo
wa mawe katika figo na mirija ya figo hata ndani ya kibofu pia ni
mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo.
Dalili
Baadhi ya dalili za mtu kuambukizwa bakteria katika njia ya mkojo kubwa ni maumivu wakati wa kukojoa, mkojo kuwa na rangi ya njano kupindukia na kuwa na harufu kali japokuwa siyo kila mwenye dalili hizo ana maambukizi katika njia ya mkojo au wengine huita UTI yaani urinary tract infection wana ugonjwa huu.

nyingine za maambukizi ni maumivu, kutokwa na usaha au majimaji wakati
wa kukojoa kabla au baada ya kukojoa kukiambatana na maumivu na kuhisi
moto wakati wa kukojoa mkojo.
Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Baadhi ya wanaume wakati mwingine hutokwa na majimaji katika njia ya mkojo wakati wa kujisaidia haja kubwa.
Wengine
wenye maambukizi hujikuta wakipata vichomi katika njia ya mkojo, au
kuhisi kuwashwa sehemu hiyo, kuumwa kiuno au tumbo na kadhalika.Mgonjwa
anaweza pia kukumbwa na homa kali mara kwa mara na mwili kuwa mchovu,
kwa watoto hupoteza hamu ya kula na mwili kuonesha kushoka.
Wagonjwa
wengine hupata maumivu kwenye kibofu cha mkojo ambapo husikia maumivu
ya chini ya tumbo usawa wa kitovu na huwa hayaishi.Matatizo haya ya
mfumo wa mkojo kama tulivyoona huko juu huwapata watu wote wanawake na
wanaume.
Watu
wenye matatizo haya kila wakipima huambiwa wana UTI. Kwa wanaume
huhisi hata nguvu za kiume kupungua na wanawake hupoteza hamu ya tendo
la ndoa.
WAJAWAZITO
Kwa wajawazito ugonjwa unaweza kuhatarisha maisha yao na mtoto aliye tumboni. Bakteria wanaweza kuingilia mfumo wa damu na kusababisha ama kwenda kusababisha madhara mengine kama vile shinikizo la damu kuwa kubwa kwenye figo na hata kusababisha ufanyaji wa kazi mbovu wa figo.

TIBA
Maambukizi katika njia ya mkojo hutibika kwa dawa mbalimbali za kisasa baada ya kufanyiwa vipimo na kuthibitika kuwa mgonjwa ana maambukizi hayo.Dawa ambazo anaweza kupewa ni kama vile Ciprofloxacin, Fosfomycin, Monurol, Furadantin, Sulfam ethoxazole, co-trimax, ampicillin, gentamicin na kadhalika lakini usitumie dawa yoyote bila kwanza kupata ushauri wa daktari.

Ushauri
Tunashauri kwa mwanamke kwamba epuka kujisafisha sehemu za siri na maji yarukayo kwa kasi, pia epuka kupaka marashi sehemu hizo, ama kutumia pedi zenye kemikali ya kukata harufu kwani hizo huua bakteria wa asili wa ukeni hali ambayo hukaribisha bakteria wa maradhi kuzaliana kwa wingi.

Ujisafishapo
baada ya kujisaidia anzia mbele kwenda nyuma kuepusha kuhamisha
bakteria walio eneo la haja kubwa kuingia njia ya mkojo.
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauriana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi.
Kwa wale walio katika kipindi cha ukomo wa hedhi, wanaweza kushauriana na daktari juu ya kutumia oestrogen ya ukeni ili kuwasaidia kujikinga na maambukizi.
Kwa
mwanaume maambukizi haya huathiri nguvu za kiume na kujipenyeza hadi
katika korodani na huathiri uzalishaji wa mbegu za kiume na kukufanya
uwe mgumba.
Maambukizi
ya njia ya mkojo huweza kusababisha matatizo ya tezi ya kiume
(prostate) kwani husababisha mrija wa mkojo kuziba, ama kutopitisha
mkojo vizuri na kuruhusu bakteria kujenga makazi. Hali hiyo ikitokea
mgonjwa lazima akamuone daktari ili awekewe mrija wa kutolea mkojo.
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Filed Under:
AFYA
Tuesday, 26 August 2014