Mwanamziki mashuhuri wa miondoko ya Hip-Hop hapa nchini, Roma Mkatoliki ametangaza rasmi kuachia ngoma zake mpya usiku wa Serengeti Fiesta-Tanga, katika uwanja wa Mkwakwani jumamosi hiii.
Mwanamuziki
huyo ambaye ni Mzaliwa wa Tanga na kipenzi cha wengi Jijiji hapo
amesema kwamba, ngoma hizo mpya zitasindikizwa na vibao kama vile Mr.
President, Pastor, Mathematics, 2013, KKK pamoja na ngoma mbalimbali
alizoshirikishwa na wasanii mbalimbali nje na ndani ya nchi.
Kauli mbiu ya Serengeti Fiesta mwaka huu ni “Sambaza upendo,”
Roma ambaye kwa sasa ni kati ya wanamuziki wakubwa hapa nchini, amekuwa akishiriki Serengeti Fiesta tangu mwaka 2007.
“Serengeti
Fiesta imenikuza kumuziki…nimeanza kupanda katika majukwaa ya Serengeti
fiesta miaka saba iliyopita na katika kipindi chote hicho nimekuwa
nikipata ushirikiano mkubwa sana kutoka kwa mashabiki zangu na
nnamshukuru Mungu kwamba sijawahi waangusha mashabiki zangu,” alisema Roma.
Roma ameishukuru Serengeti Fiesta kwa kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka pande zote hapa nchini. “Kupitia
Serengeti fiesta, imekuwa rahisi sana kwa wasanii kubadirishana
mawazo…kukutana na mashabiki zetu na vile vile kipata fursa mbalimbali
ambazo si rahisi kuzipata tukiwa mtaani.”
Roma
amewaasa wasanii na wadau wa muziki kutumia fursa vizuri fursa
zinazoambatana na serengeti fiesta ili kujinufaisha kimuziki na katika
maisha yao ya kawaida.
Wasanii
wengine watakao lipamba jukwaa la Serengeti Fiesta Tanga ni pamoja
Recho, Chege and temba, Alikiba, Ney wa mitego, Stamina, Jux, Linah,
Vanessa mdee, Mr Blue, Mkubwa na wanae, Ommy Dimpoz, Barnaba, Young
Killer na Madee.
Waandaaji
wa tamasha hili wamewahakikishia Wanatanga usalama wa hali ya juu na
kusema kwamba serikali ya Jiji la Mwanza iko makini na itatoa ulinzi
tangu mwanzo wa tamasha mpaka mwisho.
Baada
ya Tanga, burudani hili la nguvu litashuka katika mikoa mbalimbali kama
Musoma, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Singida, Dodoma, Moshi, Arusha,
Mtwara na Dar es salaam na hatimaye jijini Dar es Salaam ifikapo oktoba
18 mwaka huu.
Huu ni wakati wako wa kusambaza upendo sasa <<Bofya hapa kusambaza upendo>>
Ingia hapo juu kusambaza upendo
BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >
Ugandan socialite Zari is undeniably hot and Diamond Platnumz cannot be blamed for going kookoo for her, Besides her looks, she is also ambitious and rich. Born on 23rd of September 1980, Zari grew up in Jinja and after high school she moved Kampala where she performed karaoke in hang-outs. She later moved to London and acquired a diploma in cosmetology. She now lives in South Africa where she runs cosmetics shop while pursuing a career in music. She shared some of her never before seen photos from back in the day and she was still hot. Check her out: BONYEZA HAPA CHINI KUANGALIA MOVIE MPYA ZA BONGO== >



