Habari Kali
Loading...

STEVE NYERERE KIMENUKA TENA BONGO MOVIE

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Stori: Mwandishi Wetu
KIMENUKA! Klabu ya Bongo Movie Unity imedaiwa kuingia kwenye mpasuko mkubwa baada ya baadhi ya viongozi kutangaza kuachia ngazi kwa madai ya kuwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amechikichia mtonyo (fedha) mwingi wa klabu kwa masilahi yake.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilicho ndani ya klabu hiyo, juzikati viongozi wote wa klabu hiyo walikaa kikao kilichoitishwa na katibu wao, William Mtitu ambacho kilikuwa na lengo la kujadili jinsi ya kumwajibisha Steve Nyerere kwa madai hayo.
“Kuna fedha zilikuwa ni za maandalizi kwa ajili ya dua ya wasanii waliofariki dunia iliyofanyika Jumamosi.
“Pia kuna fedha nyingine zilitolewa hivi karibuni, walizitafuna akina Steve na baadhi ya viongozi, kilinuka kishenzi,” kilisema chanzo.
Katibu wa Bongo Muvi, William Mtitu.
Imeelezwa kuwa katika kikao hicho, hawakufikia muafaka kwani mtuhumiwa (Steve Nyerere) hakutokea pasipo kujulikana sababu za kutofika kwake.
Chanzo kiliendelea kudai, baada ya Steve kutoonekana, baadhi ya viongozi walisusa na kuondoka ambapo Katibu Msaidizi wa Bongo Movie, Devotha Mbaga na Mwekahazina Msaidizi, Sabrina Rupia ‘Cathy’ walitangaza kuachia ngazi endapo muafaka wa fedha zinazodaiwa kuliwa kinyemela hautapatikana.
Katibu Msaidizi wa Bongo Muvi, Devotha Mbaga.
“Bongo Movie ni kivumbi mtindo mmoja kwa sababu baadhi ya viongozi walio karibu na Steve wanadaiwa kuchikichia fedha nyingi tu, kitu ambacho kinazua mtafaruku kwani siyo mara ya kwanza,” kilisema chanzo hicho.
Mtitu ambaye ni katibu wa klabu hiyo, alipohojiwa kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kutokea ambapo alisema hata yeye amejipanga kuachia ngazi endapo hatapewa ufafanuzi wa fedha zinazodaiwa kuliwa na mwenyekiti wao.
Mwekahazina Msaidizi wa Bongo Muvi, Sabrina Rupia ‘Cathy’.
Steve Nyerere alipopigiwa simu kwa lengo la kuulizwa juu ya madai hayo, simu yake iliita bila majibu. Jitihada za kumtafuta zinaendelea.

BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >

TOA MAONI YAKO KUHUSU HABARI HII.. HAPA CHINI
Newer Posts Older Posts
© Copyright DONDOO ZA HABARI | Designed By Code Nirvana
Back To Top